Mnara wa Babeli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza wuu:巴別塔
Mstari 95: Mstari 95:
[[ur:بابل کا برج]]
[[ur:بابل کا برج]]
[[vi:Tháp Babel]]
[[vi:Tháp Babel]]
[[wuu:巴別塔]]
[[yo:Ilé-Ìṣọ́ Bábẹ́lì]]
[[yo:Ilé-Ìṣọ́ Bábẹ́lì]]
[[zh:巴別塔]]
[[zh:巴別塔]]

Pitio la 14:47, 20 Novemba 2012

Mnara wa Babeli ulichorwa mara nyingi na wasanii kama katika picha hii ya Pieter Brueghel Mzee.

Mnara wa Babeli ni jengo kubwa linalotajwa katika Biblia kwenye Kitabu cha Mwanzo 11:1-9. Kufuatana na taarifa hii mnara ulijengwa pamoja na mji wa Babeli kama kilele chake.

Katika mapokeo ya Mwanzo 11 Babeli ulikuwa mji wa kwanza uliojengwa baada ya gharika kuu. Binadamu waliamua kuwa na jengo kubwa katika mji na kilele chake kifike mbinguni. Mpango huu haukumpendeza Mungu aliyechanganya lugha ya watu ambao hivyo walilazimika kuachana baadaye bila ya kukamilisha mnara wao.

Kihistoria si wazi ni kipindi gani kinachoangaliwa katika simulizi la Mwanzo 11. Inaonekana ya kwamba wasimulizi walikuwa na habari za piramidi au zigurat kubwa zilizokuwepo Babeli na penginepo katika Mesopotamia.

Maelezo ya kiimani

Simulizi limechukuliwa kwa njia mbalimbali katika mapokeo ya Wayahudi na Wakristo.

Moja ni kwamba hadithi hiyo inafundisha kwamba kiburi na dhambi kwa jumla vinatenganisha watu wasiweze kuelewana wala kuishi pamoja. Isipokuwa si wazi dhambi ni ipi.

Kwa Wakristo Mwinjili Luka katika kitabu cha Matendo ya Mitume kwenye Agano Jipya alitumia mfano wa mnara kama kinyume cha matokeo ya siku ya Pentekoste ambako watu kutoka lugha mbalimbali walipata kuelewana kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Simulizi la Mwanzo 11, 1-9

11,1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
5 BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.
6 BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
8 Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.
9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: