Barabara ya hariri : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imebadilisha: hr:Svileni put
d r2.7.2) (Roboti: Imeongeza diq:Raê Birsimi
Mstari 39: Mstari 39:
[[da:Silkevejen]]
[[da:Silkevejen]]
[[de:Seidenstraße]]
[[de:Seidenstraße]]
[[diq:Raê Birsimi]]
[[en:Silk Road]]
[[en:Silk Road]]
[[eo:Silka Vojo]]
[[eo:Silka Vojo]]

Pitio la 12:24, 21 Agosti 2012

Njia za biashara ya kimataifa kati ya China na Ulaya wakati wa karne ya kwanza BK (majina ya nchi kwa Kilatini: Sinae-China, Media Persis - Uajemi)

Barabara ya hariri ilikuwa njia muhimu ya biashara kati ya China kwa upande moja na Mashariki ya Kati halafu Ulaya kwa upande mwingine. Biashara hii iliendelea tangu karne kabla ya Kristo. Jina la "barabara ya hariri" limetokana na hariri ambayo ilitengenezwa katika China pekee kwa muda mrefu ikawa kati ya bidhaa zilizotafutwa sana duniani kwa bei ya juu.

Nyavu ya njia mbalimbali zilizopita Asia ya Kati

Barabara ya hariri haikuwa njia moja tu bali jumla ya njia za misafara kati ya China na nchi za Magharibi zilizopita katika Asia ya Kati.

Palikuwa na njia za kando hasa baharini kati ya China na Uhindi halafu kutoka Uhindi hadi Irak au Misri. Njia za bahari zilikuwa muhimu kama njia ya nchi kavu ilikatika wakati wa vita au ukosefu wa usalama. Kuna vipindi vichache ambako eneo lote la barabara ya hariri lilikuwa na usalama hasa wakati wa utawala wa Wamongolia. Menginevyo safari zilikuwa za hatari zikachukua muda mrefu. Bidhaa zilipita mkononi mwa wanafanyabiashara mbalimbali zikaongezeka bei njiani.

Njia ya bidhaa, watu na mawazo

Si bidhaa tu zilizosafiri kwneye barabara ya hariri. Wasafiri, mawazo, mafundisho, dini na magonjwa vilipita pia kwa njia hiyo. Teknolojia kama kutengenezwa kwa karatasi au kuchapishwa kwa vitabu zilipita njia hii kutoka China hadi Asia ya Magharibi na kutoka hapa hadi Ulaya.

Uenezaji wa Ubuddha kwenda Mongolia na China katika karne ya 4 BK, wa Ukristo kufika China katika karne ya 3 BK na wa Uislamu kuelekea mashariki katika karne ya 8 ulifuata barabara hii.

Njia ya magonjwa

Magonjwa yalipita njia hiyohiyo. kwa mfano tauni ilianza katika miaka ya 1330 katika China kwenye jimbo la Yunnan. Ugonjwa huu unategemea viroboto kama kituo cha virusi yake. Farasi za jeshi la Mongolia na biashara ya ngozi ilipeleka viroboto vile hadi Bahari Nyeusi. Mwaka 1348 wafanyabiashara Waitalia kutoka Bahari Nyeusi waliingiza ugonjwa Ulaya penyewe ulipoua robo ya wakazi wote.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA