Nchi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.4) (Roboti: Imeondoa: pl:Pays
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza new:देय्
Mstari 99: Mstari 99:
[[nds:Land]]
[[nds:Land]]
[[ne:देश]]
[[ne:देश]]
[[new:देय्]]
[[nl:Land (geografie)]]
[[nl:Land (geografie)]]
[[pam:Country]]
[[pam:Country]]

Pitio la 17:47, 28 Oktoba 2012

Ramani ya kitopografia ya Ulaya
Ramani sawa na ya hapo juu, lakini ikionyesha mataifa huru ambayo yamekubaliwa na Umoja wa Mataifa badala ya topografia

Katika jiografia, nchi ni kanda au eneo la kijiografia. Neno hili mara nyingi hutumiwa kwa kitengo cha kisiasa au eneo la taifa huru, au kwa eneo ndogo la kijiografia, zamani likiwa kitengo cha kisiasa. Kwa kawaida, lakini si kila wakati, nchi inasanjari na eneo huru na kuhusishwa na taifa au serikali.

Nchi pia inaweza kumaanisha sehemu za mashambani, kinyume na mji.

Katika matumizi ya kawaida, neno nchi hutumiwa katika maana ya mataifa na majimbo, kukiwa na fasili tofauti. Katika baadhi ya matumizi inatumiwa kuashiria majimbo na vitengo vingine vya kisiasa,[1][2][3] ilihali katika mengine inahusu tu majimbo [4]. Si nadra kwa taarifa ya ujumla au machapisho ya takwimu kuchukua ufafanuzi mpana wa neno hili kwa makusudi kama maonyesho na ulinganifu.[5][6][7][8][9]

Baadhi ya vitengo vya kijiografia, ambavyo zamani vilikuwa majimbo yanayojisimamia, vinaaminika na kujulikana bado kama nchi kwa kawaida kama vile Uingereza, Scotland na Wales - katika Ufalme Ulioungana (Ufalme wa Muungano).[10][11][12][13] Kihistoria, nchi za Umoja wa zamani wa Kisovyeti na Yugoslavia zilikuwa zingine. Majimbo ya zamani kama Bavaria (sasa ni sehemu ya Ujerumani) na Piedmont (sasa ni sehemu ya Italia) yangekuwa si kawaida kujulikana kama "nchi" katika Kiingereza ya kisasa. Kiwango cha uhuru wa nchi zisizo mataifa inatofautiana sana. Baadhi ni mali ya mataifa, kwani mataifa kadhaa yana maeneo yanayoyategemea ya ng'ambo (kama vile Visiwa vya Virgin vya Uingereza, Saint Pierre na Miquelon, na Samoa ya Marekani), yenye eneo na raia tofauti na yao wenyewe. Maeneo tegemezi kama haya wakati mwingine yanatajwa pamoja na mataifa huru kwenye orodha ya nchi, na yanaweza kuchukuliwa kama "nchi ya asili" katika biashara ya kimataifa, kama Hong Kong ilivyo. Baadhi ya nchi zimegawanywa kati ya majimbo kadhaa, kama vile Korea na Kurdistan.

Asili na maendeleo ya neno

Neno nchi imeendelea kutoka neno contra, ya Kilatini maana yake "dhidi", inayotumika katika maana ya "inayolalia, au kinyume na, mtazamo", yaani hali ya ardhi ilivyoenea nje kwa mtazamo. Kutoka kwa hili likaja neno la Mwishoni mwa Kilatini contrata , ambalo lilikuja kuwa contrada ya Kiitaliano ya kisasa. Neno hili linaonekana katika Kiingereza ya Enzi za Kati kutoka karne ya 13, tayari katika hisia mbalimbali.[14]

Katika Kiingereza neno hili kwa zaidi limehusishwa na vitengo vya kisiasa, ili maana moja, inayohusishwa na nakala isiyo sawa - "nchi" - sasa ni kisawe kwa taifa, au taifa lililokuwa huru zamani, katika maana ya eneo huru linalojitegemea.[15] Maeneo madogo sana kuliko tawala ya kisiasa yanaweza kuitwa kwa majina kama Nchi ya Magharibi nchini Uingereza, " nchi kubwa "(inayotumika katika mazingira mbalimbali ya Magharibi ya Marekani, "nchi ya makaa"(inayotumika katika ya maeneo ya Marekani na kwingineko) na maneno mengine mengi.[16]

Maneno sawa katika lugha ya Kifaransa na Kirumi (pays na variants) hayajabeba mchakato wa kutambuliwa na majimbo ya kisiasa yaliyo huru kama "nchi" katika Kiingereza, na katika mengi ya nchi za Ulaya maneno haya hutumiwa kwa vitengo vidogo vya maeneo ya kitaifa, kama katika Länder ya Kijerumani, vilevile kama neno lisilo rasmi kwa jimbo au taifa huru. Ufaransa ina "pays" nyingi sana ambazo zinatambuliwa rasmi katika kiwango fulani, na ni aidha kanda ya asili, kama Pays de Bray, au zinaashiria miungano ya kale ya kisiasa au kiuchumi, kama Pays de la Loire. Wakati huo huo Wales, Marekani, na Brazili pia ni "pays" katika matamshi ya kila siku Kifaransa.

Makala ya "nchi" inaweza kupatikana katika lugha ya Kifaransa ya kisasa kama contrée , yenye msingi katika neno cuntrée katika Kifaransa ya Enzi za Zamani [16] ambayo inatumika sawa na neno "pays" kuelezea mikoa na miungano, lakini pia inaweza kutumika kuelezea eneo la kisiasa katika baadhi ya matumizi fulani. Contrada ya Kiitaliano ya kisasa ni neno yenye maana yake ikiwa tofauti humu nchini, lakini kwa kawaida ikimaanisha kata au mgawanyiko mdogo sawa wa mji, au kijiji au hamlet mashambani.

Angalia Pia

Marejeo

  1. Acts Interpretation Act 1901 - Sect 22: Meaning of certain words. Australasian Legal Information Institute. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  2. The Kwet Koe v Minister for Immigration & Ethnic Affairs & Ors [1997] FCA 912 (8 September 1997). Australasian Legal Information Institute. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  3. U.S. Department of State Foreign Affairs Manual Volume 2—General (PDF). United States Department of State. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  4. Rosenberg, Matt. Geography: Country, State, and Nation. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  5. Greenland Country Information. Countryreports.org. Iliwekwa mnamo 2008-05-28. The World Factbook - Rank Order - Exports. Central Intelligence Agency. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  6. Index of Economic Freedom. The Heritage Foundation. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  7. Index of Economic Freedom - Top 10 Countries. The Heritage Foundation. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  8. Asia-Pacific (Region A) Economic Information (PDF). The Heritage Foundation. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  9. Subjective well-being in 97 countries (PDF). University of Michigan. Iliwekwa mnamo 2008-11-12.
  10. Legal Research Guide: United Kingdom - Law Library of Congress (Library of Cong. Library of Congress website. Library of Congress (2009-07-23). Iliwekwa mnamo 2009-09-22. “The United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland is the collective name of four countries, England, Wales, Scotland and Northern Ireland. The four separate countries were united under a single Parliament through a series of Acts of Union.”
  11. countries within a country:number10.gov.uk. 10 Downing Street website. 10 Downing Street (2003-01-10). Iliwekwa mnamo 2009-09-22. “The United Kingdom is made up of four countries: England, Scotland, Wales and Northern Ireland.”
  12. Commonwealth Secretariat - Geography. Commonwealth Secretariat website. Commonwealth Secretariat (2009-09-22). Iliwekwa mnamo 2009-09-22. “The United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland (UK) is a union of four countries: England, Scotland, Wales and Northern Ireland.”
  13. Travelling Europe - United Kingdom. European Youth Portal. European Commission (2009-06-29). Iliwekwa mnamo 2009-09-22. “The United Kingdom is made up of four countries: England, Northern Ireland, Scotland and Wales.”
  14. John Simpson, Edmund Weiner, ed. "country". Oxford English Dictionary (1971 compact ed.). Oxford, England: Oxford University Press. ISBN 0198611862 .
  15. [30] ^ OED, Nchi
  16. 16.0 16.1 John Simpson, Edmund Weiner, ed. Oxford English Dictionary (1971 compact ed.). Oxford, England: Oxford University Press. ISBN 0198611862 .

Viungo vya nje

Ufalme wa Muungano:Країни світу