Uhispania : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.5) (roboti Nyongeza: or:ସ୍ପେନ
d r2.7.2) (roboti Nyongeza: vep:Ispanii
Mstari 355: Mstari 355:
[[uz:Ispaniya]]
[[uz:Ispaniya]]
[[vec:Spagna]]
[[vec:Spagna]]
[[vep:Ispanii]]
[[vi:Tây Ban Nha]]
[[vi:Tây Ban Nha]]
[[vls:Spanje]]
[[vls:Spanje]]

Pitio la 15:04, 4 Februari 2012

Uhispania


Hispania ni nchi ya Ulaya ya kusini-magharibi. Imepakana na Ufaransa, Andorra, Ureno na eneo la Kiingereza la Gibraltar. Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki. Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Hispania.

Hispania bara ni sehemu kubwa ya rasi ya Iberia. Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi. Eneo la nchi ni 500,000 km² ambalo lina wakazi 44.395.286 (2006).

Lugha rasmi ni Kihispania lakini majimbo 17 yamepewa mamlaka ya kujitawala katika mambo mbalimbali pamoja na siasa ya kiutamaduni hivyo lugha za Kikatalan, Kivalencia, Kibaski na Kigalicia zimekuwa lugha rasmi za kijimbo pamoja na Kihispania. Wahispania walio wengi ni waamini wa Kanisa Katoliki.

Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba. Mfalme Juan Carlos I amevaa taji tangu mwaka 1978. Anaheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana. Lakini kisheria madaraka yake ni madogo.

Utawala umo mikononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwa kura za kidemokrasia.

Historia

Historia ya awali

Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Hispania walikuwa Wakelti. Katika karne za 1 KK Wafoinike walianzisha miji kwenye pwani na kuchimba madini hasa shaba na fedha.

Waroma

Waroma wa Kale walivamia na kutawala Hispania kwa karne kadhaa wakileta lugha yao ya Kilatini kilichopata kuwa msingi wa lugha za kisasa za Hispania. Kibaski pekee si lugha ya Kirumi.

Katika karne ya tano makabila ya Kigermanik walivamia Dola la Roma pamoja na Hispania. Wavandali na Wavisigothi walitawala sehemu kubwa ya Hispania.

Waarabu

Tangu mwaka 711 jeshi la Waarabu Waislamu liliingia kutoka Afrika ya Kaskazini na kutwaa sehemu kubwa ya Hispania hadi karibu milima ya Pirenei lakini watawala wa maeneo kadhaa katika kaskazini walijihami na kufaulu kudumisha uhuru wao. Waarabu walileta fani nyingi za maendeleo nchini.

Katika kipindi cha vita cha karne nyingi Wakristo wa Kaskazini walifaulu polepole kuwarudisha nyuma Waarabu hadi kusini ya nchi.

Mwaka 1492 mfalme Boabdil wa Granada mji wa mwisho wa Waarabu alishindwa na mfalme Ferdinand II wa Aragon na malkia Isabella wa Kastilia.

Makoloni ya Amerika

Wiki chache kabla ya kushinda huko Granada wafalme wa Hispania walimkubali nahodha Kristoforo Kolumbus na kumpa kibali cha kutafuta njia ya kufika Bara Hindi kupitia magharibi. Badala ya kufika India Kolumbus alifika kwenye visiwa vya Amerika ya Kati.

Huo ulikuwa mwanzo wa upanuzi wa Hispania katika "Dunia Mpya" ya Amerika. Wahispania walijenga dola kubwa la kikoloni na kutwaa karibu Amerika ya Kusini yote pamoja na Amerika ya Kati na Mexiko hadi sehemu za kusini za Marekani ya leo.

Katika miaka mia tatu iliyofuata Hispania ilitajirika sana kutokana na maliasili ya Amerika.

(ya kuendelea)

Jiografia

Ramani ya Hispania

Miji mikubwa

Picha za Hispania

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uhispania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA