Uganda : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (Roboti: Imeongeza zh-classical:烏干達
d r2.6.2) (Robot: Modifying pa:ਯੂਗਾਂਡਾ to pa:ਯੁਗਾਂਡਾ
Mstari 226: Mstari 226:
[[or:ଉଗାଣ୍ଡା]]
[[or:ଉଗାଣ୍ଡା]]
[[os:Угандæ]]
[[os:Угандæ]]
[[pa:ਯੂਗਾਂਡਾ]]
[[pa:ਯੁਗਾਂਡਾ]]
[[pam:Uganda]]
[[pam:Uganda]]
[[pap:Uganda]]
[[pap:Uganda]]

Pitio la 17:18, 21 Desemba 2012

Republic of Uganda
Jamhuri ya Uganda
Bendera ya Uganda Nembo ya Uganda
(Bendera ya Uganda) (Nembo ya Uganda)

Wito: For God and My Country
(Kiing. ya „Kwa ajili ya Mungu na Taifa langu“)

Lugha rasmi Kiingereza, kiswahili
Mji Mkuu Kampala
Aina ya Serikali Jamhuri
Raisi Yoweri Kaguta Museveni
Waziri Mkuu Apolo Nsibambi
Eneo 241.548 km²
Wakazi 27.269.482 (Julai 2005)
Wakazi kwa km² 113
Uhuru 9. Oktoba 1962
Pesa Shillingi ya Uganda
Wakati UTC+3
Wimbo ya Taifa Oh Uganda, Land of Beauty
Namba ya simu ya kimataifa +256


Uganda ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa Magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini.

Uganda inamiliki sehemu kubwa ya ziwa la Viktoria Nyanza ikipakana hapo na Kenya na Tanzania.

Jina la Uganda lina asili yake katika ufalme wa Buganda uliopo katika kusini ya nchi pamoja na mji mkuu Kampala.

Uganda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Map of Uganda

Jiografia

Tazama pia Wilaya za Uganda na Miji ya Uganda.`

Uso wa nchi umepata tabia yake kutokana na maziwa makubwa, mito, milima ya juu na tambarare. Upande wa kusini nchi imepakana na Ziwa Nyanza Viktoria ambaya ni ziwa kubwa la Afrika. Maziwa makubwa mengine upanda wa magharibi ni Ziwa Albert na Ziwa Edward. Mto mkubwa ni Nile inayopita nchi yote kati ya Ziwa Viktoria hadi Ziwa Albert na kuendelea hadi mpaka wa Sudani ikiitwa mwanzoni Nile ya Viktoria na baadaye Nile ya Albert.

Milima ya Ruwenzori ni kati ya milima mikubwa kabisa ya Afrika baada ya Kilimanjaro na Mlima Kenya.

Kusini kuna ardhi yenye rutuba na kilimo kinastawi vizuri.

Historia

Eneo la Uganda limeona uhamiaji wa vikundi vingi. Kusini iliingiliwa hasa na wakulima Wabantu. Kaskazini iliona kufika kwa Waniloti kwa mfano Waluo na baadaye Karimojong.

Tangu karne ya 15 himaya mbalimbali zilianza kujengwa na kati ya hizo ni hasa falme za Buganda, Ankole, Bunyoro Toro zilizoendelea kuwa muhimu hadi kuja kwa ukoloni na kwa kiasi fulani kama urithi wa kiutamaduni hata katika Uganda ya kisasa.

Karne ya 19 iliona kufika kwanza kwa Waarabu na baadaye kwa Wazungu. Kila mmoja alileta dini yake yaani Uislamu na Ukristo wa Kikatoliki au Kianglikana.

Katika mashindano juu ya Afrika ya Kati Waingereza walifaulu kwa kushindana na Waarabu, Wafaransa na Wajerumani. Walienea kwa mapatano na Buganda wakisaidiana kukomesha upinzani kutoka falme za jirani.

Baadaye Waingereza walikuwa na nguvu ya kutosha kuamua hata mambo ya ndani ya Buganda wakatangaza Uganda wote kuwa nchi lindwa tangu 1894.

Uganda ilipata uhuru wake tarehe 9 Oktoba 1962 kwa katiba ya jamhuri yenye serikali ya kibunge. Rais wa kwanza alikuwa Kabaka Sir Edward Mutesa II na waziri mkuu Milton Obote.

Mwaka 1967 Obote alibadilisha katiba akamfukuza Kabaka nchini.

Serikali ya Obote ilipinduliwa na mkuu wa jeshi Idi Amini mwaka 1971. Utawala wake ulikuwa kipindi cha udikteta ulioharibu uchumi wa nchi na misingi ya dola. Takriban watu 300,000 waliuawa chini ya Amin ama wapinzani wa siasa yake au watu wa makabila yaliyotazamiwa kuwa maadui wa serikali. Raia wenye asili ya Kiasia walifukuzwa katika nchi na mali yao yote kutwaliwa na serikali.

Mwaka 1978 vikosi vya jeshi la Uganda viliingia Tanzania na kuvamia maeneo ya mpakani kaskazini ya mto Kagera. Mwaka 1979 Tanzania ilijibu kwa njia ya vita na jeshi lake pamoja na wapinzani wa Uganda walishinda jeshi la Amin na kumfukuza dikteta nchini.

Rais wa baadaye Yoweri Museveni alikuwako kati ya wanamigambo waliosaidiana na Watanzania.

Uchaguzi wa 1980 ulimrudisha Milton Obote serikalini aliyeanzisha upya udikteta na kuua watu ovyo. Wapinzani wake wakiongozwa na Museveni walirudi porini wakashika silaha. Katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kundi la Museveni likashinda na kutwaa serikali tangu mwaka 1986.

Museveni alichaguliwa rais katika kura bila vyama vya upinzani za 1996 na 2001.

Mwaka 2005 ulikuwa na uchaguzi wa vyama vingi wa kwanza. Museveni alipata kibali cha bunge kwa badiliko la katiba lililomruhusu kugombea urais tena mwaka 2006 akachaguliwa mara ya tatu.

Miji ya Uganda

Angalia pia

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira