Tofauti kati ya marekesbisho "Teresa wa Mtoto Yesu"

Jump to navigation Jump to search
1,302 bytes added ,  miaka 8 iliyopita
no edit summary
d (r2.7.3) (Roboti: Imebadilisha: simple:Thérèse of Lisieux)
 
Mwaka [[1925]] [[Papa Pius XI]] alimtangaza mtakatifu, na mwaka [[1997]] [[Papa Yohane Paulo II]] alimtangaza mwalimu wa Kanisa kutokana na mchango wake mkubwa katika [[teolojia ya Kiroho]] alioutoa kupitia maandishi yake, yaliyoenea upesi ajabu duniani kote.
 
==Sala zake==
Ee Mungu wangu! Utatu mtakatifu!
Natamani tu kukupenda na kukufanya upendwe...
 
Ili maisha yangu yaweze kuwa tendo moja tu la upendo kamili:
Ninajitoa mhanga
kama kitambiko cha kuteketezwa kabisa na upendo wako rahimu.
 
Nakusihi uniteketeze bila ya kukoma,
ukiyaruhusu yale mawimbi ya upendo wako usiopimika,
yanayojazana ndani yako, yafurike rohoni mwangu:
hivyo nami niweze kuwa shahidi wa upendo wako, Mungu wangu!
 
Unijalie kifodini hicho baada ya kunitayarisha kutokea mbele yako, hatimaye unisababishe kufa:
na roho yangu iruke moja kwa moja, bila ya kuchelewa popote pale,
ifikie kukumbatiana milele na upendo wako rahimu.
 
Ee mpenzi wangu, mimi napenda, katika kila pigo la moyo wangu,
kurudia upya, mara nyingi zisizohesabika,
hili tendo langu la kujitoa kwako.
 
Mpaka hapo vivuli vitakapotoweka,
nami nikaweza kukuambia milele, uso kwa uso, jinsi ninavyokupenda.
 
 
Ee Yesu, upendo wangu, hatimaye nimegundua wito wangu.
 
Wito wangu ni kupenda!
 
Ndiyo, nimeona nafasi yangu ndani ya Kanisa,
na nafasi hiyo umenipatia wewe, Mungu wangu.
 
Katika moyo wa Kanisa, mama yangu, nitakuwa upendo:
hivyo nitakuwa yote na hamu yangu itatimia.
 
 
Ee Bwana Yesu, mimi si tai, ila nina macho na moyo wake.
 
Ingawa ni mdogo, nathubutu kulikazia macho jua la upendo,
na kutamani kurukia kwake.
 
== Maandishi yake katika tafsiri ya [[Kiswahili]] na ya [[Kihaya]] ==

Urambazaji