Lindi (mji) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d +fr
d robot Adding: sv:Lindi
Mstari 19: Mstari 19:
[[nl:Lindi (stad)]]
[[nl:Lindi (stad)]]
[[pl:Lindi]]
[[pl:Lindi]]
[[sv:Lindi]]

Pitio la 22:28, 23 Oktoba 2007

Nyumba za Lindi

Lindi ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Lindi. Lindi iko mdomoni wa mto Lukuledi takriban 150 km kaskazini ya Mtwara mwambaoni wa Bahari Hindi. Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 41,549 [1].

Lindi ilikuwa kati ya miji ya Waswahili kwenye pwani la bahari. Mdomo wa Lukuledi ilikuwa bandari nzuri kwa ajili ya jahazi za Waswahili na pia kwa meli ndogo za zamani za ukoloni. Siku hizi haitoshi tena kwa meli kubwa.

Wakati wa ukoloni wa Wajerumani ilikuwa makao makuu ya kusini-mashariki ya Tanzania bara. Ilikuwa kituo cha Posta na pia cha kikosi na. 3 cha jeshi la Kijerumani. Ilibaki kitovu cha eneo chini ya Waingereza hadi kujengwa kwa bandari ya Mtawara. Mazao ya kibiashara yalikuwa hasa katani baadaye pia korosho.

Maendeleo ya Lindi ilikwama kutokana na hali mbaya za barabara amabazo hazikutunzwa vizuri wakati wa uhuru. Kuna matumaini ya kwamba mipango ya barabara ya lami ya Dar es Salaam - Mtwara itandelea baada ya kukamilika kwa daraja la mto Rufiji.