Chui milia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2+) (Roboti: Imebadilisha: cs:Tygr
d r2.7.2+) (Roboti: Imeongeza nah:Huēhuehocēlōtl
Mstari 135: Mstari 135:
[[ms:Harimau]]
[[ms:Harimau]]
[[my:ကျား]]
[[my:ကျား]]
[[nah:Huēhuehocēlōtl]]
[[ne:बाघ]]
[[ne:बाघ]]
[[nl:Tijger]]
[[nl:Tijger]]

Pitio la 13:33, 21 Julai 2012

Chui milia
Chui milia wa Bengali
Chui milia wa Bengali
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Felidae (Wanyama walio na mnasaba na paka)
Nusufamilia: Pantherinae (Wanyama wanaofanana na chui)
Jenasi: Panthera
Spishi: Panthera tigris
(Linnaeus, 1758)
Nususpishi: Panthera t. altaica

Panthera t. amoyensis
Panthera t. altaica
Panthera t. corbetti
Panthera t. jacksoni
Panthera t. sumatrae
Panthera t. tigris

Chui milia (pia: babara kutoka Kiarabu: babar; Kisayansi: Panthera tigris) ni mnyama mkubwa mla nyama wa familia ya felidae katika ngeli ya mamalia kwa hiyo chui milia hufanana na paka mkubwa.

Chui milia wanaishi katika Asia katika pembetatu kati ya Uhindi, Siberia ya kusini na Indonesia. Mazingira wanayoendelea ni misitu. Siku hizi idadi ya chui milia imepungua sana kutokana na upotevu wa maeneo na kuvindwa.

Chakula chao ni nyama inayopatikana kwa kuvinda wanyama. Kama wanyama wengi wanaofanana paka chui milia hupendelea kuvinda pekee yake. Kila mmoja ana eneo lake analoweka alama za kojo na kuitetea dhidi ya chui milia wengine.

Ukubwa wa wanyama hao hutofautiana kutokana na maeneo yao na nususpishi zao. Wale wa Sumatra ni wadogo wakiwa na urefu wa mwili (pamoja na kichwa bila mkia) sentimita 140 pekee na uzito wa 120 kg. Mkubwa ni chui milia wa Siberia mwenye urefu unaopita mita 2 na uzito wa kilogramu 150 (jike) hadi 250 (dume). Aina ya Siberia ni kubwa kushinda simba Mwafrika.

Jike anazaa wadogo 2-3 na kuwatunza kwa miaka 2 - 3. Baadaye wanapaswa kujitafutia eneo lao. Kwa umri wa miaka 3-4 anaweza kuzaa na kufikia umri wa miaka 20 - 25.

Ramani inaonyesha maeneo yaliyokaliwa na chui milia mnamo 1900 (chungwa) na eneo linalobaki leo (nyekundu)

Viungo vya Nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA