Mambo Huangamia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Badiliko: fr:Le monde s'effondre
No edit summary
Mstari 2: Mstari 2:


==Mkondo wa hadithi==
==Mkondo wa hadithi==
Mhusika mkuu anaitwa [[Okonkwo]], mtajiri katika kijiji cha [[Umuofia]]. Huyo Okonkwo hufuata mila na desturi za Kiigbo vizuri sana ili kumshinda babake ambaye ni mduni. Anavyofuata hizo mila ikambidi hata kumuua mwana wake wa kambo na wanakijiji wakakubali. Siku moja lakini Okonkwo kwa bahati mbaya alimuua mwanakijiji mwingine na sasa akahukumiwa kuondoka kijijini kwake kwa miaka saba zinavyoamuru mila za kijiji. Uhamishoni Okonkwo anawakuta wamisionari Wazungu, akasikitika sana kugundua mwana wake mwenyewe aliacha mila za Kiigbo na kukubali dini ya [[Ukristo]]. Okonkwo akirudi kijijini baadaye akakuta hata maisha ya kijijini yameathiriwa na hiyo dini mpya. Anaanza kuupigia vita Ukristo, hatimaye lakini aliona kuwa haiwezekani kurudi kwa maisha ya kimila akajiua kwa kujinyonga.
Mhusika mkuu anaitwa [[Okonkwo]], tajiri katika kijiji cha [[Umuofia]]. Huyo Okonkwo hufuata mila na desturi za Kiigbo vizuri sana ili kumshinda babake ambaye ni mduni. Katika kufuata hizo mila alifika hatua ya kumuua mwana wake wa kambo na wanakijiji wakakubali. Siku moja lakini Okonkwo kwa bahati mbaya alimuua mwanakijiji mwingine na sasa akahukumiwa kuondoka kijijini kwake kwa miaka saba zinavyoamuru mila za kijiji. Huko uhamishoni Okonkwo alikutana na [[wamisionari]] Wazungu, akasikitika sana kugundua mwana wake mwenyewe aliacha mila za Kiigbo na kukubali dini ya [[Ukristo]]. Okonkwo akirudi kijijini baadaye akakuta hata maisha ya kijijini yameathiriwa na hiyo dini mpya. Akaanza kuupigia vita Ukristo, hatimaye lakini aliona kuwa haiwezekani kurudi kwa maisha ya kimila akajiua kwa kujinyonga.


==Marejeo==
==Marejeo==

Pitio la 17:11, 19 Desemba 2011

Mambo Huangamia (kwa Kiingereza "Things Fall Apart") ni riwaya iliyoandikwa na Chinua Achebe. Ilitolewa mwaka wa 1958. Hadithi ya riwaya hii imefuatiwa na Hakuna Starehe Tena (1960) na Mshale wa Mungu (1964).

Mkondo wa hadithi

Mhusika mkuu anaitwa Okonkwo, tajiri katika kijiji cha Umuofia. Huyo Okonkwo hufuata mila na desturi za Kiigbo vizuri sana ili kumshinda babake ambaye ni mduni. Katika kufuata hizo mila alifika hatua ya kumuua mwana wake wa kambo na wanakijiji wakakubali. Siku moja lakini Okonkwo kwa bahati mbaya alimuua mwanakijiji mwingine na sasa akahukumiwa kuondoka kijijini kwake kwa miaka saba zinavyoamuru mila za kijiji. Huko uhamishoni Okonkwo alikutana na wamisionari Wazungu, akasikitika sana kugundua mwana wake mwenyewe aliacha mila za Kiigbo na kukubali dini ya Ukristo. Okonkwo akirudi kijijini baadaye akakuta hata maisha ya kijijini yameathiriwa na hiyo dini mpya. Akaanza kuupigia vita Ukristo, hatimaye lakini aliona kuwa haiwezekani kurudi kwa maisha ya kimila akajiua kwa kujinyonga.

Marejeo

  • (de) "Kindlers Literaturlexikon" (1970), diwani ya 10, Zürich: Kindler, uk.9345
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mambo Huangamia kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.