Istanbul : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: csb:Sztambùl
d Roboti: Imeongeza lez:Истамбул
Mstari 142: Mstari 142:
[[lb:Istanbul]]
[[lb:Istanbul]]
[[lbe:Истамбул]]
[[lbe:Истамбул]]
[[lez:Истамбул]]
[[lmo:Istanbul]]
[[lmo:Istanbul]]
[[ln:Istanbul]]
[[ln:Istanbul]]

Pitio la 15:31, 28 Machi 2012

Faili:Kizkulesi at night.jpg
Mnara wa Binti ni kati ya alama za Istanbul.
Istanbul kwa macho ya ndege; juu iko Bahari Nyeusi, chini Bahai ya Marmara; sehemu ya Asia upande wa kulia, Ulaya upande wa kushoto wa Bospurus; "Pembe la dhahabu" ni mkono wa bahari unaoonekana chini upande wa Ulaya

Istanbul (kwa Kituruki unatajwa İstanbul) ni mji mkubwa zaidi katika nchi ya Uturuki, ukiwa na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya milioni 11 na milioni 15, ambao wanaufanya kuwa miongoni mwa miji mikubwa ya dunia. Huu ndiyo mji mkuu wa Mkoa wa İstanbul.

Eneo la Istanbul linaelekea pande zote mbili za mlangobahari wa Bosporus unaotenganisha Ulaya na Asia. Hivyo ni mji wa pekee duniani uliopo katika mabara mawili.

Kiini cha kihistoria kipo upande wa Ulaya kwenye sehemu yenye umbo la rasi baina Bahari ya Marmara na Pembe la Dhahabu ambayo ni mkono wa bahari unaoingia ndani ya nchi na hivyo mahali pa mji ulikingwa kwa bahari pande tatu.

Historia

Mji huu umebadilisha jina lake mara kadhaa katika historia yake ya zaidi ya miaka 2600. Awali jiji hilo liliundwa mnamo mwaka 660 KK na Wagiriki kwa jina la Bizanti. Mnamo mwaka 330 BK Kaisari Konstantino aliufanya kuwa mji mkuu wa Dola la Roma akaupanua ukajulikana kama Konstantinopoli (yaani mji wa Konstantino).

Konstantinopoli uliendelea kama mji mkuu wa Dola la Roma na baadaye Roma ya Mashariki uliojulikana pia kama Milki ya Bizanti hadi 1453 ambako mji ulitwaliwa na Waturuki. Tangu mwaka ule uliendelea kama mji mkuu wa Milki ya Osmani hadi mwaka 1923. Baadaye serikali ya Uturuki ilihamia Ankara.

Wakati wa Waosmani majina mbalimbali yalitumiwa: Konstantinopoli au kwa kifupi "Konstantiniye", halafu tangu karne ya 18 pia "Istanbul". Tangu 1873 jina rasmi kwa Kituruki lilikuwa "Istanbul".

Kuwepo kwa bandari kumepelekea mji huo kuwa kitovu cha biashara katika Uturuki.

Katika Ukristo ni muhimu kama makao ya Askofu wa pili kwa heshima kati ya Maaskofu wote duniani, kadiri ya orodha iliyotolewa na mitaguso mikuu ya karne ya 4.

Hadi vita ya kwanza ya dunia Istanbul ilikuwa na wakazi wengi wakristo hasa Wagiriki na Waarmenia. Waarmenia waliteswa wakati ule wakapungua na baada ya vita Wakristo walibaguliwa kwa jumla kwa hiyo wengi walihamia Ugiriki. Leo hii Wagiriki waliobaki ni 2000 - 3000 pekee na Waarmenia ni takriban 50,000.

Majengo

Istanbul huwa na majengo mengi ya kihistoria kama vile

  • Hagia Sofia ilikuwa kanisa kuu la Konstantinopoli ilijengwa kwa amri ya Kaisari Justiniano na kukamilishwa mwaka 537
  • Ukuta wa Theodosio ulioimarishwa kwa amri wa Kaisari huyu na kuwa kinga la mji hadi uvamizi wa Waturuki.
  • Makanisa ya kale, mengine kati yao yamebadilishwa kuwa misikiti
  • Mnara wa Galata uliojengwa na Waitalia katika sehemu yao ng'ambo la Pembe la Dhahabu
  • Misikiti mikubwa ya Milki ya Osmani kama vile Msikiti wa Suleymaniye, Msikiti wa Sultan Ahmad na majengo mbalimbali ya Mimar Sinan
  • Topkapi iliyokuwa ikulu ya masultani hadi 1923 na leo hii kati ya makumbusho muhimu duniani


Elimu

Mjini Istanbul kuna vyuo vikuu mbalimbali, baadhi yao:

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Istanbul kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA ak:Istanbul