Waraka wa kwanza kwa Wakorintho : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 89: Mstari 89:
[[sv:Första Korinthierbrevet]]
[[sv:Första Korinthierbrevet]]
[[ta:கொரிந்தியருக்கு எழுதிய முதலாவது நிருபம்]]
[[ta:கொரிந்தியருக்கு எழுதிய முதலாவது நிருபம்]]
[[th:พระธรรม 1 โครินธ์]]
[[th:จดหมายของนักบุญเปาโลถึงชาวโครินธ์ ฉบับที่ 1]]
[[tl:Unang Sulat sa mga taga-Corinto]]
[[tl:Unang Sulat sa mga taga-Corinto]]
[[tr:Pavlus’un Korintlilere birinci mektubu]]
[[tr:Pavlus’un Korintlilere birinci mektubu]]

Pitio la 00:54, 31 Agosti 2012

Agano Jipya


Barua ya kwanza kwa Wakorintho ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira

Kutoka Korintho habari za kusikitisha zilimfikia Mtume Paulo akiwa [Efeso]] (pengine mwaka 57): katika Kanisa hilo ambalo alilianzisha na kulipenda sana kulikuwa na shaka kuhusu imani, mafarakano, upinzani wa Wakristo wa Kiyahudi dhidi yake, na makwazo.

Kilichohatarisha zaidi jumuia hiyo ni karama mbalimbali ambazo hao Wakristo wachanga walizijali mno na hatimaye wakajivunia kuwa nazo.

Vilevile walivutiwa kumfuata mtu kama Apolo, mwenye ujuzi na ufasaha mkubwa, mambo yaliyopendwa sana na Wagiriki.

Ilimbidi Paulo arekebishe hali hiyo ili kuokoa hasa umoja wa Kanisa na heshima kwa viongozi wake halali.

Basi mwaka mzima akawa na mahangaiko kwa wafuasi wake wa Korintho akawaandikia walau barua nne au tano, ingawa sisi tunazo mbili tu; pengine sehemu za baadhi yake zimeshonwa ndani ya 2Kor.

Mpangilio

Mpangilio wa barua ya kwanza una salamu na shukrani, halafu hukumu juu ya matatizo ya Wakristo hasa kufarakana (1Kor 1:10-16; 2:1-4:16), kuzini na kushtakiana mahakamani (1Kor 5-6).

Baada ya hapo akaanza kujibu maswali yao mbalimbali: kuhusu ndoa na useja (1Kor 7), nyama zilizotolewa sadaka kwa miungu (1Kor 8:1-11:1), mwenendo katika ibada na karama (1Kor 11:20-33; 12:4-13:13; 14:18-40), na hatimaye ufufuko wa wafu (1Kor 15:1-28,33-49).

Mwishoni kuna maagizo, taarifa na salamu mbalimbali (1Kor 16:1-4).

Ndiyo sababu barua ni ndefu na inagusa mambo mengi ambayo Paulo aliyatazama kwa hekima ya juu inayotokana na msalaba wa Kristo.

Madondoo muhimu

Kati ya mambo mengi muhimu, barua hiyo inatunza simulizi la kwanza la karamu ya mwisho ya Bwana Yesu (11:23-25) na kanuni ya imani ya kwanza inayoorodhesha pia matokeo ya Yesu Kristo Mfufuka (15:3-8).

Kiungo cha nje

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili