Edward Sokoine : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza no:Edward Sokoine
Mstari 31: Mstari 31:
[[id:Edward Moringe Sokoine]]
[[id:Edward Moringe Sokoine]]
[[it:Edward Sokoine]]
[[it:Edward Sokoine]]
[[no:Edward Sokoine]]
[[yo:Edward Sokoine]]
[[yo:Edward Sokoine]]

Pitio la 11:52, 14 Juni 2012

Edward Moringe Sokoine

Edward Moringe Sokoine (1938 - 12 Aprili, 1984) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Tanzania.

Aliwahi kuwa Waziri Mkuu mara mbili, tangu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba 1980, tena tangu tarehe 24 Februari 1983 hadi kifo chake, alipofariki kufuatana na ajali ya gari.

Uongozi wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na uadilifu na kufuatilia utendaji kazi huku akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Sokoine alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye kikao cha bunge Dodoma kuelekea Dar es Salaam. Wengi wanashuku ajali hiyo kuwa ilipangwa.

Kifo chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida ambao walikuwa wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao.

Mwili wa Edward Moringe Sokoine ulizikwa nyumbani kwao Monduli, mkoani Arusha.

Chuo cha Kilimo na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo cha Sokoine" ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edward Sokoine kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.