Kicheche : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
dNo edit summary
Nyongeza jamii
Mstari 39: Mstari 39:


[[Jamii:Mbwa na jamaa]]
[[Jamii:Mbwa na jamaa]]
[[Jamii:Wanyama wa Afrika]]

Pitio la 22:37, 31 Januari 2012

Kicheche
Kicheche-nyoka (Poecilogale albinucha)
Kicheche-nyoka (Poecilogale albinucha)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Mustelidae (Wanyama walio na mnasaba na chororo)
Nusufamilia: Mustelinae (Wanyama wanaofanana na chororo)
Jenasi: Galictis Bell, 1826

Ictonyx Kaup, 1835
Poecilogale Thomas, 1883 Vormela Blasius, 1884

Spishi: Angalia katiba

Vicheche au cheche ni wanyama wa jenasi mbalimbali katika familia Mustelidae. Wanyama hawa ni miongoni mwa wale wanaotoa vundo mbaya kabisa. Wataalamu wengine wanadai kwamba kicheche wa kawaida ananuka vibaya kuliko wanyama wote. Vundo hii inatoka matezi karibu na mkundu kama mnyama akitishwa, na kwa kawaida adui atoroka. Spishi zote zina pua, kidari, tumbo na miguu nyeusi. Zile za Afrika zina milia myeupe na myeusi mgongoni, zile za Amerika zina mgongo kijivu na ile ya Ulaya ina mgongo njano wenye madoa meusi. Vicheche hula wanyama, ndege na mijusi wadogo, wadudu, samaki, amfibia, nyoka na hata matunda na manyasi.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha