Nasaba ya Qing : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: hy:Ցին դինաստիա
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: hi:चिंग राजवंश
Mstari 62: Mstari 62:
[[hak:Chhîn-chhèu]]
[[hak:Chhîn-chhèu]]
[[he:שושלת צ'ינג]]
[[he:שושלת צ'ינג]]
[[hi:चिंग राजवंश]]
[[hif:Qing Dynasty]]
[[hif:Qing Dynasty]]
[[hr:Dinastija Qing]]
[[hr:Dinastija Qing]]

Pitio la 03:59, 1 Januari 2012

Bendera ya nasaba ya Qing (1890–1912)
Eneo la China chini ya nasaba ya Qing mnamo 1820

Nasaba ya Qing (Kichina: 清朝; pinyin: Qīng cháo) ilitawala China kati ya 1644 na 1912.

Watawala wa Qing walichukua nafasi ya makaisari wa nasaba ya Ming. Familia ya Qing ilitoka Manchuria na kwa sababu hii huitwa pia "Nasaba ya Manchu".

Chanzo cha watawala kutoka Manchuria

Mnamo 1580 BK Mmanchuria Nurhaci alikuwa jenerali wa kitengo cha kaskazini cha jeshi la nasaba ya Ming. Nurhaci aliunganisha makabila ya Wamanchuria na tangu 1616 akajiita Khan wa Manchuria yote.

Kuanzia 1644 jeshi la Wamanchuria lilianza kuvamia sehemu kubwa za China ya kaskazini na kupindua nasaba ya Ming.

Walihamisha mjiu mkuu wao kwenda Beijing.

Maendelo ya kipindi cha Qing

Karne za utawala wa Qing zilileta maendeleo makubwa katika uchumi na idadi ya wakazi wa China iliongezeka kutoka watu milioni 143 mnamo 1740 hadi watu milioni 430 mnamo 1850. Serikali ilisimamia karahana za mafundi waliotenegeneza bidhaa nyingi zilizopelekwa hadi Ulaya na Marekani. China ilikuwa na mapatao makubwa ya dhahabu kutoka Ulaya kutokana na biashara hii. Kati ya bidhaa zilizotafutwa Ulaya zilikuwa hasa vyombo vya kauri, fanicha na kazi za sanaa.

Ugomvi na Uingereza na vita ya afyuni

Kuanzia miaka ya 1820 Waingereza waliongeza biashara ya afyuni katika China. Majaribio ya serikali ya Qing kusimamisha biashara ya dawa hili la kulevya likasababisha vita ya afyuni ya kwanza (1839 bis 1842) ambako manowari za Uingereza zilishinda wanajeshi wa maji Wachina na kuteka niji muhimu kwenye pwani. Chini ilipaswa kukubali amani iliyoruhusu biashara ya afyuni na kuondoa masharti mengine kuhusu biashara ya nje.

Kwa njia hii China ya Waqing haikuwa tena nchi huru lakini ilipaswa kuwapa wageni kutoka Ulaya nafasi kubwa na kubwa zaidi katika biashara na uchumi. Pamoja na hayo mataifa ya Ulaya yalitwaa miji kama Hongkong kama vituo vyao vya kibiashara na kijeshi.

Mwisho wa Qing na ufalme katika China

Mwisho wa karne ya 19 vikundi mbalimbali ndani ya nasaba ya Qing walianza kuvutana juu ya matengenezo ya utaratibu wa kijamii na kisiasa. Malkia Cixi alizuia mabadiliko haya. Hadi kifo chake mwaka 1908 alitawala China iliyoendelea kushuka katika hali ya nusukoloni ya nchi za Ulaya. Kabla kifo chake alimteua mtoto Pu Yi kama kaisari mpya lakini utawala wa Qing ilipinduliwa katika mapinduzi ya China ya 1911 iliyomaliza nasaba ya Qing pamoja na ufalme katika China. Pu Yi alilazimishwa kuachana na cheo cha Kaisari mwaka 1912.

1934 hadi 1945 Japani ilimteua kama mtawala wa Manchuria iliyokuwa nchi kwa jina tu chini ya usimamizi wa Japani.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nasaba ya Qing kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA