Kemal Atatürk : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza ht:Mustafa Kemal Atatürk
Mstari 106: Mstari 106:
[[lt:Mustafa Kemalis Atatiurkas]]
[[lt:Mustafa Kemalis Atatiurkas]]
[[lv:Mustafa Kemals Ataturks]]
[[lv:Mustafa Kemals Ataturks]]
[[mhr:Ататюрк, Мустафа Кемаль]]
[[mhr:Ататӱрк, Мустафа Кемаль]]
[[mk:Мустафа Кемал Ататурк]]
[[mk:Мустафа Кемал Ататурк]]
[[ml:മുസ്തഫ കമാൽ അത്താതുർക്ക്]]
[[ml:മുസ്തഫ കമാൽ അത്താതുർക്ക്]]
Mstari 113: Mstari 113:
[[mrj:Ататӱрк, Мустафа Кемаль]]
[[mrj:Ататӱрк, Мустафа Кемаль]]
[[ms:Mustafa Kemal Atatürk]]
[[ms:Mustafa Kemal Atatürk]]
[[mt:Mustafa Kemal Atatürk]]
[[my:ကီးမား အာတာတပ်]]
[[my:ကီးမား အာတာတပ်]]
[[mzn:آتاتورک]]
[[mzn:آتاتورک]]

Pitio la 20:17, 21 Agosti 2012

Faili:Portrait of M. Kemal Ataturk.jpg
Mustafa Kemal Atatürk
Faili:General Mustafa Kemal.jpg
Atatürk kama kiongozi wa kijeshi 1921

Mustafa Kemal Atatürk (* 1881 Saloniki (leo Thessaloniki); † 10 Novemba 1938 Istanbul) alikuwa ni mwanzilishi na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Uturuki.

Jina lake lilikuwa Mustafa Kemal. Cheo cha "Atatürk" alipewa baadaye kinachomaanaisha "Baba wa Waturuki". Alizaliwa mjini Thessaloniki katika Ugiriki ya Kaskazini iliyokuwa sehemu ya Milki ya Osmani hadi 1913.

Alikuwa mwanajeshi. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia aliongoza utetezi wa Waturuki dhidi ya mashambulio ya Uingereza na Ufaransa kwenye mlango wa bahari ya Dardanili na kujipatia sifa nyingi. Baada ya kuporomoka kwa Milki ya Osmani wakati wa mwisho wa vita Atatürk aliongoza upinzani wa kitaifa dhidi ya majaribio ya Ugiriki kujipatia sehemu kubwa za Anatolia ya magharibi.

Atatürk alitangaza Uturuki kuwa jamhuri, kumpindua Sultani na kuhamisha mji mkuu kwenda Ankara kutoka Istanbul. Baadaye alifuta cheo cha Khalifa kilichokuwa kiliunganishwa na cheo cha Sultani tangu 1517.

Atatürk aliamini ya kwamba sababu za kiushindwa kwa Uturuki vitani zilikuwa desturi na imani za kale. Hivyo aliamua kubadilisha tabia za taifa lake.

Alifuta sharia ya Kiislamu na mahakama ya kadhi. Badala yake alianzisha sheria mpya zilizofuata mifano ya Uswisi na Italia. Sheria ilitangaza usawa wa jinsia na kuwapa wanawake haki ya kupiga kura. Nguo za Kiislamu na hijab zilipigwa marufuku.

Shule zilianzishwa kwa watoto wote. Mwaka 1928 alfabeti ya Kiarabu ilifutwa iliyotumiwa kuandika Kituruki na vitabu vipya vilionyesha maandishi ya lugha ya taifa kwa alfabeti ya Kilatini. Idadi ya watu waliojifunza kusoma ilipanda kutoka 20% kufikia 90%.

10 Novemba 1938 alikufa mjini Istanbul.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kemal Atatürk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA