Kitabu cha Hosea : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2+) (Roboti: Imebadilisha: vep:Osijan kirj
d r2.6.2) (Robot: Modifying yo:Ìwé Hosea to yo:Ìwé Hóséà
Mstari 81: Mstari 81:
[[uk:Книга пророка Осії]]
[[uk:Книга пророка Осії]]
[[vep:Osijan kirj]]
[[vep:Osijan kirj]]
[[yo:Ìwé Hosea]]
[[yo:Ìwé Hóséà]]
[[zh:何西阿書]]
[[zh:何西阿書]]

Pitio la 22:13, 11 Desemba 2012

Kitabu cha Hosea ni kimoja kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), na hivyo pia vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kwa kuwa kina sura 14 tu, kimepangwa tangu zamani za kale kati ya vitabu 12 vya Manabii Wadogo.

Hata hivyo umuhimu wake katika maendeleo ya Ufunuo wa Mungu kwa Israeli ni mkubwa, kwa jinsi kilivyoathiri vitabu vilivyofuata hadi Kitabu cha Ufunuo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo hayo.

Muda wa unabii wa Hosea

Nabii Hosea alitokea Ufalme wa Kaskazini ambapo alifanya kazi kuanzia miaka ya mwisho ya utawala wa Yerobohamu II (786 K.K. -746 K.K.) hadi karibu na maangamizi ya mwaka 722 K.K. ambayo aliyatabiri kutokana na uasi wa kidini wa watu wake.

Wakati huohuo walifanya kazi pia Amosi, Kaskazini halafu Isaya katika Ufalme wa Kusini (Yuda).

Mada kuu

Hosea alitangaza hasa upendo wa Mungu kwa taifa lake. Adhabu zenyewe zilizotabiriwa zinaelezwa kuwa zimetokana na upendo huo wenye wivu ambao unalenga kuwarudisha Waisraeli katika upendo wa kiuchumba.

Hosea alikuwa wa kwanza kumfananisha Mungu na mume mwaminifu wa mwanamke malaya.

Maisha ya nabii mwenyewe yalikuwa na tabu ya namna hiyo ili yawe kwa wote kielelezo che uhusiano kati ya Mungu na watu wake.

Alidai Waisraeli wawe waaminifu kwa Mungu pekee, pamoja na kusisitiza kuwa dini haiwezi kuishia katika ibada zisizohuishwa na upendo, la sivyo wataangamia.

Muhtasari

Mwanzoni mwa kitabu, Hosea aliagizwa na Mungu amuoe kahaba atakayemzalia wanaharamu anayewakilisha taifa la Israeli lililoabudu miungu mingine pia kama asili ya ustawi wake na kutegemea mbinu za kisiasa ili kujidumisha salama.

Kwa kuwa hawakumtegemea Mungu wao, Hosea aliwatabiria Waisraeli watapelekwa uhamishoni huko Ashuru.

Kama vile mke wa Hosea alivyoweza kujirekebisha, hivyo hata Israeli ikitubu itaokoka na kufaidika na baraka za Mungu.

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Viungo vya Nje