Magharibi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|250px|right|Alama za dira zikionyesha magharibi katika hali ya mkoozo (W = "West" = magharibi) '''Magharibi''' ni moja kati y...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:07, 8 Januari 2012

Alama za dira zikionyesha magharibi katika hali ya mkoozo (W = "West" = magharibi)

Magharibi ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande wa machweo ya jua.

Magahribi ni pia neno la kutaja saa ya sala ya jioni ya Waislamu na sala hii yenyewe.

Jina "magharibi" limetokana na neno la Kiarabu مَغْرِب maghrib linalomaanisha sehemu upande wa machweo.

Tanzania iko upande mwa kusini ya Kenya, na nchi za Malawi na Msumbiji ziko upande mwa kusini ya Tanzania.

Kwa maana ya kiutamaduni kuna uzoefu kutaja utamaduni wa Ulaya pamoja na Marekani (ambayo ni mtoto wa utamaduni wa Ulaya) kama "magharibi", kinyume chake ni "mashariki" kwa maana ya Asia.

Wakati wa vita baridi magharibi ilikuwa kifupi cha nchi za kibepari zilizofuata mtindo wa demokrasia kinyume na mashariki iliyomaanisha nchi za kikomunisti.

Tazama pia


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.