Kasi ya nuru : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: ckb:خێرایی ڕووناکی
d r2.6.5) (roboti Nyongeza: ga:Luas an tsolais
Mstari 44: Mstari 44:
[[fr:Vitesse de la lumière]]
[[fr:Vitesse de la lumière]]
[[fur:Velocitât de lûs]]
[[fur:Velocitât de lûs]]
[[ga:Luas an tsolais]]
[[gl:Velocidade da luz]]
[[gl:Velocidade da luz]]
[[he:מהירות האור]]
[[he:מהירות האור]]

Pitio la 18:38, 4 Februari 2012

Kasi ya nuru imekubaliwa kuwa nuru inatembea mita 299,792,458 kwa sekunde moja katika anga. Kama nuru inapita katika hewa kasi yake inapungua.

Katika nadharia ya uhusianifu ya Einstein kasi ya nuru inadhaniwa kuwa ni ileile wakati wowote pia katika hali yoyote. Yaani kasi inabaki ileile hata kama nuru inatoka katika chombo chenye kasi yenyewe au kama mtazamaji ana mwendo wake mwenyewe. Katika nadharia hii hakuna mwendo mwenye kasi kushinda nuru. Kasi ya nuru imekuwa kipimo cha kimsingi katika sayansi za fizikia na unajimu.

Kasi hiyo haihusu nuru pekee inayoonekana kwa macho ya binadamu lakini pia kwa aina mbalimbali ya mnururisho kama mawimbi ya redio n.k.

Tangu safari ya kwanza ya watu kufika mwezi chini ya Mradi wa Apollo wa NASA tabia ya nuru kuwa na kasi ilionekana kwa watazamaji wote. Kila safari kituo cha NASA katika mji wa Houston iliwaita wanaanga kwa redio jibu ilichukua sekunde kadhaa hadi kufika kutokana na umbali wa kilomita lakhi tatu kati ya dunia na mwezi hivyo mazungumzo yaliendelea kwa vituo vya kusubiri hadi sauti imefika na kurudi. Kama siku moja wanaanga watasafiri mbali zaidi hadi Meriki au Zohali muda huu utaongezeka kutokana na umbali na kasi ya nuru inayobaki ileile.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA