Majadiliano ya mtumiaji:Riccardo Riccioni : Tofauti kati ya masahihisho

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 294: Mstari 294:


::Pamoja na hayo, hatujaingiza mikoa (k. mf. Njome, Simiu) na wilaya mpya za Tanzania (k. mf. Gairo, Nyasa). --[[Maalum:Michango/41.221.34.70|41.221.34.70]] 08:10, 25 Januari 2012 (UTC)
::Pamoja na hayo, hatujaingiza mikoa (k. mf. Njome, Simiu) na wilaya mpya za Tanzania (k. mf. Gairo, Nyasa). --[[Maalum:Michango/41.221.34.70|41.221.34.70]] 08:10, 25 Januari 2012 (UTC)

::Asante kwa jibu. Kuhusu mikoa na wilaya mpya - niko mbali. Unaweza kuanzisha makala ?'''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 13:08, 25 Januari 2012 (UTC)
::Asante kwa jibu. Kuhusu mikoa na wilaya mpya - niko mbali. Unaweza kuanzisha makala ?'''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 13:08, 25 Januari 2012 (UTC)

:::Sina DATA za kutosha. --[[Maalum:Michango/41.221.34.70|41.221.34.70]] 14:26, 28 Januari 2012 (UTC)

Pitio la 14:26, 28 Januari 2012

--Kipala (majadiliano) 19:12, 27 Machi 2008 (UTC)--Kipala (majadiliano) 19:12, 27 Machi 2008 (UTC)Bwana Ricardo, karibu sana kwenye wikipedia ya Kiswahili! Twamfurahia kila mmoja anayejiunga nasi na kuchangia. Tuko wachache tu na kazi ni kubwa kujenga Kamusi Elezo ya Kiswahili. Ukiwa na swali uliza tu. --Kipala 17:52, 16 Desemba 2007 (UTC)[jibu]

Fransisko wa Asizi

Riccardo, salam. Nd. Riccardo, ile makala ya Fransisko wa Asizi, umeandika safi sana na inaeleweka. Lakini je vipi kuhusu mwaka aliozaliwa huyu bwana unaujua? Natumai utakuwa umeitafsiri kutoka wiki zingine ama sivyo? Natumai ndivyo!! Basi kama utaweza kuandika mwanzo kabisa mwaka aliozaliwa itakuwa bora zaidi. Labada nikupe mfano mdogo: Fransisko wa Asizi (tarehe na mwaka aliozaliwa) alikuwa mtakatifu kutoka nchini Italia. Asizi alizaliwa katika mkoa wa Umbria, wilaya ya Perugia, Italia.... Kisha unaweka kama ndugu na mambo mengine!! Haya basi kama hujaelewa labda umwulize Kipala atakupa habari zaidi!! Kingine usisahau kuweka InterWiki katika makala yako kama ipo katika wiki zingine-[[it:Fransisko of Asizi]] (sijui kwa lugha ya Kitaliano wanahitaje) lakini inategemea na lugha vyovyote vile inaswihi. Kingine kuweka vichwa katika makala, hili nenda kaangalie makala yako utaona nimefanya vipi mpaka kimekuja kichwa cha habari-Fransisko wa Asizi. Sina mengi na nakutakia kheri ya mwaka mpya na furaha tele moyoni!!--Mwanaharakati 05:08, 7 Januari 2008 (UTC)[jibu]

Kuna kitu nimesahau kukueleza. Kuweka jamii au category katika makala, mfano: [[Category:Watakatifu wa Italia]] au [[Category:Watakatifu]] na nyingine ya mwaka aliozaliwa -unaweka mabano kama hayo kisha unaadika (Waliozaliwa 19 na...) kama kafa unaandika Waliofariki (mwaka aliokufa). Natumai utakuwa umeelewa!!--Mwanaharakati 05:20, 7 Januari 2008 (UTC)[jibu]

Ushauri

Salam. Ukiwa bado humchanga katika wiki hii, ni vyema ku-login kabla ya kuumba makala!!! Nimeona baadhi ya makala umeandika bila ku-login, kisha nikafikiri ni Kipala aliyefanya hiyo hivyo, kwani yeye ndiye huwa na kawaida hiyo!! Basi endelea na kazi yako Ndugu, wako katika ujenzi wa Wikipedia,--"Mwanaharakati" (talk) 12:19, 28 Februari 2008 (UTC)[jibu]

Mpanglio wa makala

Salaam! Kuna mapendekezo kuhusiana na muundo wa makala na vichwa vyake. Naomba angalia hapa kwa maelezo zaidi....--"Mwanaharakati" (talk) 12:43, 11 Machi 2008 (UTC)[jibu]

Salaam! Tukiwa tunaendelea na mada yetu ya vichwa vya habari katika makala, labda nikueleze kingine nimekiona! Ni vyema wakati wa kutaka kumwachia mtu ujumbe katika kurasa ya majadiliano, uwe unaanzia chini na sio juu. Ukifanya hivyo inakuwa rahisi mtu kufahamu ujumbe upo wapi. Vinginevyo uangalia mabadiliko ya mwisho ndiyo utajua ujumbe upo wapi. Pendekezo: Ni vyema uwe unaweka (au kuacha ujumbe wako kuanzia chini). Vichwa vya habari: Labda nikuonyeshe namna ya kuweka vichwa vya habari

==Hapa unaweka maelezo husika na kichwa cha habari hiki==

Hapa chini yake unaaza kuelezea vile habari kama kilivyo kichwa chake cha habari.

Naomba angalia makala hii :Maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi wa Ulaya na vichwa vyake vya habari, labda utapata mwelekeo mzuri zaidi. Ukiwa unaona bado huja elewa basi nijulishe au mwulize mkabidhi yoyote atakupa maelekezo zaidi! Kila lakheri....--Mwanaharakati (majadiliano) 04:18, 25 Machi 2008 (UTC)[jibu]

Viungo vya nje

Salam. Ndugu Riccardo, hamna uwezekano wa kupata viungo vya nje katika makala unazo-changia? Maana naona makala nyingi umeandika bila ya viungo vya nje, wakati ukiziangalia katika Wikipedia zingine unazikuta wamewekea viungo vya nje. Je vipi utafanya ili uweze kuweka hata viungo vya nje katika baadhi ya makala utakazo changia-zenye kuhitaji viungo vya nje?--Mwanaharakati (majadiliano) 11:57, 27 Machi 2008 (UTC)[jibu]

Ualimu

Salaamu Ricardo,nafurahi sana kuona kazi yako. Nina neno kuhusu ualimu naomba utazame ukurasa wa majadiliano huko. ̰-Kipala (majadiliano) 19:12, 27 Machi 2008 (UTC)[jibu]

Hongera ya makala 7,000

Salam nyingi zikufikie Nd. Riccardo! Ninapenda kukupa hongera kwa kusukuma wiki yetu juu ya kiwango cha makala 7,000! Nafurahia kuona tumefikia makala elfu saba. Naona kama naota kufikia kiwango hicho, ingawaje si nyingi hivyo lakini tumefika!. Basi tuendelee kushauriana na kuvumiliana!--Mwanaharakati (majadiliano) 07:32, 21 Aprili 2008 (UTC)[jibu]

Fransiko

Ricardo, niliandika hapa kitu juu ya umbo la makala lakini nimeifuta tena kwa sababu sijaona ya kwamba umeshabadilisha mwenyewe. --Kipala (majadiliano) 11:19, 14 Mei 2008 (UTC)[jibu]

Vitabu vya Biblia

Riccardo salaam, nimeona umechapa kazi kan bisa kuhusu vitabu vya Biblia. Ombi langu ni: tujaribu kushikamana pamoja. Labda umeona ya kwamba hata Oliver na mimi tumeshaanza makala kadhaa juu ya vitabu vya Biblia lakini sijandelea kwa muda mrefu. Hapa naona kuna mamabo mawili yanaofaa tukumbuke: tupatane juu ya majina na jamii.

  • Kwanza tukiwa na makala nyingi napendekeza tutumie jamii za "Vitabu vya Agano la Kalre" na "Vitabu yva Agano Jipya" zote mbili chini ya "Category:Biblia". Menginevyo jamii zitajaa mno tukiweka kila kitu chini ya Biblia. Vile vile misahafu naona tutumie hii wka ngaziy a juu maana yake tukitaja vitabu vya dini mbalimbali si sehemu za kila kitabu cha kila dini (kwa mfano upande wa Uhindu tunapata nyingi mno, kama vile upande wa Ukristo).
  • Pili naomba ukiongeza kumbuka makala za

kwa sababu hapa kuna orodha na tukiunda makala kwa jina tofauti orodha hizi si msaada tena. Au tunafanya kazi mara mbili, linganisha Kumbukumbu la Sheria (Biblia) na Kumbukumbu la Sheria. Kumbe makala imeshakupatikana tayari. Basi sasa tuunganishe. Halafu ona jinsi nilivyofanya kwa Ruth: wewe uliandika Kitabu cha Ruth halafu nikaweka kiungo cha #REDIRECT kutoka orodha inapoandikwa kw< umbo la "Ruthu". Unaonaje? --Kipala (majadiliano) 14:43, 2 Juni 2008 (UTC)[jibu]

Salaaam! Namna ya kuelekeza ukurasa mmoja kuelekeza kwingine ni:
  • #REDIRECT [[andika ukurasa unaotaka ku-redirect hapa]].
Mengineyo, waone wataalamu wa "Dini", yaani Kipala! Ushauri: Naona mara nyingi ukiandika ujumbe, huwa hakuna jina lako linalotokea katika ukurasa wa majadiliano wa mtu uliyemwachia ujumbe. Fanya hivi: --~~~~ kisha yenyewe itaandika jina lako, muda, tarehe n.k. Kazi njema na kila lakheri! Wako katika ujenzi wa Wikipedoia hii ya Kiswahili,--Mwanaharakati (majadiliano) 10:56, 3 Juni 2008 (UTC)[jibu]

Kutia sahihi

Salam, Riccardo. Kuna kitu nimeona wakati wa kumaliza kuandika, jina lako linatoka bila kiungo. Hapa naona mambo mawili: Huenda akawa umeilemaza ile sehemu ya kuweka automatic link(angalia "mapendekezo yangu - raw signature"). Pia inawezekana ukawa unakosea namna ya kujisajilisha ili uweze kupatikana katika viungo hivi vya wiki. Angalia mfano huu tena kwa njia ya picha kisha uwe unafanya hivyo:

Faili:Kutia Saini.JPG
Fuata hizi alama kama zilivyo.

Samahani lakini kama nitakuwa na kukera katika kukumbushia namna ya kijisajili. Kazi njema na natumai utakuwa umeelewa! Endapo ukiwa bado, basi nijulishe...--Mwanaharakati (majadiliano) 13:07, 12 Juni 2008 (UTC)[jibu]

Salaaam! Riccardo, nimeona makala nyingi ukiwa unaandika vichwa vya habari kwa "herufi kubwa". Kwani haiwezekani kuandika herufi ndogo?? Unaombwa ufuate format ya wikipedia jinsi inavyokwenda! Usijisikie vibaya pale unapoelezwa kwani tupo katika kuboresha makala zetu! Hata mimi nilikuwa nafanya kama unavyofanya, lakini Kipala akanieleza namna ya kufanya vyema!!! Basi tushirikiane katika kazi ili tuwe wabora zaidi. Mengineyo: Ujumbe wa juu natumai umeuona, na kama umeona naomba nifute ile picha!--Mwanaharakati (majadiliano) 10:06, 13 Juni 2008 (UTC)[jibu]
Umefaulu. Ila usiandike jina lako, yenyewe itaandika jina lako na muda uliacha ujumbe ule. Hongera na kazi na tuendelee kushauriana! Wako katika ujenzi wa Wikipedia hii,--Mwanaharakati (majadiliano) 10:30, 13 Juni 2008 (UTC)[jibu]

Masharti ya makala

Salaam Riccardo umefanya kazi kubwa ya kutunga makala mengi juu ya vichwa vyenye maana. Nashukuru. Lakini naona tatizo juu ya makala kadhaa kulinganana na masharti ya kamusi elezo. Kwa upande mmoja makala kuhusu maazimio ya mtaguso wa pili wa Vatikani hayafuati muundo wa makala. Maana yake mwanmzoni hazielezi waziwazi neno hili ni nini bali zinaanza na maelezo juu ya nia au mawazo ya Mtaguso. Hii haisaidii kueleweka vema. Halafu kuna jambo la pili nimeona mara nyingi namna ya mahubiri inayochanganywa na habari. Hii si mtindo wa kamusi elezo. Labda kama ukiandika kwa ajili ya homepage ya kanisa lako ingekuwa sawa. Lakini hapa tunahitaji maelezo yaliyo wazi kwa mtu yeyote. Kama Waislamu, Wakristo wa madhehebu mengine na watu wanaokanusha dini wanafanya hivihivi wikipedia yetu haieleweki tena. Naona haja kuleta masahihisho hapa. Ningeomba usinedelee kuandika makala kwa muundo huohuo bali tujitahidi pamoja kuleta mpanglio unaofaa. Napenda kurudia ya kwamba naona makala yote yanahusu mada muhimu lakini hatuna budi kusaidiana kutunza kiwango cha ubora fulani.--Kipala (majadiliano) 17:09, 15 Juni 2008 (UTC)[jibu]

Nimesahihisha kidogo mwanzo wa makala kuhusu "Dei Verbum". Pamoja na muundo niliona mafundisho au mahubiri ya kidhehebu. Ilikuwa vema ya kwamba ulinikumbusha juzi ya kwamba haikuwa sahihi kuonyesha mafundisho ya Kiprotestant juu ya idadi ya vitabu vya Agano la Kale. Nimekubali kabisa. Vivyo hivyo hakuna mahali hapa kuingiza mafundisho ya kidhehebu juu ya madhehebu mengine.
Mfano: Si kweli ya kwamba viongozi Waprotestanti walikataa ualimu wa kanisa; kinyume chake ualimu huu unasisitizwa sana! Tofauti ilikuwa ya kwamba wakati ule Waprotestanti hawakukubali Kanisa Katoliki kuwa kanisa kweli. Sasa tuna kazi ya kueleza mawazo haya katika makala juu ya historia ya kanisa au historia ya mafundisho ya kidini na hapo ni sawa. Lakini haifai kurudia matamko ya upinzani wa kidhehebu ndani ya makala kama hii, isipokuwa kama ni kweli sehemu ya kichwa fulani. Lakini inapaswa kuelezwa kama maoni fulani si kama habari halisi. Tuhurumie wasomaji wetu wanaotoka katika mazingira mbalimbali. Naomba tuelewane hapa na kusaidiana. --Kipala (majadiliano) 17:09, 15 Juni 2008 (UTC)[jibu]

Agano la Kale

Ricccardo, asante kwa kunikumbusha. Samahani lakini sina uhakika unalenga nini yaani makala gani. Pale nilipoangalia nakuta vitabu vipo bila shaka unamaanisha sehemu nyingine ambako sioni. Naomba fanya hivi: weka kiungo (link) pale unapoandika kwenye ukurasa wangu ili nifike palepale. Mfano: Agano la Kale kuna vitabu vyote unavyotaja. Je wewe unalemha nini hasa? (halafu: Kuanzia kesho kutwa sitakuwepo kwa wiki 4 - naomba uvumilivu wako). --Kipala (majadiliano) 22:30, 16 Julai 2008 (UTC)[jibu]

Nimeelewa. Ilikuwa Template:Biblia_AK. Nimesahihisha. Halafu ilikuwa nini juu ya kulinganisha "Biblia ya Kiebrania" na "Agano la Kale"? --Kipala (majadiliano) 07:42, 17 Julai 2008 (UTC)[jibu]
Nimejibu ujumbe wako hapa!--Mwanaharakati (majadiliano) 15:10, 25 Agosti 2008 (UTC)[jibu]

Hi Ricardo Riccioni ;)

Hi! How are you? Could you please help me add a couple of sentences to the Kiswahili version of this interesting article?

Thanks so much! -Ivana Icana (majadiliano) 22:30, 6 Septemba 2008 (UTC)[jibu]

Lugha

Riccardo, salam. Eti, umefikia wakati wa wewe kujiwekea viwango vya lugha uzifahamuzo katika ukurasa wako wa mtumiaji! Hapa kuna orodha chache ya mifano hai yenye kuonyesha lugha unazozijua. Angalia hizi:

Haya, katika kila kodi ya lugha, kwa mfano: sw-2 au 3, ni kiwango cha lugha unachokifahamu. Ikiwa en-2, 3, 4, ni namna ya kutaja vyema uwezo wa ujua wako wa lugha! Ukiona unajua zaidi ya namba 1,2,3 basi ongeza hadi nne katika kila kodi ya lugha, halafu ukimaliza kopi hayo mabano yote kisha nenda ka-paste katika ukurasa wako wa mtumiaji! Chukua hizi:

{{Babel|it|sw-3|en-3|es-3|fr-2|la-1}}

Karibu sana!--Mwanaharakati (Longa) 05:54, 13 Oktoba 2008 (UTC)[jibu]

Tayari nsihaongeza msingi wa lugha "A" katika Kihispania! Ni kama uonavyo hapo juu. Natumai kwa hili tushamalizana, kwa maelezo mengine zaidi, tafadhali uliza tu ukijisikia wataka kuuliza! Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 13:08, 1 Novemba 2008 (UTC)[jibu]

Picha

Riccardo Riccioni, salam. Namna ya kuweka picha ni rahisi sana ndugu yangu! Hebu fuata taratibu hizi kisha tuone kama tutafaulu katika kuelekezana huku. Andika:

[[Image:Jina la picha.jpg, .png, .svg, .gif n.k.|thumb|hapa weka kulia au kushoto (kwa Kiingereza)|ukubwa wa picha=250px n.k.|Maelezo ya picha, kisha]]

Kingine: Ukitaka kutumia formula hiyo, tafadhali usi kopi na hayo maandishi yaliyoandikwa. Chukua maelezo matupu bila ya nowiki! Haya, tazama picha jinsi inavyokuja kwa hapa: [[Image:Flag of Italy.png|thumb|left|15px|Bendera ya Italia]]. Ukiona bado hujaelewa, basi nijulishe nitakuelekeza zaidi!--Mwanaharakati (Longa) 13:21, 10 Novemba 2008 (UTC)[jibu]

Ndugu, sijaelewa. Pole! Kwanza sijui nowiki ni nini. Pili sijui picha niichukue wapi. Tatu nijueje ukubwa. Nilichoelewa ni kulia na kushoto... Pamoja na hayo, naona unapenda kufahamu niko wapi: si mbali na wewe, naishi Morogoro, hivyo itakuwa rahisi kukutana siku yoyote... Nimetekeleza agizo lako kuhusu Holy See. Natumaini inatosha. Kama ningeweza, ningeweka picha nzuri iliyopo mwanzoni mwa makala hiyo kwa Kiitalia! Pia katika user page yangu ya Kiingereza nimepandisha maksi zangu za Kiswahili kwa kuandika 4. Mbona mimi ni Mtanzania? Ila nimeona template hiyo haipo katika Kiitalia na Kiswahili. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 23:19, 15 Novemba 2008 (UTC)[jibu]
Duh! Ebwana eeeh! Basi mie sikujua kamama wewe ni Mtanzania. Lakini mbona una jina la Kiitalia (hata lugha yako ya kwanza ni Kiitalia!). Basi naona unge badilisha ile sehemu ya Kiswahi uweke (sw tupu bila namba!) Maana wewe ni Mswahili? Aaah, nahisi umekaa Tanzania mda mrefu, kiasi hata ujue Kiswahili kama Mzawa! Haya, basi eti picha ujuaelewa? Naona unge fungua ile picha na uitazame kama inatoka Wikimedia Commons (Commons ni mradi unaopakia picha kwa ajili ya Wikipedia zote au hata mieadi yote ya Wiki!). Basi tazama hii jinsi nilivyoongeza picha halafu muda mwingine ufanye kama hivyo. Pale utaona maandishi ya kijani (hayo ndiyo niliongeza mimi!). Ukiona bado hujaelewa, basi niulize tena kisha nitakueleza vyema! Na kuhusu mie, nina kaa huku kwetu shamba Kiwalani! Bwana akubariki,--Mwanaharakati (Longa) 12:19, 17 Novemba 2008 (UTC)[jibu]

Ombila la tafsiri ya makala

Salam nyingi zikufikie Nd. Riccardo Riccioni popote ulipo! Naomba kama utapata muda wa kuweza kutafsiri makala ya Holy See kutoka lugha ya Kiingereza au Kitaliano kama utapenda! Nataka kujua kuhusiana na hiyo Holy See, yaani uandike makala ya Holy See katika Wikipedia hii, ikiwezekana kwa Kiswahili itakuwa bora zaidi ama unaonaje?--Mwanaharakati (Longa) 13:21, 10 Novemba 2008 (UTC)[jibu]

Mambo mbalimbali

Ndugu Riccardo, salaam! Nakushukuru kwa jumbe zako kadhaa za siku zilizopita, na sina budi kukuomba radhi kwa kimya yangu. Upande wa Carl Hinton, nitaendelea kuangalia sehemu ambazo amenakilisha tu kutoka katika "Biblia Inasema". Nimesafiri bila nakala yangu ya kitabu hicho kwa hiyo itanichukua muda kadhaa kabla sijaweza kuendelea na kazi hii ya ufutaji tena. Upande wa kichwa cha makala mbalimbali, mimi sioni shida, hasa kwa vile makala za zamani zitarejea zile za kisasa. Ila kuhusu "vita" nakubaliana na Ndugu Muddyb kwamba neno hili liendelee katika ngeli ya nomino ya 9 (yaani kihusishi chake kiwe "ya", siyo "vya"). Nyakati hubadilika. Kwa vyovyote turejee moja kwa nyingine. Basi, nakushukuru kwa kazi yako inayonifurahisha sana (mbona umehangaika ingewezekana kunichukiza? Haikufanya hivyo hata kidogo!). Na kazi njema! Baba Tabita (majadiliano) 14:27, 10 Novemba 2008 (UTC)[jibu]

Mtaguso

Ndugu Riccardo, salaam. Naomba uangalie maoni kwenye ukurasa wa majadiliano ya Talk:Mtaguso Mkuu na pia makala ya Mitaguso_ya_kiekumene. Ningefurahi tukiweza kushirikiana katika jambo hili. --Kipala (majadiliano) 08:51, 18 Novemba 2008 (UTC)[jibu]

Hongera ya makala 8,000

Salam nyingi zikufikie Nd. Riccardo! Ninapenda kukupa hongera kwa kusukuma wiki yetu juu ya kiwango cha makala 8,000! Nafurahia kuona tumefikia makala elfu nane. Nikikumbuka vile ulivochangia kwa hali na mali ili walau nasisi Waswahili tufikie elfu kadhaa, Naona sasa tumesogea! Shukrani za dhati zikufikie na tuendelee kushauriana na kuvumiliana--Mwanaharakati (Longa) 14:31, 19 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Badiliko la baadhi ya viungo!

Riccardo, salam! Kuna mabadiliko katika baadhi ya viungo vyetu! Sasa hivi kuna baadhi ya viungo vyetu vinatumika kwa Kiswahili. Kwa mfano CATEGORY hii sasa hivi ipo kama JAMII au picha, zamani ilikuwa Image:jina la picha. hiyo na hiyo. Lakini sasa ni Picha: halafu jina.... Ila zote zinafanya kazi, yaani kwa Kiswahili na Kiingereza! Lakini bora zaidi tukitumia kwa lugha yetu, au wewe unaonaje?--Mwanaharakati (Longa) 09:04, 24 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Mpendwa, nafurahi kuona maendeleo hayo ya lugha yetu. Tusonge mbele bila ya kugeuka nyuma! Ila sehemu nyingine kuna makosa: kwa mfano ukarasa badala ya ukurasa. Naomba nyinyi wataalamu mrekebishe. Kuhusu picha nimefaulu kuziingiza kwa njia tofauti na ile uliyonielekeza, yaani nazikopi kutoka lugha nyingine, ila mara mojamoja inashindikana. Mah! Hatumalizi kujifunza... Kuhusu uraia wangu, ni kama ulivyoelewa: nilizaliwa Italia, lakini nipo Tanzania tangu mwaka 1984. Nimekuwa raia tangu mwaka 1997. Asante. --196.45.46.171 06:44, 25 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Sawa, lakini hujaonyesha uo ukurasa wenye jina la "UKARASA". Ni bora kuonyesha kiungo kile ambacho umeokiona kinamakosa! Ahsante--Mwanaharakati (Longa) 05:42, 27 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Kwa mfano hapa pembeni na hapa chini katika Majadiliano ya mtumiaji. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 16:04, 29 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Galileo

Hongera na asante kwa masahihisho ya maana! Nakiri nina udhaifu wa kupitia tena hasa nikiandika usiku manane wakati mwingine sioni makosa (tahajia, muundo wa sentensi). Basi tuendelee kusaidiana. Kitu kidogo: nashauri usitumie "jamii" badala ya "category". Najua inatakiwa kuwa sawa lakini bado kuna mdudu ndani yake --Kipala (majadiliano) 22:11, 29 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Ndugu,kweli nimeona unafanya kazi kubwa usiku, na si mara mojamoja kama mimi... Hongera na heri kwa mwaka mpya! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 22:33, 29 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Ni vyema kutoa sababu zinazopelekea shida ya JAMII au CATEGORY. Kuna tatizo lolote lililotokea au kutofautisha, kuleta tabu, au kutoonekana kwa makala pindi utakapoweka kiungo cha JAMII badala ya CATEGORY? Naomba nifahamishwe ili niende kuwaeleza wale Madevoloper wa MediaWiki haraka iwezekanavyo--Mwanaharakati (Longa) 05:49, 30 Desemba 2008 (UTC)[jibu]
Mimi sijaona tatizo lolote. Sasa mmeniweka njia panda: nionekane mkaidi kwa Kipala au kwa Muddy Blast? --196.45.46.171 13:34, 31 Desemba 2008 (UTC)[jibu]

Ndugu Riccardo. Hongera kwa kazi njema! Miezi miwili iliyopita, ndugu wetu Kipala aliuliza kuhusu hatimiliki ya makala ya Historia ya Wokovu. Nadhani ni wewe uliyeandika makala hiyo kwa sehemu kubwa kabisa. Ikiwa umenakilisha kutoka kitabu fulani na kuvunja hatimiliki, naomba urekebishe na kufupisha makala. Hata hivyo imekuwa ndefu mno kwa ajili ya kamusi elezo. Tukazane kusaidiana na kazi njema. Umesalimiwa na Baba Tabita (majadiliano) 16:22, 23 Januari 2009 (UTC)[jibu]

Ndugu, usiwe na wasiwasi: mwandishi wa makala hiyo ni mimi mwenyewe tu. Ni kweli kwamba ni ndefu, lakini historia ya binadamu ni ndefu zaidi... ni vigumu kusimulia miaka elfu kwa nusu saa! --196.45.46.171 06:41, 25 Januari 2009 (UTC)[jibu]

Hongera ya makala 9,000

Riccardo, salam. Ni siku 43 nyuma, yaani, 19 Desemba 2008 hadi tar. 2 Februari 2009 - 9,000. Leo tuna makala 9,000. Inazidi kuifanya Wikipedia yetu kuwa vilevile ya pili kama jinsi ilivyozoeleka! Sina maneno mengi, ila ni kukutakia furaha ya kufika hapa tulipo! Pia, maisha mema na kazi kwa ujumla. Kila la kheri. --Mwanaharakati (Longa) 16:25, 2 Februari 2009 (UTC)[jibu]

Mpendwa, bado kidogo kufikia 10,000 na kupanda chati katika wiki za lugha nyingine... Bahati mbaya, sina muda mwingi kukuungia mkono katika harakati zako. Halafu siku hizi napoteza muda kuboresha makala zilizopo kuliko kuanzisha mpya. Asante! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:45, 4 Februari 2009 (UTC)[jibu]

11,000

Riccardo Riccioni, salaaaaam! Wikipedia yetu imefikisha makala 11,000! Ni furaha iliyoje? Basi tu, niseme tujitahidi kuendeleza na kushauriana kwa kila jambo litakalosaidia Wikipedia yetu kuwa juu! Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 15:51, 9 Aprili 2009 (UTC)[jibu]

Tuzo ya Barnstar

Barnstar Hongera: Umepewa Tuzo ya Barnstar!

Kwa juhudi ya kazi zako hapa katika Wikipedia ya Kiswahili!--Mwanaharakati (Longa) 14:37, 27 Aprili 2009 (UTC)[jibu]

Ukifanyakazi kwa kiasi kikubwa katika Wikipedia, basi unastahili pongezi ya TUZO YA WIKI kila unapochangia zaidi! Ukifungua ukurasa huo, utaona maelezo marefu kuhusu BARNSTAR kwa lugha ya Kiitalia! Kila la kheri.--Mwanaharakati (Longa) 13:06, 30 Aprili 2009 (UTC)[jibu]

Jamii za Juu na Chini

Riccardo Riccioni, salam! Kuna tatizo nimeliona, kaka. Ukianzisha JAMII, unatakiwa pia uweke JAMII za chini. Kwa mfano: JAMII ya JUU

  • Jamii:Nyimbo za Tupac

JAMII ya CHINI

  • Jamii:Nyimbo msanii kwa msanii

Kifupi hakuna jamii bila mwenziwe. Na ikiwa hakuna uwezekano wa kupata mwenziwake, ni afadhali zisiumbwe! Bimaana, JAMII YA WANAMUZIKI WA TANZANIA, ipo chini ya WATU WA TANZANIA. Natumai ya kwamba utakuwa umenielewa namna jinsi nilivyoeleza. Kazi njema.--Mwanaharakati (Longa) 05:07, 4 Mei 2009 (UTC)[jibu]

Mwanaharakati awe bureaucrat

Nimemteua Mwanaharakati achaguliwe kuwa msimamizi mkuu pamoja nasi (b'crat). Naomba upige kura kwenye ukurasa wa wakabidhi. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 07:17, 28 Mei 2009 (UTC)[jibu]

Flowerparty awe mkabidhi

Nimemteua Flowerparty achaguliwe kuwa mkabidhi pamoja nasi. Naomba upige kura kwenye ukurasa wa Wakabidhi. Ahsante! --Mwanaharakati (Longa) 10:34, 9 Julai 2009 (UTC)[jibu]

Hongera ya makala 12,000

Riccardo, salam! Hongera kwa kusukuma Wikipedia yetu na kufikisha makala zaidi ya 12,000! Ninatumainia kuona michango yako mengine kibao kuliko hiyo uliyoifanya hapo awali!. Siku takii lolote lile, isikuwa kheri ya maisha. Wako kijana mtiifu, MuddybA.K.A.--Mwanaharakati (Longa) 13:02, 25 Julai 2009 (UTC)[jibu]

Riccardo, bila samahani kwani mjadala huu ni wetu wote! Kuhusu kungongeza mbegu: ni vyema pia kuongeza mbegu kwani hata ile Wikipedia ya Kiitalia ilipiga hatua kubwa kwa kufuatia mbegu zilizowekwa (niliyajua haya wakati ninaandika makala kuhusu matoleo ya Mawikipedia - ya Kiitalia umekuwa kubwa baada ya kujaza mbegu za miji na vitongoji vya Ufaransa). Hivyo tunakaribisha mbegu kedekede. Lete tu, kaka! Kuhusu picha: Pole kwa kusahau tena. Picha ukitaka ije hapa ni lazima uhakikisha kwamba hiyo picha ipo kwenye commons? Ikiwa ipo, basi suala lake ni dogo sana, kaka yangu. Ni kiasi cha kubadili tu kama umeitoa kutoka Wikipedia ya Kiitalia (jinsi ulivyoeleza "Immagine" badilia kuwa [[Picha:jina la faili.jpg/ siyo lazima iwe .jpg hata kama ipo .png, .svg, .gif na kadhalilika|thumb|righ/left/centre - vyovyote vile|ukubwa wa picha/mfano 250px|maelezo ya picha.]] Umeelewa?--06:31, 27 Julai 2009 (UTC)

Picha

Ndugu Riccardo, salaam! Narudi sasa hivi kutoka kwako nyumbani (ziara ad limina apostolorum..) naona swali lako kwenye ukurasa wa Muddy kuhusu picha. Kila picha iliyopo kwenye commons inaonekana ukibadilisha tu "immagine" kuwa ""picha" kwenye jina lake. Majina ya Kiingereza hupokelewa vile bila mabadiliko kama picha iko kwenye commons. Lakini picha nyingi ziko tu kwenye wikipedia ya lugha fulani. Hapa kua njia ifuatayo: a) unanakili picha kwa kompyuta yako (je hii unajua? rightclick - save image as - halafu uiweke mahali unapojua kwa mfano desktop) b) katika sw.wikipedia unapakia picha: bofya "pakia faili" kwenye orodha upande wa kushoto-chini, fuata maelezo kwenye fomu c) nashauri kufuta picha baadaye kwenye mashine yako kusudi usijaze nafasi iliyopo mno.

Wasalaam --Kipala (majadiliano) 09:30, 28 Julai 2009 (UTC)[jibu]

Ushauri uliokokotezwa. Ukipakia picha kutoka Wikipedia zingine usisahau kuiwekea mabano ya hatimili (license tag). Bimaana usipofanya hivyo, siku hizi tumepata mtu wa kushughulikia picha (Flowerparty) ninamashaka ataiondoa ikiwa haina maelezo yeyote ya hatimiliki! Pole kwa mengi tuliokueleza!--Muddyb MwanaharakatiLonga 13:19, 7 Agosti 2009 (UTC)[jibu]

13,000

Riccardo, salaam! Si umeona kwamba tumekuwa wa kwanza katika Afrika - na taarifa hizo ulinieleza hapo juzi. Leo hii tumefikia 13,000!!! Basi hongera na tuendelee kushauriana!--Muddyb MwanaharakatiLonga 08:03, 18 Agosti 2009 (UTC)[jibu]

defaultsort

Bila samahani. Machoni mwangu, 'Defaultsort' maana yake ni kuorodhesha kufuatana na alfabeti. Kwa hiyo naona, mtakatifu ambaye hana jina la familia, aorodheshwe chini ya jina lake la kwanza na siyo chini ya jina lake la mahali wala la baba. Tunaweza kuongeza ubini ila tusiuweke kwanza katika 'Defaultsort'. Au unasemaje? Kila la kheri, --Baba Tabita (majadiliano) 10:56, 3 Septemba 2009 (UTC)[jibu]

Riccardo, salam. Unaweza kuchungulia majadala huu mara moja?--Muddyb MwanaharakatiLonga 13:10, 4 Septemba 2009 (UTC)[jibu]
Labda ni mimi ambaye sijakuelewa vizuri. Ungalikuwa umeniorodheshea makala za watakatifu hao watatu ili niangalie mimi mwenyewe, ningalikuelewa haraka zaidi. Kwa vyovyote inaonekana kama tumeelewana hatimaye. Ila katika tamaduni zetu kuna tofauti kati ya jina la familia na jina la baba. Ndiyo maana, tukiangalia ubini, hatuelewi kitu kilekile. Hata hivyo, ni vizuri kumworodhesha mtu yeyote katika 'Defaultsort' kulingana na jina lake ambalo chini yake amejulikana vizuri zaidi - liwe jina binafsi au jina la familia (sijamkuta mtu anayejulikana chini ya ubini). Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 13:16, 4 Septemba 2009 (UTC)[jibu]
Ah - nimeanza kuelewa. Umebadilisha mfululizo wa majina ya watu fulani baada ya kubadilishwa nami. Ukiangalia k.m. Mtakatifu Alberto Hurtado, wikipedia nyingine, hata ya Kiitalia na ya Kiingereza, zinamworodhesha chini ya H, na siyo chini ya A. Tufuate mifano yao. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 13:42, 4 Septemba 2009 (UTC)[jibu]

Riccardo, salaam! Husika na kichwa cha habari hapo juu ni sanduku la kujumlishia habari za Watakatifu kama jinsi wanavyoweka katika Wikipedia zingine. Dhumuni la kuandika ujumbe huu ni kukutaka utoe msaada wako wa kutfasiri baadhi ya maeno yaliyomo kwenye kigezo hicho. Binafsi najua kuandika kaziliwa wapi/kufa na kadhalika. Mengine kama "feast" (ndani yake kuna maneno kama "calender of saints"). Si kazi kubwa saana. Lakini ningependa tufanye pamoja kwa sababu kazi hii inakuhusu sana wewe. Ni katika kutaka kuboresha makala zako zaidi, kaka yangu. Ukiwa tayari, basi nijulishe! Unaonaje?--Muddyb MwanaharakatiLonga 09:52, 5 Septemba 2009 (UTC)[jibu]

Riccardo, salaam! Pole kwa kuchelewa kukujibu! Muda mzuri ni ule wa saa nane au saa tisa. Lakini zaidi ni saa nane naona itakuwa poa zaidi. Ukiona saa nane tu - basi utaona nimebadilisha baadhi ya vitu na kuviorodhesha kwenye ukurasa wa majadiliano husika na kigezo hicho. Wasalaaam!--Muddyb MwanaharakatiLonga 05:59, 7 Septemba 2009 (UTC)[jibu]
Basi kwa sasa hivi unaweza?--Muddyb MwanaharakatiLonga 08:31, 7 Septemba 2009 (UTC)[jibu]
Riccardo: ukitazama yale majadiliano ya lile jedwani utaona mabadiliko kidogo. Je, unaweza kuendeleza zile sehemu zilizosalia?--Muddyb MwanaharakatiLonga 09:49, 7 Septemba 2009 (UTC)[jibu]

14,000

Riccardo, salaaaam! Ninapenda kukutaarifu kwamba Wikipedia yetu imefikisha zaidi ya makala 14,000! Ni matumaini yangu kwamba tutafika elfu 15,000? Mmmh, ni safari ndefu! Labda tu nitoe pongezi zako kwa kuendeleza zaidi makala za dini na jamii? Haikuwa kazi rahisi, lakini uliweza! Basi hongera kwa kuliwezesha na kila la kheri katika maisha! Ni mimi mdogo wako mtiifu.--Muddyb MwanaharakatiLonga 14:47, 11 Septemba 2009 (UTC)[jibu]

Riccardo, salam! Ahsante kwa kutupia jicho na kusahihisha makala ya Matengenezo ya Kiprotestanti. Halafu ingekuwa vizuri zaidi ukamalizia kuandika makala ya Matengenezo ya Ukatoliki. Niliiona makala ile kule kwenye Wikipedia ya Kiingereza Rahisi. Wameelezea kama jinsi ilivyo ile ya Uprotestanti. Je, ungependa kuanzisha makala hiyo? Ni mimi mdogo wako,Muddyb, au,--Muddyb MwanaharakatiLonga 08:28, 5 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Riccardo, kumradhi kwa kukitelekeza kigezo cha Mtakatifu. Nilijaribu kitu fulani lakini maarifa yangu yalisimama kimwendelezo. Si kitu. Ngoja nipitie tena ili nione wapi nilikwama hapo awali.--Muddyb MwanaharakatiLonga 08:40, 5 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Nimebadilisha mfumo wa jedwali la Kigezo:Walimu wa Kanisa‎. Hebu tazama na uniambie kama inafaa?--Muddyb MwanaharakatiLonga 09:57, 5 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

mradi wa Google kwa ajili ya wikipedia yetu

Bwana Riccardo, salaam!
Nimepata mawasiliano kutoka Christine Moon huko Palo Alto, California. Yeye anafanya kazi kwa shirika la Google, nao wameanza kupanga mradi au huduma kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Tanzania na Kenya ili waelimishwe kuandika makala kwa wikipedia ya Kiswahili. Kumbe!
Christine sasa ametualika kumwandikia maoni yetu, angalia tovuti hiyo:
http://docs.google.com/Doc?docid=0AbIPJ9Nv6udZZGd6MndwcGdfMzFkODNzOG0zYw&hl=en
Bahati mbaya yeye haelewi Kiswahili, kwa hiyo itakuwa lazima kumwandikia kwa Kiingereza. Ukihitaji msaada wangu upande wa kumwandikia, karibu unijulishe. Asante kwa michango yako!
Ni wako katika ujenzi wa lugha yetu, --Baba Tabita (majadiliano) 07:57, 10 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Kanisa la Armenia

Riccardo, salam. Kwanza nitoe shukrani zangu nyingi za dhati kwa msaada wako juu ya masawazisho ya makala zenye athira ya kidini. Nimeona maranyingi ukisawazisha (na hata kupanua makala hizo). Leo hii, nimeonelea angalao uandike makala moja au mbili za katika hicho kichwa husika hapo juu - kwa sababu niliona umeiweka sawa kwa kiasi kikubwa. Je, ungeweza angalao kuandika kitu kama labda: Kanisa la Kifalme la Armenia au lile la Katoliki? Yaani, dhumuni la kusema hivi ni kwa sababu kile kiungo au ile maana ya kutofautisha makala zile bila hata kuwepo ni sawasawa na bure! Nitakuwa mwenyekushukuru iwapo utanisaidia kwa hili. Zile makala zingekuwa za kawaida, kwa mfano muziki au filamu, basi ningeendelea mwenyewe. Lakini masuala ya kidini, aah, sijui kitu kwa kweli. Ni hayo tu. Wako,--Muddyb MwanaharakatiLonga 10:55, 13 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Riccardo, salaam! Haya, kwanza ahsante kwa kuanzisha makala zile za kidini kama jinsi nilivyoomba hapo juu. Pili, nimeona maranyingi ukiandika "waamini" badala ya "waumini." Sasa hapa sijajua kama ni Kiswahili kipya? Maana, nimezoea kuona wakiandika waumini na si "waamini". Je, hiyo ni sawa?--Muddyb MwanaharakatiLonga 12:55, 19 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Muddyb mpendwa, nimefikiria swali lako. Sina hakika, lakini naona neno waumini linamaanisha wafuasi wa dini fulani, wakati waamini linasisitiza zaidi kuwa ndio wanaoamini ufunuo fulani, tofauti na wasiouamini. Ningesema waumini ni neutral zaidi. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:25, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

majadiliano kuhusu utafsiri wa istilahi

Bwana Riccardo, salaam! Nimeanzisha majadiliano mapya kuhusu utafsiri wa istilahi ya wikipedia yetu hapa. Naomba uyaangalie na kuchangia maoni yako. Asante! --Baba Tabita (majadiliano) 09:54, 23 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]

Salaam Riccardo, nimesoma na kukubali hoja lako kuhusu aina na kundi/jamii. Umenishtusha kidogo ktika mfano mmoja uliyotoa kuhusu maharagwa na nafaka. Niliandika makala za maharagwe, jamii kunde na nafaka; kwangu kunde na nafaka ni makundi mawili tofauti. Sina neno ukipumzisha watakatifu kidogo na kuingia kwenye mboga. Ila tu nashukuru kwa maelezo ya ndani aidi --Kipala (majadiliano) 04:08, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Ndugu, usihangaike. Biolojia yangu iliishia darasa la kumi tu. Ukiona maharagwe si nafaka,inawezekana nimekosea kutoa mfano. Afadhali nisijaribu kugusa kurasa za mambo nisiyoyajua. Tena watakatifu na mambo ya dini wananivutia zaidi... SHALOM! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:20, 26 Oktoba 2009 (UTC)[jibu]
Baada ya muda mrefu narudia suala hilo kwa kusema nimesoma kamusi ya Kiswahili Sanifu: inasema haragwe ni nafaka... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 04:46, 19 Septemba 2010 (UTC)[jibu]

Uchaguzi Mpya

Salam, Riccardo. Unaombwa upige kura katika ukurasa wa wakabidhi wa Wikipedia. Mmoja kati ya wachangiaji wenzetu (Mr Accountable) amejiteua kuwa mkabidhi! Ili kumpgia kura, tafadhali fungua hapa. Ahsante sana.--Muddyb MwanaharakatiLonga 18:39, 28 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Salam, Riccardo! Ahsante kwa masahihisho na ongezeko lako la kwenye makala ya Baptisti. Kwa kweli makala imekaa vyema kabisa. Tatizo langu lipo palepale - sijui mengi kuhusu dini. Ikiwa tunapata msaada kama huo, basi mambo yatakuwa mazuri.--MwanaharakatiLonga 16:33, 5 Machi 2010 (UTC) [jibu]

Eeeh, kweli. Lakini kwa bahati mbaya tafsiri ile sijaitunga miye! Nilisoma kutoka katika kamusi ya TUKI niliyonayo kwenye kompyuta yangu. Ili sema Baptist - SW = Baptisti. Lakini bila kutafakari juu ya uitaji wa wanadini jinsi wafanyavyo, basi ikawa imetokea. Ahsante sana na ni tumaini kila niandikapo makala za dini, basi utawasawazisha!--MwanaharakatiLonga 11:35, 6 Machi 2010 (UTC)[jibu]
Afadhali ulivyoliona hilo! Binafsi nilijaribu, lakini hali yangu haikuwa vyema tena - nikaona bora kutumia muda huo kuanzisha makala mapya kuliko kuendelea na zile. Labda tutarekebisha! Kuhusu Kipala, sifahamu kwa sababu ni muda sasa hatujazungumza kuhusu mahali alipo. Ninatumai yupo kulekule Iran! Ila tu kazi zimembana!!! Salam teeele kutoka mjini Dar es Salaam, Tanzania. Wako,--MwanaharakatiLonga 07:16, 8 Machi 2010 (UTC)[jibu]

Kanisa la Scientology

Salam, Riccardo! Unaweza kunieleza au hata kuandika makala kuhusu kichwa cha bari hapo juu? Ningependa kujua ni dhehebu la namna gani. Wako katika ujenzi wa Wikipedia yetu,--MwanaharakatiLonga 06:54, 19 Machi 2010 (UTC) [jibu]

Salaaam! Ahsante kwa itikio lako la vitendo!!! Ni tumaini lako kwamba nimefurahi, basi kweli nimefurahi!!! Shukrani tena. Wako,--MwanaharakatiLonga 13:43, 23 Machi 2010 (UTC)[jibu]

Hongera ya makala 18,000

Salam, Riccardo Riccioni! Hongera ya makala 18,000! Kumbe tumefika - japokuwa kuna mengi ya kusahihisha na kufuta pia. Lakini si mbaya tukipongezana! Tuendeleeni jamani.--MwanaharakatiLonga 09:13, 31 Mei 2010 (UTC) [jibu]

Wafiadini wa Uganda

Naona kama makala hii inataka kujadili habari za "Wafiadini wa Uganda" ipanushwe kidogo kulingana na pande zote zilizohusika yaani Wakatoliki na Waanglikana. Sasa inaonekana kama habari ya upande mmoja tu inayotaja upande mwingine kandokando. Sawa nikiongeza? Kipala (majadiliano) 11:06, 13 Juni 2010 (UTC)[jibu]


Questionnaire

Nadhani labda wewe umepata pia maswali yale ya Rachel - hapa majibu yangu: Mtumiaji:Kipala/questionnaire - Kipala (majadiliano) 19:08, 30 Juni 2010 (UTC)[jibu]


Kura ya kuamua juu ya wakabidhi waliopotea

Karibu kutembelea ukurasa wa wakabidhi na kuamua juu ya wenzetu waliopewa haki za wakabidhi lakini hawakuonekana tangu miezi mingi: Wikipedia:Wakabidhi#Kura_ya_kuondoa_wakabidhi_waliopotea. Tuliwahi kujadili swali hili mwaka uliopita (tazama kwenye ukurasa unaotajwa, juu ya pendekezo) ; sasa njia imeonekana. Kipala (majadiliano) 05:27, 1 Oktoba 2010 (UTC)[jibu]

Salamu na viungo vya mwili

Riccardo, salaam, nafurahia jinsi unavyochungulia makala nilipoandika na kuboresha Kiswahili na tahajia. Sana nina ombi. Nliwahi kuanzisha makala juu ya viungo vya mwili na hao vijana wa mashindano ya makala za afya waliendelea. Makala hizi zote zinahitaji kuangaliwa kwa sababu Wakenya (nadhani) waliunda sentensi za ajabu kidogo na pia mara nyingi walikosa viungo. Nikiingia hapa nakiri udhaifu: kwa Wasafwa na Wanyakyusa nilipojifunza Kiswahili na baadaye Nairobi sijasikia kitu kingine ila "mkono" na "mguu". Kumbe. Sasa nimetengeneza picha ya mkono nikilenga ktaja sehemu zake kuanzia bega kupitia kisugidi hadi kiganja. Lakini ninahisi ya kwamba sina uhakika kwa sababu sina uzoefu kutaja sehemu zile (yooote mkono!) na kamusi zangu si wazi sana; mara nyingi maelezo si kamili, yanaingiliana maana au kuna maneno kadhaa na mimi sijui lipi ni afadhali. Je unajua wewe majina haya au unaweza kuchungulia kidogo? Tuanze kumaliza mkono baadaye inafuata mguu na mengine! Namwuliza pia Muddy ni vema kusikia jinsi wanavyosema Dar. Asante ndimi wako Kipala (majadiliano) 08:38, 10 Aprili 2011 (UTC)[jibu]

Asante kwa maneno yako ya kunitia moyo. Kuhusu viungo vya mwili mimi pia nina shida kuelezea sehemu mbalimbali, labda hata kwa Kiitalia! Sidhani nitaweza kukusaidia. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:03, 11 Aprili 2011 (UTC)[jibu]

Bunda vijijini

Je kuna wilaya ya Bunda vijijini?? Kama iko naomba habari na marejeo kwa ajili ya makla za wilaya / Mkoa wa Mara. Kama la, makala ya Jimbo Katoliki la Musoma isahihishwe. Kipala (majadiliano) 11:05, 22 Januari 2012 (UTC)[jibu]

Sidhani... ni haraka tu ya kuandika! Samahani! --41.221.34.70 08:04, 25 Januari 2012 (UTC)[jibu]
Pamoja na hayo, hatujaingiza mikoa (k. mf. Njome, Simiu) na wilaya mpya za Tanzania (k. mf. Gairo, Nyasa). --41.221.34.70 08:10, 25 Januari 2012 (UTC)[jibu]
Asante kwa jibu. Kuhusu mikoa na wilaya mpya - niko mbali. Unaweza kuanzisha makala ?Kipala (majadiliano) 13:08, 25 Januari 2012 (UTC)[jibu]
Sina DATA za kutosha. --41.221.34.70 14:26, 28 Januari 2012 (UTC)[jibu]