Adamu : Tofauti kati ya masahihisho
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza ko:아담 |
d r2.7.2) (Roboti: Imeongeza arz:آدم |
||
Mstari 27: | Mstari 27: | ||
[[ar:آدم]] |
[[ar:آدم]] |
||
[[arc:ܐܕܡ]] |
[[arc:ܐܕܡ]] |
||
[[arz:آدم]] |
|||
[[az:Adəm]] |
[[az:Adəm]] |
||
[[be:Адам]] |
[[be:Адам]] |
Pitio la 21:18, 17 Septemba 2012
Adamu (kwa Kiebrania: אָדָם maana yake mtu, mtu wa udongo, chaudongo, au wa udongo mwekundu) ni jina analopewa mtu wa kwanza katika Biblia. Anatajwa na Kurani pia.
Kadiri ya kitabu cha Mwanzo, alizaliana na mke wake Eva watu wote waliopo duniani, ambao kwa sababu hiyo wanaitwa binadamu; kwa namna ya pekee waliweza kuzaa wenyewe Kaini, Abeli na Set.
Kanisa Katoliki linamheshimu kama mtakatifu kila tarehe 24 Desemba.
Katika Biblia
Uumbaji wa watu wa kwanza unasimuliwa na kitabu cha Mwanzo mara mbili: katika 1,26-28 na katika 2,7-22.
Masimulizi hayo yanayotofautiana katika vipengele mbalimbali hayadai yachukuliwe kama habari za historia zinazoandikwa siku hizi. Yanatokana na tafakuri ya kina juu ya hali ya binadamu kwa lengo la kuelewa asili yake.
Katika Kurani
Humo Adamu anatajwa kwa namna inayofanana na ile ya Biblia. Anahesabiwa kuwa mtume wa kwanza. Kigezo:Link FA