Binadamu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2+) (Roboti: Imeongeza mdf:Ломанць
Mstari 20: Mstari 20:
== Binadamu kadiri ya sayansi ==
== Binadamu kadiri ya sayansi ==


Ki[[sayansi]] jina hilo linaweza kutumika kwa maana ya '''Homo Sapiens''' ili kumtofautisha na viumbe wengine wa [[jenasi]] Homo ambao wa mwisho wao (Homo Neanderthalensis) walitoweka miaka 35,000 hivi iliyopita. Wanadamu wote walioko leo hii ni [[spishi]] ileile na tofauti zinazoonekana kati ya maumbile ya watu katika sehemu mbalimbali za dunia ni kidogo tu.
Ki[[sayansi]] jina hilo linaweza kutumika kwa maana ya '''Homo Sapiens''' ili kumtofautisha na viumbe wengine wa [[jenasi]] Homo ambao wote walitoweka walau miaka 12,000 hivi iliyopita.


Watu wote walioko leo hii ni [[spishi]] ileile na tofauti zinazoonekana kati ya maumbile yao katika sehemu mbalimbali za dunia ni kidogo tu.
Utafiti juu ya [[DNA]] umethibitisha kwamba binadamu wote wametokana na watu waliokuwepo [[Afrika]] Mashariki tangu miaka 200,000 hivi iliyopita.

Utafiti juu ya [[DNA]] umethibitisha kwamba binadamu wote wametokana na watu waliokuwepo [[Afrika]] Mashariki walau miaka 200,000 hivi iliyopita.


Kwa namna ya pekee, upimaji wa [[DNA ya mviringo]], ambayo kila mmoja anarithi kwa mama tu, unaonyesha kuwa binadamu wote waliopo duniani wanachanga mama mmoja aliyewahi kuishi miaka 130,000 hivi iliyopita.
Kwa namna ya pekee, upimaji wa [[DNA ya mviringo]], ambayo kila mmoja anarithi kwa mama tu, unaonyesha kuwa binadamu wote waliopo duniani wanachanga mama mmoja aliyewahi kuishi miaka 130,000 hivi iliyopita.


Halafu upimaji wa [[DNA ya mstari]], hususan [[kromosomu Y]], ambayo kila mwanamume anarithi kwa baba tu, umeonyesha kuwa wanaume wote waliopo duniani wanachanga baba mmoja aliyewahi kuishi miaka 70,000 hivi iliyopita, kidogo kabla ya watu wa kwanza kuhama bara la Afrika na kuenea [[Asia]] kufuatia pwani za [[Bahari ya Hindi]].
Halafu upimaji wa [[kromosomu Y]], ambayo kila mwanamume anarithi kwa baba tu, umeonyesha kuwa wanaume wote waliopo duniani wanachanga baba mmoja aliyewahi kuishi walau miaka 70,000 hivi iliyopita, kidogo kabla ya watu wa kwanza kuhama bara la Afrika na kuenea [[Asia]] labda kufuatia pwani za [[Bahari ya Hindi]].

Hata hivyo, upimaji wa [[DNA ya mstari]] kwa jumla umeonyesha miaka ya mwisho uwezekano wa kwamba baadhi ya binadamu wa leo, wale wasio wa kusini kwa Sahara, wana asilimia 1-6 ya urithi wa kibiolojia kutoka kwa aina nyingine za homo, hususan [[Homo neanderthalensis]] na ile ya pango la Donovani.

Kama hao waliweza kweli kuzaliana na [[Homo sapiens]] maana yake walikuwa [[spishi]] moja na yeye. Hapo asili ya binadamu inatakiwa kuhesabiwa ya zamani zaidi sana kuliko miaka 200,000.


== Uenezi wa binadamu ==
== Uenezi wa binadamu ==

Pitio la 16:23, 23 Aprili 2012

Binadamu

Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Primates (Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu)
Familia ya juu: Hominoidea (Wanaofanana zaidi na binadamu)
Familia: Hominidae (Walio karibu na binadamu kimaumbile)
Nusufamilia: Homininae
Jenasi: Homo
Spishi: H. sapiens

Binadamu ni neno linalomaanisha "Mwana wa Adamu", anayeaminiwa na dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu kuwa ndiye mtu wa kwanza.

Binadamu kadiri ya sayansi

Kisayansi jina hilo linaweza kutumika kwa maana ya Homo Sapiens ili kumtofautisha na viumbe wengine wa jenasi Homo ambao wote walitoweka walau miaka 12,000 hivi iliyopita.

Watu wote walioko leo hii ni spishi ileile na tofauti zinazoonekana kati ya maumbile yao katika sehemu mbalimbali za dunia ni kidogo tu.

Utafiti juu ya DNA umethibitisha kwamba binadamu wote wametokana na watu waliokuwepo Afrika Mashariki walau miaka 200,000 hivi iliyopita.

Kwa namna ya pekee, upimaji wa DNA ya mviringo, ambayo kila mmoja anarithi kwa mama tu, unaonyesha kuwa binadamu wote waliopo duniani wanachanga mama mmoja aliyewahi kuishi miaka 130,000 hivi iliyopita.

Halafu upimaji wa kromosomu Y, ambayo kila mwanamume anarithi kwa baba tu, umeonyesha kuwa wanaume wote waliopo duniani wanachanga baba mmoja aliyewahi kuishi walau miaka 70,000 hivi iliyopita, kidogo kabla ya watu wa kwanza kuhama bara la Afrika na kuenea Asia labda kufuatia pwani za Bahari ya Hindi.

Hata hivyo, upimaji wa DNA ya mstari kwa jumla umeonyesha miaka ya mwisho uwezekano wa kwamba baadhi ya binadamu wa leo, wale wasio wa kusini kwa Sahara, wana asilimia 1-6 ya urithi wa kibiolojia kutoka kwa aina nyingine za homo, hususan Homo neanderthalensis na ile ya pango la Donovani.

Kama hao waliweza kweli kuzaliana na Homo sapiens maana yake walikuwa spishi moja na yeye. Hapo asili ya binadamu inatakiwa kuhesabiwa ya zamani zaidi sana kuliko miaka 200,000.

Uenezi wa binadamu

Kutoka bara la Asia, watu walienea kwanza Australia na Ulaya, halafu Amerika toka kaskazini hadi kusini.

Hatimaye, katika karne ya 20 watu walikwenda kukaa kwa muda katika bara la Antaktika kwa ajili ya utafiti.

Upekee wake

Ingawa binadamu ana undugu mkubwa wa kibiolojia na sokwe na viumbe vingine, ustawi wake hauna mfano, kiasi cha kufanya wengi waamini tofauti iliyopo inadai kuelezwa kwa uwemo wa roho ndani ya mwili wake; roho ambayo dini hizo zinasadiki imetiwa na Mungu moja kwa moja.

Binadamu kadiri ya Biblia

Kadiri ya Biblia, binadamu ameumbwa “kwa mfano wa Mungu” (Mwa 1:27), mwenye roho isiyokufa.

Ameshirikishwa naye ukuu juu ya viumbe vyote vinavyoonekana.

Yeye tu ni nafsi, anaweza kujifahamu, kujitawala, kujitolea na kupendana na wengine.

Basi, anapaswa kulinda hadhi hiyo asitawaliwe na tamaa za kila aina.

Akifanya hivyo anatimiza mpango wa Mungu juu yake na kupendana naye.

Utotoni anasukumwa tu na haja za umbile lake, ambazo ni muhimu kwake na anazilenga bila ya kuhitaji juhudi.

Lakini akikua anaanza kutambua tunu za maadili na dini, ambazo ni njema, ni muhimu kwa zenyewe na zinamdai azifuate kwa nia imara hadi afikie lengo.

Kwa bidii za kudumu za namna hiyo anamlenga hasa Mungu, wema mkuu.

Anapopitia misukosuko ya ujana asikubali kushindwa na vionjo wala asikate tamaa, kwa kuwa Mungu amemuumba atawale hata nafsi yake na mwili wake.

“Mungu aliona kila kitu alichokifanya, na tazama ni chema sana” (Mwa 1:31).

Hata hivyo, baada ya dhambi ya asili anadaiwa bidii katika kutekeleza tunu ili wema alionao uzae matunda.

Basi, apanie kukuza wema aliojaliwa ili kesho awe mtu bora kama mzazi, raia, kiongozi wa dini na jamii n.k.

Penye nia pana njia hata ya kuelekea utakatifu utakaokamilika katika uzima wa milele.

Binadamu amekabidhiwa na Mungu dunia, lakini hasa amekabidhiwa nafsi yake mwenyewe. Itamfaa nini kujua na kutawala ulimwengu, asipojijua na kujitawala kweli?

Binadamu na elimunafsia

Karne XX imeleta maendeleo makubwa katika elimunafsia (= saikolojia). Hivyo anaweza kutambua vizuri mema na mabaya yaliyomo ndani mwake.

Lakini akitaka kujifahamu haitoshi asikilize mafundisho hayo au kusoma vitabu vingi juu yake.

Anahitaji kuishi katika mazingira bora ambapo ajisikie nyumbani, huru na mtulivu kwa kupendana na wenzake, kusikiliza watu wanaomfahamu (hasa walezi wake) wanasema nini juu yake, kujipatia muda wa kutulia peke yake na kujifikiria kulingana na maneno yao, kujichunguza kwa makini kuanzia miaka ya utotoni.

Kwa kuwa utu unategemea urithi, mazingira na utashi wa kila mmoja, anapaswa kuchunguza hayo yote yaliyochangia kumjenga.

Mara kwa mara ajitenge na watu na shughuli ili kutathmini tena maisha yake, kupima maono yake na kuweka maazimio ya kufaa, bila ya kusahau kwamba uhai wake ni fumbo, kwa kuwa unamtegemea Mungu.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Binadamu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Binadamu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

[1]

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA