Norwei : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Badiliko: got:𐌽𐌰𐌿𐍂𐍅𐌹𐌲𐍃
d r2.6.5) (roboti Nyongeza: or:ନରଵେ
Mstari 249: Mstari 249:
[[oc:Norvègia]]
[[oc:Norvègia]]
[[om:Norway]]
[[om:Norway]]
[[or:ନରଵେ]]
[[os:Норвеги]]
[[os:Норвеги]]
[[pam:Norwega]]
[[pam:Norwega]]

Pitio la 19:22, 3 Februari 2012

Norwei


'Norwei (au Unowe au Norwe; kwa Kinorwei Norge/Noreg au rasmi huitwa Ufalme wa Norwei) ni nchi ya Skandinavia katika Ulaya ya Kaskazini.

Imepakana hasa na Uswidi, ila kaskazini na Ufini (Finland) na Urusi pia. Ina pwani ndefu kwenye Bahari ya Kaskazini na ya Atlantiki.

Mji mkuu ni Oslo.

Visiwa vya Svalbard na Jan Mayen katika bahari ya Aktiki ni maeneo chini ya Norwei.

Pia visiwa visivyokaliwa na watu vya Bouvet Island katika Atlantiki ya kusini na Peter I Island katika Pasifiki ya kusini ni maeneo chini ya Norwei.

Nchi inadai pia sehemu ya Queen Maud Land barani Antaktika penye kituo cha kisayansi cha Troll.

Ufalme wa Norwei umekuwa huru tangu mwaka wa 1905. Mkuu wake kwa sasa ni Mfalme Harald V.

Sikukuu ya taifa ni tarehe 17 Mei, ambapo husherekewa katiba ya Norwei ya mwaka wa 1814.

Bunge huitwa Stortinget na wanachama wake huchaguliwa na watu kila baada ya miaka minne.

Watu

Takriban watu milioni 4.6 wanaishi nchini Norwei. Wengi wao ni Wakristo wa madhehebu ya Kilutheri.

Miji

Mji mkuu wake una wakazi wanaozidi 530,000. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Bergen wenye wakazi 230,000 na Trondheim wenye wakazi 150,000; yote miwili imewahi kuwa miji mikuu ya Norwei katika miaka ya mwanzoni.[1]

Uchumi

Norwei ilikuwa nchi maskini ya wakulima na wavuvi, lakini tangu kupatikana kwa mafuta ya petroli baharini imekuwa kati ya nchi tajiri kabisa duniani.

Marejeo

  1. "Trondheim - the official website". Iliwekwa mnamo 2009-09-04. 

Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Norwei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA