Nikaragua : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: su:Nikaragua
d r2.6.5) (roboti Nyongeza: or:ନିକାରାଗୁଆ
Mstari 188: Mstari 188:
[[nov:Nikaragua]]
[[nov:Nikaragua]]
[[oc:Nicaragua]]
[[oc:Nicaragua]]
[[or:ନିକାରାଗୁଆ]]
[[os:Никарагуæ]]
[[os:Никарагуæ]]
[[pam:Nicaragua]]
[[pam:Nicaragua]]

Pitio la 19:49, 3 Februari 2012

Nikaragua


Ramani ya Nikaragua

Nikaragua ni nchi ya Amerika ya Kati yenye wakazi milioni 5.5. Imepakana na Honduras na Kosta Rika; upande wa magharibi ni pwani la Pasifiki na upande wa mashariki kuna pwani la Bahari ya Karibi.


Jina la nchi linasemekana kuwa mchanganyiko wa jina la wakazi asilia walioitwa "Nikarao" na neno la Kihispania la "agua" (=maji) kutokana na maziwa makubwa mawili nchini yanayoitwa Lago Managua na Lago Nicaragua. Maelezo mengine yanamtaja chifu wa wazalendo wakati wa kufika kwa Wahispania aliyeitwa "Nikarao".


Wakazi

Wakazi walio wengi sana hukalia maeneo ya mji mkuu Managua na pwani la Pasifiki. Sehemu kubwa (70 %) ni chotara kati ya wakazi asilia na Wazungu. Takriban asilimia 10 za Wanikaragua ni wa asili ya kiafrika wakikaa hasa kwenye pwani la Bahari ya Karibi.


Jiografia

Nikaragua ina volkeno nyingi; nyororo ya milima ya kivolkeno hufuata mstari wa pwani la Pasifiki. Sehemu ya juu ni mlima Mogoton mwenye kimo cha 2,438 m juu ya UB. Maziwa makubwa mawili ya maji matamu ni Lago Managua na Lago Nicaragua. Eneo upande wa Karibi ina wakazi wachache sana ni hasa eneo la misitu minene.

Historia

Nchi ilikuwa koloni ya Hispania tangu 1524. Mwaka 1821 iliachana na utawala wa Hispania pamoja na nchi jirani na kuingia katika Shirikisho la Amerika ya Kati. Tangu mwaka 1854 imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.


Viungo vya Nje

  • [www.pronicargua.org.ni Pronicaragua.org]


Sanaa na utamaduni

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nikaragua kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.