Kitabu cha Yeremia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
Kitabu cha [[Yeremia]] ni kimojawapo kati ya [[vitabu vya kinabii]] vilivyo virefu zaidi katika [[Tanakh]] ([[Biblia ya Kiebania]]), na kwa hiyo pia katika [[Agano la Kale]] ambalo ni sehemu ya kwanza ya [[Biblia ya Kikristo]].
Kitabu cha [[Yeremia]] ni kimojawapo kati ya [[vitabu vya kinabii]] vilivyo virefu zaidi katika [[Tanakh]] ([[Biblia ya Kiebrania]]), na kwa hiyo pia katika [[Agano la Kale]] ambalo ni sehemu ya kwanza ya [[Biblia ya Kikristo]].


Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya [[ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya [[ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].

==Mhusika mkuu==

Yeremia, mtu mpole sana, aliitwa na [[Mungu]] akiwa bado kijana, akapewa kazi ngumu ya kutabiri maangamizi ya [[Yerusalemu]] viongozi wasipoacha siasa yao ili kumtegemea Mungu tu.

Habari zake zinapatikana hasa katika kitabu hiki, ingawa humo hazikupangwa kitarehe.


==Wito na muda wa unabii wake==
==Wito na muda wa unabii wake==
Akiwa bado [[kijana]], [[kuhani]] huyo mpole aliitwa na Mungu awe [[nabii]] katika kipindi cha [[misukosuko]] huko [[Mashariki ya Kati]], ambapo [[Wakaldayo]] wa [[Babeli]] waliwashinda [[Waashuru]] na kueneza [[utawala]] wao hadi kuteketeza [[Yerusalemu]] na [[hekalu]] lake. Katikati ya matukio hayo yote, Yeremia alipewa kazi ngumu ya kuonya na kutisha watu wa [[Yuda]] kwa kutabiri maangamizi hayo ili wamrudie kweli Mungu wasipatwe na [[adhabu]] kali kama wenzao wa [[kaskazini]]. Lakini wao hawakuwa tayari kufanya hivyo, wakijiamini hawatakoma kwa kuwa, tofauti na hao, wanatawaliwa na [[ukoo]] halali wa [[Daudi]] ulioahidiwa kudumu [[milele]], tena wanatunza hekalu pekee la Mungu na [[sanduku la agano]] analokalia. Walidanganywa na ma[[nabii wa uongo]] waamini hivyo, kumbe walitakiwa kujirekebisha na kufuata kweli masharti ya [[agano]] lenyewe.


Hivyo Yeremia alilazimika kupambana na wote: wafalme, makuhani na manabii wenzake, [[ndugu]] wa ukoo wake na wananchi kwa jumla. Ilimbidi ashindane nao kinyume cha [[silika]] yake ya [[upole]] iliyomfanya apende kuelewana na watu. [[Upweke]] wake ulizidiwa na [[useja]] alioitiwa na Mungu ili aonye hata kwa njia hiyo kwamba mambo yajayo ni magumu na ya kutisha hata iwe afadhali kutozaa watoto.
Toka mwanzo Yeremia alitaka kukataa wito wa unabii, na hata baadaye akafikia hatua ya kukata tamaa alipodhulumiwa. Lakini Mungu alimuita kwa mpango wa milele, Yeremia asiweze kukataa (15:10-21; 20:7-18).


Katika miaka yote 40 na zaidi ya [[unabii]] wake kipindi kizuri ni miaka ile 13 tu ([[622 K.K.|622]] - [[609 K.K.]]) ambapo [[Yosia]] alifanya urekebisho wa kidini kuanzia Yerusalemu hadi kwa mabaki ya [[Waisraeli]] wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mungu [[sadaka]] nje ya [[hekalu la Yerusalemu]]. Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha Nahumu (612 hivi K.K.).
Katika muda wa utume wake (626-585 hivi [[K.K.]]) kipindi kizuri ni kile tu ambacho [[mfalme Yosia]] alifanya [[urekebisho]] (622-609 K.K.).


Lakini Yosia alipokufa [[vita]]ni kabla ya wakati mambo yakaharibika haraka sana, kwa sababu urekebisho ulitokana zaidi na [[juhudi]] zake binafsi. Basi, ikambidi Yeremia awakaripie wafalme waliomrithi mmoja baada ya mwingine waache [[siasa]] yao ili kumtegemea Mungu tu. Aliwakaripia pia wananchi wasifanye dini kisingizio cha kuendelea na maovu badala ya kutubu (7:1-15; 19:1-13).
Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha [[Nahumu]] (612 hivi K.K.).


Aliwakaripia vilevile manabii wa uongo waliotumainisha watu bure (20:1-6). Ndipo alipoanza kupigwa, kufungwa na kuhukumiwa, akawa mfano wa Yesu, yeye ambaye peke yake katika Agano la Kale aliishi bila ya ndoa kwa agizo la Mungu; lakini hakuuawa (26:1-19). Kwa hofu akajificha, ila hakuacha kutabiri maangamizi kwa maandishi kwa njia ya karani wake [[Baruku]] (36).
Lakini kisha kufa Yosia mambo yakaharibika haraka sana, ikambidi Yeremia awakaripie wafalme na wananchi wasifanye [[dini]] kisingizio cha kuendelea na maovu badala ya kutubu (7:1-15; 19:1-13).


Basi, mfalme [[Nabukadreza]] wa Babeli akazidi kuwa na nguvu: mwaka 602 K.K. akamtiisha mfalme [[Yehoyakimu]] wa Yuda, na mwaka 598 K.K. akazingira Yerusalemu akawahamishia Babeli mfalme [[Yekonia]] na viongozi wengine 8000. Hapo Yeremia akawaandikia wasikate tamaa ila wasitarajie kurudi upesi kwa kuwa watabaki uhamishoni miaka 70 (29:4-23). Lakini katika mpango wa Mungu hao ndio wa kutegemewa, sio walioachwa Yerusalemu (24). Nabukadreza alipohusuru mji huo mara ya pili, mfalme na viongozi wengine walikataa shauri la Yeremia la kusalimu amri, wakamfunga pabaya sana mpaka siku ya Yerusalemu kutekwa na kuteketezwa (37-38).
Aliwakaripia vilevile [[manabii wa uongo]] waliotumainisha watu bure (20:1-6).


Yeye alishuhudia hayo yote kwa [[huzuni]] kubwa na kati ya [[dhuluma]] nyingi hata akamlalamikia sana Mungu kwa kumuumba awe mtu wa [[mateso]]. Toka mwanzo alitaka kukataa [[wito]] wa [[unabii]], na baadaye akafikia hatua ya kukata tamaa. Lakini Mungu alimuita kwa mpango wa milele, Yeremia asiweze kukataa (15:10-21; 20:7-18). [[Unyofu]] wa maneno yake katika [[sala]] ([[Maungamo ya Yeremia]]) unatuwezesha kumfahamu mpaka ndani kuliko mtu yeyote wa [[Agano la Kale]]. Lakini mateso hayo hayakuwa bure, bali kwa njia yake alizidi kuelewa [[dini]] kama [[suala]] la [[moyo]]. Ni hivyo kwamba aliona agano lililoandikwa katika [[mbao]] za mawe limeshindikana, na [[tohara]] inayohitajika ni ile ya ma[[sikio]] na moyo. Basi, kwa kutambua [[uaminifu]] wa Mungu, alitabiri agano litakaloandikwa katika mioyo ya watu, ambao hapo wataweza kulishika na kumfahamu kweli [[Bwana]].
Ndipo alipoanza kupigwa, kufungwa na kuhukumiwa, akawa mfano wa [[Yesu]], yeye ambaye peke yake katika [[Agano la Kale]] aliishi bila ya [[ndoa]] kwa agizo la Mungu; lakini hakuuawa (26:1-19).


Kwa kawaida Yeremia alitabiri kinyume cha matazamio madanganyifu ya watu, lakini walipokata tamaa akawatuliza na kutabiri heri. Basi, [[kilele]] cha mafundisho yake na ya [[Agano la Kale]] lote ni kwamba Mungu atafunga na Israeli yote Agano Jipya (31:31-34).
Kwa hofu akajificha, ila hakuacha kutabiri maangamizi kwa maandishi kwa njia ya karani wake [[Baruku]] (36).


==Mwisho wa unabii wake==
Basi, mfalme [[Nabukadreza]] wa [[Babeli]] akazidi kuwa na nguvu: mwaka 602 K.K. akamtiisha mfalme [[Yehoyakimu]] wa [[Yuda]], na mwaka 598 K.K. akazingira Yerusalemu na kuwahamishia Babeli mfalme [[Yekonia]] na viongozi wengi.


Baada ya Yerusalemu kuteketezwa (587 K.K.) Yeremia alichagua kubaki nchini pamoja na mafukara badala ya kuhamia Babeli kwa [[heshima]] ya pekee (39:8-40:6), ila ukatokea uasi akalazimishwa na Waisraeli wenzake kuwafuata Misri: huko akawaonya wasifuate Upagani lakini wakakataa tena kumsikiliza (42-44).
Hapo Yeremia akawaandikia wasikate tamaa ila wasitarajie kurudi upesi kwa kuwa watabaki uhamishoni miaka 70 (29:4-23).

Lakini katika mpango wa Mungu hao ndio wa kutegemewa, sio walioachwa Yerusalemu (24).

Nabukadreza alipohusuru mji huo mara ya pili, mfalme na viongozi wengine walikataa shauri la Yeremia la kusalimu amri, wakamfunga pabaya sana mpaka siku ya Yerusalemu kutekwa (37-38).

Kwa kawaida Yeremia alitabiri kinyume cha matazamio madanganyifu ya watu, lakini walipokata tamaa akawatuliza na kutabiri heri.

Kilele cha mafundisho yake ni kwamba Mungu atafunga na [[Israeli]] yote [[Agano Jipya]] ambalo litaandikwa mioyoni (31:31-34).

==Mwisho wa unabii wake==


Hatimaye, kadiri ya [[mapokeo]] ya [[Wayahudi]], [[kifodini|akauawa]] nao huko. Ingawa alionekana kufeli kabisa, [[sadaka]] yake ilizidi kuzaa, kwa kuwa wengi walizingatia mafundisho yake bora.
Baada ya Yerusalemu kuteketezwa (587 K.K.) Yeremia alichagua kubaki nchini pamoja na mafukara badala ya kuhamia Babeli (39:8-40:6), ila ukatokea uasi akalazimishwa na Waisraeli wenzake kuwafuata [[Misri]]: huko akawaonya wasifuate Upagani lakini wakakataa tena kumsikiliza (42-44).


==Nyongeza==
==Nyongeza==

Pitio la 08:05, 1 Julai 2012

Kitabu cha Yeremia ni kimojawapo kati ya vitabu vya kinabii vilivyo virefu zaidi katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania), na kwa hiyo pia katika Agano la Kale ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Wito na muda wa unabii wake

Akiwa bado kijana, kuhani huyo mpole aliitwa na Mungu awe nabii katika kipindi cha misukosuko huko Mashariki ya Kati, ambapo Wakaldayo wa Babeli waliwashinda Waashuru na kueneza utawala wao hadi kuteketeza Yerusalemu na hekalu lake. Katikati ya matukio hayo yote, Yeremia alipewa kazi ngumu ya kuonya na kutisha watu wa Yuda kwa kutabiri maangamizi hayo ili wamrudie kweli Mungu wasipatwe na adhabu kali kama wenzao wa kaskazini. Lakini wao hawakuwa tayari kufanya hivyo, wakijiamini hawatakoma kwa kuwa, tofauti na hao, wanatawaliwa na ukoo halali wa Daudi ulioahidiwa kudumu milele, tena wanatunza hekalu pekee la Mungu na sanduku la agano analokalia. Walidanganywa na manabii wa uongo waamini hivyo, kumbe walitakiwa kujirekebisha na kufuata kweli masharti ya agano lenyewe.

Hivyo Yeremia alilazimika kupambana na wote: wafalme, makuhani na manabii wenzake, ndugu wa ukoo wake na wananchi kwa jumla. Ilimbidi ashindane nao kinyume cha silika yake ya upole iliyomfanya apende kuelewana na watu. Upweke wake ulizidiwa na useja alioitiwa na Mungu ili aonye hata kwa njia hiyo kwamba mambo yajayo ni magumu na ya kutisha hata iwe afadhali kutozaa watoto.

Katika miaka yote 40 na zaidi ya unabii wake kipindi kizuri ni miaka ile 13 tu (622 - 609 K.K.) ambapo Yosia alifanya urekebisho wa kidini kuanzia Yerusalemu hadi kwa mabaki ya Waisraeli wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mungu sadaka nje ya hekalu la Yerusalemu. Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha Nahumu (612 hivi K.K.).

Lakini Yosia alipokufa vitani kabla ya wakati mambo yakaharibika haraka sana, kwa sababu urekebisho ulitokana zaidi na juhudi zake binafsi. Basi, ikambidi Yeremia awakaripie wafalme waliomrithi mmoja baada ya mwingine waache siasa yao ili kumtegemea Mungu tu. Aliwakaripia pia wananchi wasifanye dini kisingizio cha kuendelea na maovu badala ya kutubu (7:1-15; 19:1-13).

Aliwakaripia vilevile manabii wa uongo waliotumainisha watu bure (20:1-6). Ndipo alipoanza kupigwa, kufungwa na kuhukumiwa, akawa mfano wa Yesu, yeye ambaye peke yake katika Agano la Kale aliishi bila ya ndoa kwa agizo la Mungu; lakini hakuuawa (26:1-19). Kwa hofu akajificha, ila hakuacha kutabiri maangamizi kwa maandishi kwa njia ya karani wake Baruku (36).

Basi, mfalme Nabukadreza wa Babeli akazidi kuwa na nguvu: mwaka 602 K.K. akamtiisha mfalme Yehoyakimu wa Yuda, na mwaka 598 K.K. akazingira Yerusalemu akawahamishia Babeli mfalme Yekonia na viongozi wengine 8000. Hapo Yeremia akawaandikia wasikate tamaa ila wasitarajie kurudi upesi kwa kuwa watabaki uhamishoni miaka 70 (29:4-23). Lakini katika mpango wa Mungu hao ndio wa kutegemewa, sio walioachwa Yerusalemu (24). Nabukadreza alipohusuru mji huo mara ya pili, mfalme na viongozi wengine walikataa shauri la Yeremia la kusalimu amri, wakamfunga pabaya sana mpaka siku ya Yerusalemu kutekwa na kuteketezwa (37-38).

Yeye alishuhudia hayo yote kwa huzuni kubwa na kati ya dhuluma nyingi hata akamlalamikia sana Mungu kwa kumuumba awe mtu wa mateso. Toka mwanzo alitaka kukataa wito wa unabii, na baadaye akafikia hatua ya kukata tamaa. Lakini Mungu alimuita kwa mpango wa milele, Yeremia asiweze kukataa (15:10-21; 20:7-18). Unyofu wa maneno yake katika sala (Maungamo ya Yeremia) unatuwezesha kumfahamu mpaka ndani kuliko mtu yeyote wa Agano la Kale. Lakini mateso hayo hayakuwa bure, bali kwa njia yake alizidi kuelewa dini kama suala la moyo. Ni hivyo kwamba aliona agano lililoandikwa katika mbao za mawe limeshindikana, na tohara inayohitajika ni ile ya masikio na moyo. Basi, kwa kutambua uaminifu wa Mungu, alitabiri agano litakaloandikwa katika mioyo ya watu, ambao hapo wataweza kulishika na kumfahamu kweli Bwana.

Kwa kawaida Yeremia alitabiri kinyume cha matazamio madanganyifu ya watu, lakini walipokata tamaa akawatuliza na kutabiri heri. Basi, kilele cha mafundisho yake na ya Agano la Kale lote ni kwamba Mungu atafunga na Israeli yote Agano Jipya (31:31-34).

Mwisho wa unabii wake

Baada ya Yerusalemu kuteketezwa (587 K.K.) Yeremia alichagua kubaki nchini pamoja na mafukara badala ya kuhamia Babeli kwa heshima ya pekee (39:8-40:6), ila ukatokea uasi akalazimishwa na Waisraeli wenzake kuwafuata Misri: huko akawaonya wasifuate Upagani lakini wakakataa tena kumsikiliza (42-44).

Hatimaye, kadiri ya mapokeo ya Wayahudi, akauawa nao huko. Ingawa alionekana kufeli kabisa, sadaka yake ilizidi kuzaa, kwa kuwa wengi walizingatia mafundisho yake bora.

Nyongeza

Kama nyongeza ya kitabu cha Yeremia tuna Maombolezo matano juu ya Yerusalemu ulioteketezwa, ambamo inaonekana toba halisi baada ya tukio hilo. Hatujui yametungwa na nani.

Viungo vya nje

Kitabu cha Yeremia katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.