Moto : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: tn:Molelo
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: cv:Çулăм
Mstari 58: Mstari 58:
[[cr:Ishkuteu]]
[[cr:Ishkuteu]]
[[cs:Oheň]]
[[cs:Oheň]]
[[cv:Çулăм]]
[[cy:Tân]]
[[cy:Tân]]
[[da:Ild]]
[[da:Ild]]

Pitio la 16:10, 18 Desemba 2011

Moto kubwa
Tetrahedron ya moto inaonyesha masharti manne yanayohitajika kwa moto kuwaka
Kiberiti kinawaka


Moto ni hali ya kuchoma haraka kwa gimba na kutoa joto pamoja na nuru. Kisayansi ni mmenyuko wa kikemia kati ya oksijeni ya hewani na kampaundi za kaboni. Moto ni mfano mkuu wa harakati ya kuoksidisha.

Katika historia ya ubinadamu matumizi ya moto yalikuwa hatua kubwa ya kujenga utamaduni. Watu hutumia moto kwa kupika, kujilinda dhidi ya baridi na giza, kupeana habari, kuendesha vyombo vya usafiri na kutengeneza umeme.

Moto ni pia kiharibifu ina hatari kwa mali, afya na maisha ya watu na viumbe vyote.

Moto kikemia

Moto inawaka kama masharti manne yako mahali pamoja:

  • gimba lenye uwezo wa kuwaka, kwa kawaida lenye kiasi cha kampaundi za kaboni na hidrojeni
  • oksijeni ya kutosha (au: kampaundi za oksijeni)
  • chanzo cha joto ya kutosha kwa kuwasha mchanganyiko wa fueli na oksijeni
  • mmenyuko mfululizo unaoendeleza hali ya kuwaka kwa moto

Masharti haya manne huelezwa kwa tetrahedroni ya moto. Hakuna moto kama masharti haya manne hayapo pamoja.

Mmwnyuko mfululizo ni lazima kwa kuendelea kwa moto ukihkikisha ya kwamba kuna joto la kutosha kuendeleza moto.

Moto inazimika kama moja kati ya masharti manne linaondolewa. Katika mfamo wa moto ya gesi kwenye jiko la kupikia ya gesi moto huu unazimika kwa:

  • kuzima gesi ambayo inaodoa chanzo cha fueli
  • kufunika moto kabisa maana hii inazuia oksijeni kufika motoni; baada ya muda mfupi akiba ya oksijeni iliyo karibu na moto imekwisha na moto inazimika
  • kumwaga maji juu ya moto; hii inapunguza joto motoni haraka sana na harakati ya kuwaka inakwama; kupuliza sana inaweza kuleta tokeo lilelile kwa kuondoa joto kutoka kwa gesi inayoendelea kutoka
  • kuingiza kemikali kama halon motoni inayochelewesha mmenyuko ndani ya moto kiasi cha kusimamisha mmenyuko mfululizo.

Moto na utamaduni

Matumizi asilia ya moto

Wataalamu wanaamini ya kwamba watu wa kale sana waliona faida ya kutumia moto uliotokea kiasili kutokana na radi n.k.. Walipokuta wanyama waliokufa katika moto ya aina hii waliona ya kwamba nyama iliyochomwa na moto ni lishe bora kuliko nyama bichi. Walitambua pia ya kwamba mimea au sehemu za mimea zilikuwa chakula bora baada ya kukaa motoni kwa muda fulani.

Kwa hiyo inaaminiwa hao watu wa kwanza walijifunze kubeba moto asilia na kuitunza kwenye makazi yao. Baadaye watu walijifunza kuwasha moto. Kuwa na moto karibu na makazi au mahali pa kulala kulikuwa namna ya ulinzi dhidi ya wanyama wakali wanaoogopa moto na hawana akili ya kubainisha matumizi yake. Moto ilisaidia pia wakati wa kuvinda.