Siku : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (Roboti: Imeongeza dsb:Źeń
d r2.7.1) (Roboti: Imeongeza hy:Օր
Mstari 76: Mstari 76:
[[ht:Jou (Tan)]]
[[ht:Jou (Tan)]]
[[hu:Nap (időegység)]]
[[hu:Nap (időegység)]]
[[hy:Օր]]
[[ia:Die]]
[[ia:Die]]
[[id:Hari]]
[[id:Hari]]

Pitio la 17:03, 5 Juni 2012

Muda wa siku husababishwa na mzunguko wa dunia yetu kwenye mhimili wake. Hapa tunatazama upande wa mchana unaoangazwa na jua. Upande mwingine ni upande wa giza au usiku.

Siku ni muda wa wakati wa saa 24 ambamo tunaona vipindi viwili; kile cha mwanga wa mchana na kile cha giza la usiku.

Mchana na usiku

Mabadiliko haya ya mchana na usiku husabibishwa na mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake. Upande wa dunia unaotazama jua unapata mwanga wa mchana lakini upande mwingine usiotazama jua unakuwa gizani.

Sisi pamoja na vitu vyote vilivyo juu ya uso wa dunia, yaani majengo, barabara, bahari, mito, milima, binadamu, misitu, majangwa na kila kitu unachoweza kuwaza kuwa kipo kwenye uso wa dunia, basi vyote huwa katika mwendo kadri dunia inavyojizungusha kwenye mhimili wake. Hivyo basi, wakati upande ule wa uso wa dunia tulipo unapogeukia au kutazamana na jua, basi kwetu inakuwa mchana, pale ambapo upande huo hatutazamani na dunia, basi tunapata usiku, yaani tunakuwa kwenye giza.

Muda wa siku

Mzunguko huo wa dunia kwenye mhimii wake unachukua muda wa nukta (sekondi) 86,400 au masaa 24.

Kwa sababu muda wa mzunguko haulingani kamili na kipimo cha sekondi kuna siku ndefu au fupi zinazopatikana kwa kuingiza au kupunguza nukta moja kufuatana na azimio ya wataalamu wa wakati. Hii haina umhimu wowote katika maisha ya kila siku lakini inapaswa kuangaliwa pale ambako saa kamili sana ya kiatomi hutumiwa.

Siku na mwaka

Dunia pamoja na kujizungusha kwenye mhimili wake pia inafanya mwendo mwingine, yaani ule wa kulizunguka jua. Ikikamilisha mwendo huu basi mwaka unakuwa umekamilika. Kipindi cha mwaka hakilingani kwa kila mwaka, kuna miaka mirefu na miaka mifupi. Hii ni kwa mujibu wa Kalenda ya Gregori ambapo mwaka wa kawaida (mfupi) huwa na siku 365 na kila mwaka wa nne (mwaka mrefu) kuwa na siku 366.