Kokain : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza war:Cocaina
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza new:कोकेन
Mstari 74: Mstari 74:
[[ms:Kokaina]]
[[ms:Kokaina]]
[[mzn:کوکائین]]
[[mzn:کوکائین]]
[[new:कोकेन]]
[[nl:Cocaïne]]
[[nl:Cocaïne]]
[[nn:Kokain]]
[[nn:Kokain]]

Pitio la 22:58, 7 Januari 2013

Unga wa Kokaini

Kokain ni dawa inayotengenezwa kutokana na majani ya kituka cha koka kinachostawi katika milima ya Amerika Kusini.

Umbo lake ni unga wa fuwele nyeupe. Ilianza kutumiwa kama dawa ya kutuliza maumivu. Ilitambuliwa kama dawa ya kulevya na kusambaa hivyo kimataifa.

Matumizi ya kiganga

Matibabu hutumia kokain kama dawa ya kutuliza maumiivu hasa wakati wa upasuaji mdomoni na puani.

Dawa la kulevya

Kiasili wenyeji wa Amerika Kusini walitafuna majani ya koka jinsi watu wa Afrika ya Mashariki na Arabia hutafuna majani ya miraa kwa jina lingine milungi. Kiasi cha dawa kinachopatikana katika majani hakileti ulevi bali hutuliza njaa na kuondoa uchovu.

Tangu 1860 wanakemia wameweza kuondoa dawa tupu kutoka majani kama unga. Kutokana matumizi ya tiba watu walianza kuonja dawa na kutambua uwezo wake wa kusababisha ndoto na hali ya kusikia raha. Ilionekana baadaye ya kwamba kokain ina tabia kama madawa mengine ya kulevya ya kuwa watu huzoea haraka kiasi cha kutawaliwa na dawa hawawezi kuiacha.

SIku hizi sehemu kubwa ya kokain hutegenezwa kwa matumizi ya dawa za kulevya. Bila masharti ya tiba matumizi yake ni marufuku lakini watu hupenda ndoto wanazopata kutokana na matumizi yake. Mara wakitawaliwa na dawa huona haja ya kurudiarudia matumizi yake. Kwa sababu hiyo biashara ya kokain inazalisha pesa nyingi hata kama ni marufuku.

Biashara

Majani ya Koka huvunwa hasa katika nchi za Kolombia, Peru na Bolivia. Maabara makubwa ya siri ya kuondoa dawa ya kokain tupu yapo hasa Kolombia.

Mabwana wa biashara hii ni matajiri wakitumia wanamigambo wanaotetea eneo la maabara dhidi ya polisi. Kiasi cha pesa inayopatikana kimetosha mara kwa mara kuhonga wanasiasa na maafisa wa juu serikalini na hivyo kupata nafasi ya kuendesha maabara pamoja na biashara inayotumia ndege ndogo zinazopeleka kokain nje ama moja kwa moja hadi Marekani au hadi visiwa vya Karibi ambako hufikishwa kwenye meli kwa biashara ya kimataifa.


Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kokain kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA