Petro Kanisio : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.5) (roboti Nyongeza: eu:Pedro Canisio
d r2.7.2+) (Roboti: Imeongeza hr:Petar Kanizije
Mstari 61: Mstari 61:
[[fi:Petrus Canisius]]
[[fi:Petrus Canisius]]
[[fr:Pierre Canisius]]
[[fr:Pierre Canisius]]
[[hr:Petar Kanizije]]
[[hu:Canisius Szent Péter]]
[[hu:Canisius Szent Péter]]
[[id:Petrus Kanisius]]
[[id:Petrus Kanisius]]

Pitio la 23:59, 7 Oktoba 2012

Sura ya Petro iliyochongwa katika shaba mwaka 1600 hivi
Sura ya Petro iliyochongwa katika shaba mwaka 1600 hivi

Petro Kanisio (kwa Kiholanzi Pieter Kanijs, au Kanisius, au Kanijs, au Kanîs) alizaliwa Nijmegen (leo nchini Uholanzi) tarehe 8 Mei 1521 akafariki Freiburg (Uswisi) tarehe 21 Desemba 1597.

Alikuwa mtawa wa kwanza wa Shirika la Yesu kutoka Uholanzi na kiongozi wa kwanza wa kanda ya Ujerumani, mwanateolojia na padri wa Kanisa Katoliki.

Alitangazwa na Papa Pius IX kuwa mwenye heri mwaka 1869, halafu na Papa Pius XI kuwa mtakatifu na mwalimu wa Kanisa mwaka 1925.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake 21 Desemba, lakini Ujerumani tarehe 27 Aprili.

Kwa kawaida Petro Kanisio anachorwa akiwa na fuvu la kichwa, Yesu msulubiwa na katekisimu.

Maisha

Petro alizaliwa na meya wa Nijmegen, katika Dola takatifu la Roma.

Tarehe 8 Mei 1543, siku ya kutimiza miaka 22, alikuwa Mholanzi wa kwanza kujiunga na Shirika la Yesu na mwanashirika wa nane.

Alipofanywa mkuu wa kwanza wa kanda ya Ujerumani ya Wajesuiti, alitoa mchango mkubwa katika urekebisho wa Kikatoliki hata Papa Leo XIII alimtaja "mtume wa pili wa Ujerumani" baada ya Mt. Bonifas.

Mnamo Januari 1547 aliitwa na askofu wa Augsburg, kardinali Otto von Waldburg, ashiriki mtaguso wa Trento.

Kanisio alikuwa gombera na mwalimu wa teolojia katika chuo kikuu cha Ingolstadt, pia aliongoza jimbo la Wien kati ya 1554 na 1555, ingawa alikataa kuwa askofu ili aweze kuendelea na utume wake huko na huko.

Aliheshimiwa kwa adabu yake, akikwepa kuita Waprotestanti "wazushi" katika mahubiri yake.

Katekisimu yake, ambayo ilitungwa kama jibu kwa Martin Luther na kutolewa mwaka 1555 kwa jina la Summa doctrinae christianae, ilirudia kuchapwa mara 200 hivi wakati wa maisha yake.

Mwaka 1580 alianzisha huko Freiburg (Uswisi) chuo Sankt Michael, ambapo alifariki na kuzikwa.

Maandishi

Toleo refu (lenye madondoo ya kuthibitishia):

Volume. 1: Faith, Hope, Charity, the Precepts of the Church
Vol. 2: The Sacraments
Vol. 3: Christian Justification, good works, Cardinal Virtues, Gifts and Fruits of the Holy Ghost, Eight Beatitudes, Evangelical Counsels, etc.

Viungo vya nje