Pablo Picasso : Tofauti kati ya masahihisho
d Robot: uk:Пабло Пікассо is a featured article |
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: vep:Pikasso Pablo |
||
Mstari 161: | Mstari 161: | ||
[[ur:پابلو پکاسو]] |
[[ur:پابلو پکاسو]] |
||
[[uz:Pablo Picasso]] |
[[uz:Pablo Picasso]] |
||
[[vep:Pikasso Pablo]] |
|||
[[vi:Pablo Picasso]] |
[[vi:Pablo Picasso]] |
||
[[vls:Pablo Picasso]] |
[[vls:Pablo Picasso]] |
Pitio la 04:19, 5 Februari 2012
Pablo Ruiz Picasso (25 Oktoba 1881 - 8 Aprili 1973) alikuwa mchoraji mashuhuri na pia mchongaji wa Hispania. Jina lake kamili ni Pablo Diego José Francisco de Paula Juan Nepomuceno María de los Remedios Cipriano de la Santísima Trinidad Clito Ruiz y Picasso.
Umuhimu wa Picasso
Picasso anahesabiwa kati ya wasanii wakuu wa karne ya 20. Alibadilisha uzoefu jinsi ya kuona dunia katika utamaduni wa Kimagaharibi wa Ulaya na Marekani. Mtindo wake wa uchoraji ulianza kutumia maumbo ya jiometria. Katika hatua hii aliathiwirwa na sanaa ya Afrika.
Picasso hakuwa mchoraji wa kwanza wala mchoraji wa pekee aliyetumia mibinu mipya lakini alijulikana kushinda wote na ile "sanaa ya kisasa" ilitambulishwa mara nyingi kwa lugha ya "picha kama Picasso".
Mwanzo wa kazi
Picasso alianza kuchora kwa umri mdogo wa miaka saba akisaidiwa na babake aliyekuwa mwalimu wa sanaa. Akiwa na miaka 10 aliandikishwa kwenye chuo cha sanaa na 1895 alipokelewa kwenye chuo kikuu cha sanaa huko Barcelona.
Alitembelea sana makumbusho penye taswira na sanamu za wasanii waliotangulia. Alipenda kusafiri penye maonyesho makubwa kama Madrid au Paris.
Taswira zake za awali badi zililingana zaidi na picha jinsi zilivyokuwa kawaida. Mwanzoni alipenda rangi ya buluu na mfano wake ni picha ya Suzanne Bloch hapo chini.
Athira ya Kiafrika na mtindo mpya
Mjini Paris alikuta maonyesho ya sanaa ya Kiafrika iliyomwathiri sana. Hii inaonekana katika "Mabinti wa Avignon" (1910).
Baadaye aliendelea kuvunja maumbile ya kawaida na kuyajenga upya kwa kutumia maumbo ya kijiometria. Mtindo huu uliitwa "cubisme" kwa Kifaransa yaani "umchemraba" kutokana na mchemraba kama umbo la kijiometria linalotumiwa kujenga upya maumbile ya yale yanayoonyeshwa kwenye picha.
Picasso aliendelea kujaribu mitindo mpya-mpya. Kati ya taswira zake zilikuwa maarufu sana kimataifa ilikuwa "Guernica" (1937) iliyonesha kikuli na maafya ya vita. Ilichorwa wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Hispania baada ya shambulio la wanahewa Wajerumani dhidi ya mji mdogo wa Guernica.
Kwa jumla imekadiriwa ya kwamba Picasso aliumba kazi za sanaa zaidi ya 20,000 kama vile taswira, picha za mchapo na sanamu.
Maisha ya binafsi
Picasso alioa mara mbili lakini alikuwa na wapenzi wengi. Alizaa watoto wanne na wake watatu.
Baada ya kuhamia Paris alibaki huko akakataa kurudi Hispania kwa sababu alimchukia dikteta Francisco Franco. Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia alikaa Paris chini ya utawala wa Wajerumani na wakati ule hakuweza kuonyesha kazi zake kwa sababu siasa ya Ujerumani ilichukia mtindo wake. 1945 alijiunga na chama cha Kikomunisti abakabi mkomunisti hata kama pia siasa ya Umoja wa Kisovyeti haikupenda mtindo wake.
Tangu 1961 aliishi katika Ufaransa ya Kusini alipoaga dunia 1973. Aliacha taswira maelfu ya akiacha
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pablo Picasso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |