Kitenzi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d Roboti: Imeongeza ur:فعل
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza eml:Vêreb
Mstari 41: Mstari 41:
[[dsb:Werb]]
[[dsb:Werb]]
[[el:Ρήμα]]
[[el:Ρήμα]]
[[eml:Vêreb]]
[[en:Verb]]
[[en:Verb]]
[[eo:Verbo]]
[[eo:Verbo]]

Pitio la 10:43, 30 Desemba 2012

Kitenzi ni istalihi ya sarufi kwa maneno yanaotaja matendo kama vile kufanya, kwenda, kulala, kupiga, kuishi na kadhalika.

Lugha nyingi zinatumia vitenzi ingawa kuna pia lugha zisizoweka tofauti kati ya vitenzi na majina.

Kwa Kiswahili kila kitenzi kina shina yake inayobeba maana yake. Mfano: ku-fanya ambamo "fanya" ni shina; kiambishi awali "ku-" ni alama ya aina ya neno yaani kitenzi chenyewe.

Ndani ya shina kuna tofauti kati ya mzizi wa neno "fany" na kiambishi tamati ambacho ni silabi "a".

Mzizi wa kitenzi mwenyewe haubadiliki wakati wowote kitenzi kitaponyambuliwa katika kauli yoyote iwayo.

Vitenzi kwa Kiswahili hupokea viambishi mbalimbali vinavyoeleza kwa undani zaidi maana ya matumizi ya neno. Viambishi awali ni silabi zilizopo mbele ya mzizi na viambishi tamati ni silabi zilivyopo baada ya mzizi wa kitenzi.

Viambishi awali vinaweza kutaja:

  • nafsi ya mtenda - ni nani au nani anayetenda na hivi ni silabi ni /u / a upande wa umoja na tu / m / wa upande wa uwingi mtawalia katika hali yakinishi na "si"/ "hu"/"ha" kuwa vikanushi vya viambishi vya nafsi za mtenda- umoja na "hatu"/"ham"/"hawa" kuwa vikanushi vya viambishi vya nafsi za mtenda-wingi .
  • njeo au wakati - kama tendo linatokea sasa au lilitokea wakati uliopita au litatokea wakati ujao ; mifano ni silabi za a pamoja na na kwa wakati wa kisasa, li kwa wakati uliopita na ta kwa wakati ujao katika hali yakinishi.

Viambishi tamani vinaweza kupanusha au kubadilisha maana ya kimsingi ya mzizi wa neno. Mifano ni kimbi-a, kimbi-lia, kimbili-ana, kimbi-za, kimbi-zana, kimbi-liwa.