Ambrosi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: sl:Sveti Ambrož
d r2.6.4) (Roboti: Imebadilisha: sl:Sveti Ambrož Milanski
Mstari 164: Mstari 164:
[[sh:Ambrozije Milanski]]
[[sh:Ambrozije Milanski]]
[[sk:Ambrosius Milánsky]]
[[sk:Ambrosius Milánsky]]
[[sl:Sveti Ambrož]]
[[sl:Sveti Ambrož Milanski]]
[[sq:Shën Ambrozi]]
[[sq:Shën Ambrozi]]
[[sr:Амброзије Милански]]
[[sr:Амброзије Милански]]

Pitio la 12:53, 3 Mei 2012

Mt. Ambrosi alivyochorwa kwa nakshi za mawe katika kanisa lake huko Milano

Aureli Ambrosi (334/339 - 397), alikuwa askofu wa Milano kuanzia mwaka 374 hadi kifo chake.

Ndiye aliyemuongoa na kumbatiza Agostino wa Hippo

Anaheshimiwa kama mtakatifu, babu wa Kanisa na mwalimu wa Kanisa. Sikuku yake ni tarehe 7 Desemba kila mwaka.

Maisha

Mwanasiasa

Ambrosi alizaliwa katika familia ya Kikristo ya Dola la Roma kati ya miaka 334 na 340 akakulia Trier (Ujerumani).

Baba yake, aliyeitwa Ambrosius Aurelianus, alikuwa liwali wa Gallia (leo Ufaransa); mama yake alijulikana kwa akili na imani yake. Ndugu zake, Satyrus na Marselina wanaheshimiwa pia kama watakatifu.

Alipofiwa baba, Ambrosi alifuata nyayo zake katika siasa. Alisomea Roma, hasa fasihi, sheria na hotuba.

Liwali Anicius Probus kwanza alimpa nafasi katika halmashauri halafu akamfanya gavana wa Liguria na Emilia, akiwa na makao makuu huko Milano, mji wa pili wa Italia.

Ambrose aliendelea na ugavana hadi mwaka 374 alipochaguliwa askofu wa Milano.

Ni kwamba, baada ya kifo cha Auxentius wa Milano aliyefuata uzushi wa Arios, Ambrosi alikuwa amefika kanisani ili kutuliza ghasia kati ya Waarios na Wakatoliki. Lakini alipohutubia umati, akashangiliwa, "Ambrosi, askofu!". Alitaka kukataa, kwa kuwa hata hajabatizwa, lakini hatimaye alikubali.

Alipewa ubatizo, kipaimara na ekaristi, halafu baada ya wiki moja daraja takatifu ya uaskofu.

Askofu

Mt. Ambrose, alivyochorwa na Francisco de Zurbarán

Kama askofu, zaidi ya useja wake, alishika juhudi za kitawa, alisaidia mafukara kwa mali zake karibu zote, akajitahidi kupata elimu ya Biblia na teolojia akaitumia vema katika kuhubiri.

Ilimbidi atetee imani sahihi dhidi ya wafuasi wa Arios, mmojawao kaisari aliyedai awaachie makanisa mawili ya Milano, lakini Ambrosi alikataa katakata, akisema, "Ukinitaka mwenyewe, niko tayari kutii: unipeleke gerezani au kifoni, sitapinga; lakini sitasaliti kamwe Kanisa la Yesu Kristo. Sitaita watu kunisaidia; nitakufa kwenye altare lakini si kuikimbia. Sitahimiza watu kupiga kelele: lakini Mungu tu anaweza kuwatuliza.

Mt. Ambrosi na kaisari Theodosius walivyochorwa na Anthony van Dyck.
Kikanisa chini ya basilika lake.

Ikulu halikupendezwa na msimamo wa Ambrosi, lakini ilimuogopa na kumhitaji katika mapambano ya siasa.

Theodosius I, kaisari wa mashariki, alipoangamiza (390) watu 7,000 huko Thesalonike (Ugiriki), Ambrosi alitisha kumtenga na Kanisa asipofanya toba kama mfalme Daudi, akamruhusu kupokea tena ekaristi baada tu ya miezi kadhaa ya malipizi.

Msimamo wake ulibaki kielelezo kwa Kanisa la magharibi hata likaendelea mara nyingi kushindana na serikali.

Ambrosi alipaswa pia kupambana dhidi ya Wapagani waliotaka kufanya tena dini ya jadi kuwa dini rasmi ya Dola la Roma badala ya Ukristo. Alifaulu kumfanya Theodosius I kutoa hati zake maarufu za mwaka 391.

Kati ya mambo ya pekee aliyoacha ni urithi wa tenzi na liturujia ya pekee inayoendelea kutumika Milano na sehemu nyingine za Italia kaskazini na Uswisi ("liturujia ya Kiambrosi").

Tarehe 4 Aprili Ambrosi alifariki, akaheshimika mara kama mtakatifu.

Masalia yake, ambayo ni kati ya maiti za zamani zaidi zilizopo nje ya Misri, yanatunzwa katika kanisa lake mjini Milano.

Maandishi

Ufafanuzi wa Biblia

  • Hexameron
  • De Paradiso
  • De Cain et Abel
  • De Noe
  • De Abraham
  • De Isaac et Anima
  • De Bono Mortis
  • De Fuga Saeculi
  • De Jacob et Vita Beata
  • De Joseph
  • De Patriarchis
  • De Helia e Jejunio
  • De Nabuthae Historia
  • De Tobia
  • De Interpellatione Job et David
  • De Apologia Profhetae David
  • Ennarrationes in XII Psalmos Davidicos
  • Expositio Psalmi CXVIII
  • Esposizione Evangelii Lucae
  • Expositio Isaiae Prophetae

Kuhusu dogma

  • De Fide ad Gratianum
  • De Spiritu Sancto
  • De Incarnationis Dominicae Sacramento
  • Explanatio Symboli ad Initiandos (imetafsiriwa kwa Kiswahili)
  • Expositio Fidei
  • De Mysteriis (imetafsiriwa kwa Kiswahili)
  • De Sacramentis (imetafsiriwa kwa Kiswahili)
  • De Poenitentia
  • De Sacramento regenerationis vel de Philosophia

Kuhusu maadili na maisha ya kiroho

  • De Officiis Ministrorum
  • De Virginibus
  • De Viduis
  • De Virginitate
  • De Instituitione Virginis
  • Exhortatio Virginitatis

Mengineyo

  • De obitu Theodosii
  • Epistulae, hymni, etc.

Tafsiri ya Kiswahili

  • MT. AMBROSI WA MILANO, Juu ya Sakramenti za kikristo (Explanatio Simboli – De Sacramentis – De Mysteriis) – tafsiri ya G. M. Brandolini na Tommaso Serra – ed. Ndanda Mission Press – Ndanda 2004 – ISBN 9976-63-664-4

Vyanzo

Viungo vya nje