Dameski : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza pa:ਦਮਸ਼ਕ
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza or:ଡାମାସକସ
Mstari 181: Mstari 181:
[[nov:Damaskus]]
[[nov:Damaskus]]
[[oc:Damasc]]
[[oc:Damasc]]
[[or:ଡାମାସକସ]]
[[os:Дамаск]]
[[os:Дамаск]]
[[pa:ਦਮਸ਼ਕ]]
[[pa:ਦਮਸ਼ਕ]]

Pitio la 12:33, 22 Desemba 2012

Dameski - دمشق
Damaskus bei Nacht, fotografiert vom Dschabal Qasiun aus; Die grünen Punkte sind Minarette
Habari za msingi
Mkoa Dameski
Anwani ya kijiografia 33°30'35" N; 36°18'33"E
Kimo 690 m juu ya UB
Eneo 105 km²
Wakazi 1.580.909 (2006)
Msongamano wa watu watu 15.056/km²
Simu 963 (nchi), 11 (mji)
Lage

Dameski (pia: Damasko, Damaskus, Damascus; kiar.: دمشق "dimashk") ni mji mkuu wa Syria, pia ni mji mkubwa wa nchi hiyo wenye wakazi milioni 4.5.

Dameski ni kati ya miji ya kale kabisa duniani iliyoendelea kukaliwa mahali palepale: inaaminiwa imekaliwa tangu miaka 8,000 au zaidi.

Jina

Nchini mji huitwa mara nyingi الشام ("ash-shām"). Jina hilo latumiwa na Waarabu wengine pia kwa nchi yote ya Syria. Kihistoria "Shamu" ilikuwa jina la nchi yote upande wa mashariki wa bahari ya Mediteranea.

Jiografia

Dameski iko takriban kilometa 80 mashariki ya pwani ya Mediteranea na kilometa 30 kutoka mpaka kati ya Syria na Lebanoni kando ya mto Barada. Iko kwenye kimo cha mita 680 juu ya UB.

Upande wa magharibi ni milima ya Libanoni ndogo inayozuia mawingu yenye mvua kufika kutoka Mediteranea. Upande wa mashariki inaanza jangwa.

Historia

Akiolojia imeonyesha makazi ya kibinadamu katika eneo la Dameski tangu milenia ya 5 KK.

Utawala wa Misri

Mji ulitajwa mara ya kwanza kimaandishi kwa jina la "Tamasqu" (tmsq) katika taarifa za Misri ya Kale wakati wa Farao Thutmosis III (1479 KK - 1425 KK). Ilikuwa chini ya utawala wa Misri hadi mnamo mwaka 1100 KK.

Ufalme wa Aramu

Tangu 1000 KK mji ukawa kitovu cha ufalme wa Aramu-Dameski unaotajwa pia mara nyingi katika Biblia. Baada ya kushindana mara nyingi na Israeli ulikwisha katika vita dhidi ya Assyria mwaka 732 KK.

Utawala wa Babeli, Uajemi, Wagiriki na Roma

Assyria ilishindwa na Nebukadreza II wa Babeli na Dameski ikawa sehemu ya milki ya pili ya Babeli tangu 572 KK.

Mwaka 538 KK Uajemi iliPOchukua nafasi ya Babeli Dameski ikawa mji mkuu wa jimbo la Syria.

Kufika kwa Aleksanda Mkuu tangu 333 KK kulibadilisha siasa ya Mashariki ya Kati na Dameski ikawa sehemu ya dunia ya Kigiriki.

Wafuasi wa Aleksander waliendelea kushindania mji baadaye: mara ukawa upande wa Waptolemayo (Misri) mara upande wa Waseleukido.

Tangu 64 KK Dola la Roma likaingia Shamu. Dameski ikawa mji mkuu wa jimbo la Kiroma likakua na kustawi. Mpangilio wa Waroma yameonekana hadi leo katika mji wa Kale wa Dameski hata kama majengo ya nyakati zile yamefichwa mita 5 chini ya uwiano wa mji wa leo. Barabara ya decumanus ya Kiroma, ambayo imetajwa katika Biblia kama "barabara iliyonyoka" au "barabara iitwayo Nyofu" (Mdo 9,11), inaoonekana hadi leo.

Kaisari Theodosio I alijenga kanisa kubwa la Mt. Yohane lililotunza kichwa cha Yohane Mbatizaji.

Maziara ya kichwa cha Yohane Mbatizaji ndani ya msikiti wa Muawiya inatembelewa na Waislamu na Wakristo vilevile

.

Waarabu na Waosmani

Dameski ilivamiwa na jeshi la Waarabu Waislamu chini ya khalifa Umar I mwaka 636 B.K.. Kanisa la Mt. Yohane likabadilihswa kuwa msikiti mkuu. Baada ya ushindi wa Muawiyya mwaka 661 juu ya Hussain ibn Ali alichukua cheo cha khalifa akikaa Dameski. Hivyo mji ukawa mji mkuu wa milki ya Wamuawiya iliyotawala nchi kati ya Hispania hadi milango ya China.

Khalifa wa mwisho wa Wamuawiya Marwan II alihamisha makao yake kwenda Haran katika Mesopotamia ya kaskazini. Marwan alishindwa baadaye na Abu al-`Abbās `Abdu'llāh as-Saffāh aliyeanzisha utawala wa makhalifa Waabbasi na kupeleka mji mkuu Baghdad. Dameski haikurudishwa tena umuhimu na heshima jinsi ilivyokuwa wakati wa Wamuawiya.

Iliendelea kuwa maKao makuu ya kijimbo tu, isipokuwa kwa vipindi vifupi ilipokuwa mji huru tena pasipokuwa na utawala wenye nguvu ya makhalifa.

Salah-ad-Din aliweka mji tena chini ya utawala wa Misri hadi 1516. Mnamo 1400 Dameski ilivamiwa na kuharibiwa kabisa na Timur.

Utawala wa Milki ya Waturuki Waosmani ulianza 1516 ukaendelea hadi 1918. Dameski ilijikuta tena mbali na mji mkuu wa milki huko Istanbul. Ilikuwa na umuhimu fulani kwa sababu misafara ya hija kwenda Maka ilianzia Dameski.

Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivunja milki ya Waosmani ikaleta utawala wa Ufaransa katika Syria.

Mji Mkuu wa Syria huru

Uhuru wa Syria mwaka 1946 ulifanya Dameski mji mkuu wa nchi huru. Tangu hapo Dameski ikakua sana ikawa mji wa viwanda na biashara.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Dameski kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.