Ufini : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.2+) (roboti Nyongeza: vep:Suomenma
d r2.7.2+) (roboti Badiliko: ilo:Pinlandia
Mstari 170: Mstari 170:
[[ie:Finland]]
[[ie:Finland]]
[[ig:Finland]]
[[ig:Finland]]
[[ilo:Finlandia]]
[[ilo:Pinlandia]]
[[io:Finlando]]
[[io:Finlando]]
[[is:Finnland]]
[[is:Finnland]]

Pitio la 03:37, 22 Februari 2012

Ufini


Ufini (pia: Finland, Finlendi; Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia au Ulaya ya Kaskazini. Pia ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Imepakana na Norwei upande wa Kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia na watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini.

Mji mkuu ni Helsinki. Nchi ina wakazi milioni tano tu katika eneo la 338,000 km² hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu.

Watu

Kuna jumuiya tatu katika Ufini: Wafini wenyewe ambao ni 92% ya wakazi wote. Waswidi wako hasa upande wa kusini mwa nchi kwa jumla takriban 5.5% ya wakazi. Hasa visiwa vya Aland kuna Waswidi watupu walio na hali ya kujitawala ndani ya Ufini. Wakazi asilia ni Wasami wako kaskazini tu. Maisha yao yanategemea uwindaji na ufugaji. Wako wachache, jumla yao haifiki 1% ya wakazi wote.

Lugha rasmi ni Kifini na Kiswidi. Lugha ya Kifini ina asili ya Asia ya kati haina uhusiano na lugha nyingine ya Kiulaya isipokuwa lugha ya Waestonia inafanana. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.

Wakazi wenye lugha ya Kiswidi wako upande wa kusini mwa nchi kwa sababu Ufini ilitawaliwa na Uswidi kwa karne nyingi. Katika karne hizi walikuwepo Waswidi waliohamia Ufini lakini kuna pia Wafini walioanza kutumia Kiswidi pekee. Hasa kwenye visiwa vya Aland Kiswidi ni lugha ya pekee. Lakini Waswidi wa Ufini wanajisikia wako Wafini kisiasa. Viongozi wa kwanza baada ya uhuru wa Ufini mwaka 1917 walikuwa Waswidi Wafini.

Waja

Links

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA