Mizengo Kayanza Peter Pinda : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza no:Mizengo Pinda
Mstari 43: Mstari 43:
[[id:Mizengo Pinda]]
[[id:Mizengo Pinda]]
[[ja:ミゼンゴ・ピンダ]]
[[ja:ミゼンゴ・ピンダ]]
[[no:Mizengo Pinda]]
[[pl:Mizengo Pinda]]
[[pl:Mizengo Pinda]]
[[ro:Mizengo Pinda]]
[[ro:Mizengo Pinda]]

Pitio la 17:07, 13 Juni 2012

Faili:Kikwete Pinda.JPG
Rais Kikwete wa Tanzania (kushoto) na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) tarehe 9 Februari 2008.

Mizengo Kayanza Peter Pinda (*12 Agosti 1948) ni mwanasiasa nchini Tanzania aliyechaguliwa Februari 2008 kuwa Waziri Mkuu wa nchi.

Maisha

Pinda alizaliwa Mpanda vijijini katika mkoa wa Rukwa kama mtoto wa kwanza wa mkulima maskini.

Alifuata elimu hadi kutunukiwa shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam mwaka 1974.

Mwaka uleule akajiunga na utumishi wa serikali kama wakili wa serikali katika Wizara ya Katiba na Sheria.

Mwaka 1978 akahamia ofisi ya Usalama wa Raia kwenye Ikulu ya rais, kwanza chini ya Julius Nyerere, halafu chini ya Ali Hassan Mwinyi.

Kuanzia mwaka 1982 akaendelea kuwa Katibu Mnyeka Msaidizi wa Rais hadi 1992.

Tangu mwaka 1996 hadi 2000 akawa Katibu wa Baraza la Mawaziri.

Bungeni ameingia mwaka 2000 kama mbunge wa Mpanda Mashariki mkoani Rukwa akawa naibu waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa tawala za mikoa na serikali za mitaa.

Mwaka 2006 akapandishwa cheo kuwa waziri kamili.

Baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Pinda aliteuliwa na rais Jakaya Kikwete na kuthibitishwa na bunge kwa kura 279 za ndio katika jumla ya kura 283 zilizopigwa.

Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 aliendelea na wadhifa huo.

Viungo vya nje