Papa Alexander VI : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza simple:Pope Alexander VI
Mstari 70: Mstari 70:
[[ru:Александр VI]]
[[ru:Александр VI]]
[[sh:Aleksandar VI.]]
[[sh:Aleksandar VI.]]
[[simple:Pope Alexander VI]]
[[sk:Alexander VI.]]
[[sk:Alexander VI.]]
[[sl:Papež Aleksander VI.]]
[[sl:Papež Aleksander VI.]]

Pitio la 14:25, 19 Juni 2012

Papa Alexander VI

Papa Alexander VI (1 Januari, 143118 Agosti, 1503) alikuwa papa kuanzia 11 Agosti, 1492 hadi kifo chake. Alimfuata Papa Innocent VIII akafuatwa na Papa Pius III.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Roderic Borgia. Alikuwa papa wa pili kutoka familia ya Borgia. Callixtus III aliyekuwa Borgia wa kwanza alimsaidia mpwa wake Roderic kupanda ngazi ndani ya kanisa. Kijana asiyekuwa na mafunzo wowote wa kiroho asiyepokea ubarikio wa upadre bado alipewa cheo na mapato ya askofu mara kadhaa katika dayosisi mbalimbali. 1456 alipewa cheo cha kardinali na 1458 akapadrishwa.

Alizaa watoto na mke wake wa kando Vannozza dei Cattani akaendelea kuwaangalia na kuwatunza hata alipokuwa papa. Arusi ya binti yake Lucrecia Borgia ilisheherekewa rasmi katika jumba la kipapa la Vatikano.

Lakini kabla hajachaguliwa kuwa papa alimwacha Vannozza akaanza uhusiano na binti Giulia Farnese aliyezaa binti naye mwaka 1492 alipokuwa papa.

Mwanawe Caesare alipewa cheo cha askofu alipokuwa na umri wa miaka 16 na kardinali alipofikia miaka 18. Baadaye aliacha maisha ya kanisa akafanywa na babaye jemadari wa jeshi la papa.

Alexander VI amejulikana pia kwa azimio lake la kugawa dunia kati ya Hispania na Ureno katika mkataba wa Tordesillas mwaka 1494. Mkataba huu ulikuwa msingi wa koloni ya Kireno cha Brazil na utawala wa Hispania juu ya nchi nyengine za Amerika Kusini.

Wapinzani walimwona kama mfano mbaya wa uharibifu wa Upapa wakati wake.

Viungo vya nje

Papa Alexander VI katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki