Aljeri : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.4) (Roboti: Imeongeza zu:Algiers
d r2.7.2) (Roboti: Imebadilisha: ps:الجزيره
Mstari 132: Mstari 132:
[[pms:Algeri]]
[[pms:Algeri]]
[[pnb:الجیرز]]
[[pnb:الجیرز]]
[[ps:الجزیره]]
[[ps:الجزيره]]
[[pt:Argel]]
[[pt:Argel]]
[[ro:Alger]]
[[ro:Alger]]

Pitio la 00:21, 12 Machi 2012








Jiji la Algiers

Nembo
Nchi Algeria
Jimbo Jimbo ya Algiers
Waingereza walivamia meli za maharamia Algiers mwezi wa Agosti 1816
Majengo ya nyakati za ukoloni
Mtaa wa Algiers mwambaoni
Uwanja wa "Mashahidi wa Uhuru"
Algiers inavyonekana kutoka angani
Algiers inavyonekana kutoka angani

Algiers (Kiarabu مدينة الجزائر, madīnat al-djazā'ir ("mji wa visiwa"), Kifaransa Alger) ni mji mkuu pia mji mkubwa kabisa wa nchi Algeria ikiwa na wakazi milioni 2 (mwaka 2005), pamoja na mitaa ya nje takriban milioni tano. Iko mwambaoni wa Mediteranea. Algiers ni makao ya serikali na kitovu cha uchumi, biashara, utamaduni na mawasiliano nchini.

Historia

Mji ulianzishwa kama koloni ya Wafinisia katika karne ya 4 KK. Mahali palifaa kutokana na visiwa vinne vidogo vilivyokuwepo karibu na mwambao (lakini katika karne ya 17 BK viliunganishwa na bara). Baada ya kuenea kwa Dola la Roma ikawa mji wa Icosium na kuvamiwa na Waarabu Waislamu mwaka 702. Waberber wa kabila la Beni Mezghenna walikaa katika eneo hili. Mwaka 960 kiongozi wa Kiberber Buluggin ibn Ziri aliyekuwa gavana ya makhalifa wa Fatimiya wa Misri aliteua mahali pa Icosium na kujenga boma hapa. Mji uliitwa sasa "Al-djazair-Mezghenna" yaani "visiwa vya Beni Mezghenna". Hapa ndipo asili ya jina la leo "Al djaza'ir (الجزائر)" yaani "visiwa". Katika karne zilizofuata mji ulivamiwa na watawala Wamurabitun na Wamuwahidun kutoka Moroko. Baadaye mji ukawa chini ya masultani wa Algeria ya Kaskazini.

Mnamo mwaka 1302 Hispania ilifaulu kushika visiwa vidogo mwambanoni kwa miaka kadhaa hadi kufukuzwa tena na mharamia Barbarossa aliyeteka mji kwa niaba ya Sultani wa Uturuki. Tangu karne ya 16 BK Algiers ikawa mji wa kujitawala ndani ya Dola la Uturuki. Imekuwa mara kwa mara makao makuu ya maharamia ya Mediteranea ya magharibi. Maharamia hawa walishambulia jahazi za Wakristo kama Waitalia, Wafaransa, Wahispania na kadhalika na kuteka abiria pamoja na mabaharia. Waliuzwa kama watumwa au kurudishwa kwao baada ya kulipa pesa. Maharamia waliweza pia kushambulia miji ya Wakristo mwambaoni wa Mediteranea na kutwaa wakazi kama watumwa. Hali hiyo ilisababisha tena na tena majaribio ya nchi za Ulaya kuvamia Algiers lakini bila kufaulu hadi karne ya 19. Mwaka 1815 Marekani ilishambulia Algiers baada ya kupotea meli na raia kwa maharamia wa mji; mwaka 1816 Waingereza pamoja na Waholanzi walishambilia tena kwa kusudi ya kulinda meli na raia zao. Walifaulu kumlazimisha mtawala wa Algiers atie sahihi kwenye mkataba wa kutochukua tena Watumwa kutoka nchi za Ulaya ingawa biashara hii iliendelea kwa siri hata baadaye.

Mwaka 1830 Wafaransa walivamia mji na kuanzisha utawala uliokuwa mwanzo wa ukoloni wa Kifaransa katika Algeria.

Wafaransa walipanusha na kubadilisha mji wa Kiarabu na Kiberber. Katika karne ya 19 Wafaransa wengi walihamia Algeria hadi Algiers ilikuwa mji mwenya wakazi wengi Wafaransa kuliko wenyeji asilia waliokaa hasa katik mji wa kale ulioitwa "Kasbah". Wafaransa waliozaliwa Algeria walijiita "pieds noir" (miguu meusi). Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Alegria ilikuwa chini ya serikali ya Kifaransa katika maeneo yasiyovamiwa na Ujerumani hadi kuingiliwa na wanajeshi Waamerika na Waingereza mwaka 1942. Baadaye ikawa mji mkuu wa "Ufaransa Huru" hadi mwisho wa vita.

Tangu uhuru wa Algeria 1962 Algiers imekuwa mji mkuu wa Algeria. Akina pieds noir walio wengi waliondoka wakihofia uchungu baada ya vita ya ukombozi.

Marejeo

Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Aljeri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: