Tyra Banks : Tofauti kati ya masahihisho
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: lv:Taira Benksa |
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: kk:Тайра Бэнкс |
||
Mstari 123: | Mstari 123: | ||
[[ja:タイラ・バンクス]] |
[[ja:タイラ・バンクス]] |
||
[[ka:ტაირა ბენქსი]] |
[[ka:ტაირა ბენქსი]] |
||
[[kk:Тайра Бэнкс]] |
|||
[[lt:Tyra Banks]] |
[[lt:Tyra Banks]] |
||
[[lv:Taira Benksa]] |
[[lv:Taira Benksa]] |
Pitio la 19:32, 2 Machi 2012
Tyra Lynne Banks aliyezaliwa Desemba 4, 1973 nchini Marekani ni mwigizaji, mwanamitindo, mfanyibiashara na pia mwimbaji.[1][2][3] Alipata umaarufu kama mwanamitindo alipokuwa kwenye miji ya Paris, Milan, London, Tokyo na New York. Banks ni mbunifu na mtangazaji mkuu wa kipindi cha America's Next Top Model. Yeye pia ni mbunifu wa True Buauty na mtangazaji wa kipindi cha mahojiano cha The Tyra Banks Show.
Maisha yake
Tyra Banks alizaliwa mjini Inglewood, California; mwana wa Carolyn na Donald Banks.[4] Wazazi wake waliachana pindi Tyra alipokuwa na miaka sita. Baadaye, Carolyn aliolewa na Clifford Johnson. Banks alisoma katika shule ya John Burroughs iliyopo mjini Los Angeles na kisha akaenda katika shule ya upili ya Immaculate Heart.
Kazi yake
Mwanamitindo
Tyra alianza uanamitindo alipokuwa darasa la 11.[5] Baadaye, alienda mjini Paris kwa ajili ya kufanya kazi hii. Katika wiki yake ya kwanza mjini Paris, Tyra alipata umaarufu na mafanikio yaliyovunja rekodi kwani ilikuwa mwanzo wake katika uanamitindo. Yeye alishirikiana Anna Sui, CoverGirl, Badgley Mischka, Bill Blass, Chanel, Christian Dior, Dolce & Gabbana, H&M, McDonald's, Pepsi, Nike, Victoria's Secret na Yves Saint Laurent. Yeye ameonekana kwenye majalada maarufu kama Vogue, Harper's Bazaar, Cosmopolitan na Elle. Mnamo 1997, Tyra alipokea tuzo la VH1 Award for Supermodel of the Year. Mwaka huo huo, yeye alikuwa Mwamerika mweusi wa kwanza kutokea kwenye kasha ya jalada la Victoria's Secret.[6]
Filamu na televisheni
Banks alianza kuigiza kwenye msimu wa nne wa kipindi cha The Fresh Prince of Bel-Air ambapo aliigiza kama Jackie Ames. Aliigiza kwenye vipindi kama Felicity, MADtv na The Price Is Right
Hivi sasa yeye ana kipindi cha mahojiano cha The Tyra Banks Show, kilichoanza mnamo Septemba 12, 2005. Vilevile, yeye ni hakimu kwenye kipindi cha America's Next Top Model. Mnamo 2008, Banks alishinda tuzo la Daytime Emmy Award kwa kazi yake kwenye The Tyra Banks Show.
Banks amesema kuwa ataigiza kama Ursula Nyquist kwenye kipindi cha Gossip Girl msimu wa tatu.[7]
Muziki
Banks ameonekana kwenye video za muziki kama "Black or White" ya Michael Jackson, "Love Thing" ya Tina Turner na kwenye wimbo wa "Too Funky" ya George Michael.
Filamu
Film | |||
---|---|---|---|
Mwaka | Filamu | Aliigiza kama | Maelezo |
1995 | Higher Learning | Deja | |
1999 | Love Stinks | Holly Garnett | |
2000 | Love & Basketball | Kyra Kessler | |
Life-Size | Eve Doll | ||
Coyote Ugly | Zoë | ||
2002 | Halloween: Resurrection | Nora Winston | |
Eight Crazy Nights | Victoria's Secret Gown | Sauti yake pekee | |
2007 | Mr. Woodcock | Mwenyewe | |
2008 | Tropic Thunder | Mwenyewe | |
2009 | Hannah Montana | mwenyewe | [8] |
Vipindi | |||
Mwaka | Kipindi | Aliigiza kama | Maelezo |
1993 | The Fresh Prince of Bel-Air | Jackie Ames |
Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:
|
1999 | Felicity | Jane Scott |
Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:
|
Just Shoot Me! | Mwenyewe |
Aliigiza kwenye vipindi vifuatavyo:
| |
2000 | MADtv | Katisha Latisha Parisha Farisha Johnson |
|
2003-hadi leo | America's Next Top Model | Hakimu | Tyra ni hakimu na mtunzi wa kipindi hiki |
2004 | American Dreams | Carolyn Gill | |
All of Us | Roni | ||
2005-2010 | The Tyra Banks Show | Mtangazaji | Kipindi cha mahojiano |
2009 | Gossip Girl | Ursula Nyquist |
Marejeo
- ↑ Jason Clark (2008). "Tyra Banks:Biography on MSN". MSN. Iliwekwa mnamo 2008-07-18.
- ↑ "ABC News: Tyra Banks Experiences Obesity Through Fat Suit".
- ↑ "Tyra Banks On It - Forbes.com".
- ↑ "Tyra Banks Biography". FilmReference.com.
- ↑ Hirschberg, Lynn (June 1, 2008). "Banksable". New York Times. Check date values in:
|date=
(help) - ↑ http://findarticles.com/p/articles/mi_m1077/is_n7_v52/ai_19383832/
- ↑ http://www.usmagazine.com/news/tyra-banks-joining-gossip-girl-2009317}}
- ↑ "'Hannah Montana' Film Scenes Shot In Cool Springs Mall". NewsChannel 5.com. 2008-05-28.
Viungo vya nje
- Tyra Banks kwenye Internet Movie Database
- Tyra Banks katika All Movie Guide
- banks Tyra Banks katika People.com
- The Tyra Banks Show website
- The New York Times profile/interview