Methodio : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.8) (Roboti: Imeongeza eo:Metodo (nomo)
Mstari 44: Mstari 44:
[[cs:Svatý Metoděj]]
[[cs:Svatý Metoděj]]
[[de:Method von Saloniki]]
[[de:Method von Saloniki]]
[[eo:Metodo (nomo)]]
[[fy:Metoadius]]
[[fy:Metoadius]]
[[hu:Szent Metód]]
[[hu:Szent Metód]]

Pitio la 10:00, 7 Desemba 2012

Ndugu Sirili na Methodi mitume wa Waslavoni.

Methodio wa Thesalonike (kwa Kigiriki: Μεθόδιος - Methodios; kwa Kislavoni: Мефодии) * mnamo 826 katika mji wa Thesalonike; † 6 Aprili 885 huko Velehrad Moravia (Ucheki) alikuwa mmisionari wa Waslavoni wa Ulaya ya kusini-mashariki katika karne ya 9 BK akishirikiana na kaka yake Kyrilo.

Alizaliwa kwa jina la "Mikaeli" mjini Thesalonike au Saloniki katika Ugiriki ya kaskazini wakati wa enzi za Dola la Bizanti kama mtoto wa Leontios askari wa Kibizanti na Maria mke wake Mslavoni.

Methodio alijiunga na wamonaki akawa msimamizi wa monasteri.

Mnamo mwaka 861 Rastislav mtawala wa Moravia alitafuta njia ya kuimarisha utawala wake kwa kupunguza athira ya majirani wake Wafrankoni wa Mashariki (au Wajerumani jinsi walivyoitwa baadaye). Wajerumani waliwahi kuleta imani ya Kikristo Moravia. Ratislav alitaka kuwa na maaskofu na mapadri wasio Wajerumani. Hivyo alimwomba Kaisari wa Bizanti kutuma wamisionari kwake kutoka huko.

Kaisari Michael III Konstantino wa Konstantinopoli alituma ndugu Kyrilo na Methodio kwa sababu wote wawili walikuwa watu wa Kanisa wenye elimu nzuri wakijua lugha ya Kislavoni tangu utoto.

Baadaya ya kifo cha Kyrilo Methodio aliendelea kuwa askofu na mwalimu wa kikristo mwenye athira kubwa katiy a Waslavoni. Tangu 883 alitafsiri Biblia katika lugha ya Kisalvoni na kuweka misingi ya liturgia ya Kislavoni.

Anasifiwa kama mmisionari aliyefaulu kuunganisha ujumbe wa Ukristo na utamaduni wa Waslavoni.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: