Kitabu cha Yeremia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Ondoa: de:Buch Jeremia (deleted)
d Bot: Simplifying links ([link|linktext] → [link]text)
Mstari 1: Mstari 1:
Kitabu cha [[Yeremia]] ni kimojawapo kati ya [[vitabu vya kinabii]] vilivyo virefu zaidi katika [[Tanakh]] ([[Biblia ya Kiebania]]), na kwa hiyo pia katika [[Agano la Kale]] ambalo ni sehemu ya kwanza ya [[Biblia ya Kikristo]].
Kitabu cha [[Yeremia]] ni kimojawapo kati ya [[vitabu vya kinabii]] vilivyo virefu zaidi katika [[Tanakh]] ([[Biblia ya Kiebania]]), na kwa hiyo pia katika [[Agano la Kale]] ambalo ni sehemu ya kwanza ya [[Biblia ya Kikristo]].


Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[Historia ya Wokovu|historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya [[Ufunuo|ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya [[ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].


==Mhusika mkuu==
==Mhusika mkuu==

Pitio la 14:35, 1 Desemba 2011

Kitabu cha Yeremia ni kimojawapo kati ya vitabu vya kinabii vilivyo virefu zaidi katika Tanakh (Biblia ya Kiebania), na kwa hiyo pia katika Agano la Kale ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mhusika mkuu

Yeremia, mtu mpole sana, aliitwa na Mungu akiwa bado kijana, akapewa kazi ngumu ya kutabiri maangamizi ya Yerusalemu viongozi wasipoacha siasa yao ili kumtegemea Mungu tu.

Habari zake zinapatikana hasa katika kitabu hiki, ingawa humo hazikupangwa kitarehe.

Wito na muda wa unabii wake

Toka mwanzo Yeremia alitaka kukataa wito wa unabii, na hata baadaye akafikia hatua ya kukata tamaa alipodhulumiwa. Lakini Mungu alimuita kwa mpango wa milele, Yeremia asiweze kukataa (15:10-21; 20:7-18).

Katika muda wa utume wake (626-585 hivi K.K.) kipindi kizuri ni kile tu ambacho mfalme Yosia alifanya urekebisho (622-609 K.K.).

Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha Nahumu (612 hivi K.K.).

Lakini kisha kufa Yosia mambo yakaharibika haraka sana, ikambidi Yeremia awakaripie wafalme na wananchi wasifanye dini kisingizio cha kuendelea na maovu badala ya kutubu (7:1-15; 19:1-13).

Aliwakaripia vilevile manabii wa uongo waliotumainisha watu bure (20:1-6).

Ndipo alipoanza kupigwa, kufungwa na kuhukumiwa, akawa mfano wa Yesu, yeye ambaye peke yake katika Agano la Kale aliishi bila ya ndoa kwa agizo la Mungu; lakini hakuuawa (26:1-19).

Kwa hofu akajificha, ila hakuacha kutabiri maangamizi kwa maandishi kwa njia ya karani wake Baruku (36).

Basi, mfalme Nabukadreza wa Babeli akazidi kuwa na nguvu: mwaka 602 K.K. akamtiisha mfalme Yehoyakimu wa Yuda, na mwaka 598 K.K. akazingira Yerusalemu na kuwahamishia Babeli mfalme Yekonia na viongozi wengi.

Hapo Yeremia akawaandikia wasikate tamaa ila wasitarajie kurudi upesi kwa kuwa watabaki uhamishoni miaka 70 (29:4-23).

Lakini katika mpango wa Mungu hao ndio wa kutegemewa, sio walioachwa Yerusalemu (24).

Nabukadreza alipohusuru mji huo mara ya pili, mfalme na viongozi wengine walikataa shauri la Yeremia la kusalimu amri, wakamfunga pabaya sana mpaka siku ya Yerusalemu kutekwa (37-38).

Kwa kawaida Yeremia alitabiri kinyume cha matazamio madanganyifu ya watu, lakini walipokata tamaa akawatuliza na kutabiri heri.

Kilele cha mafundisho yake ni kwamba Mungu atafunga na Israeli yote Agano Jipya ambalo litaandikwa mioyoni (31:31-34).

Mwisho wa unabii wake

Baada ya Yerusalemu kuteketezwa (587 K.K.) Yeremia alichagua kubaki nchini pamoja na mafukara badala ya kuhamia Babeli (39:8-40:6), ila ukatokea uasi akalazimishwa na Waisraeli wenzake kuwafuata Misri: huko akawaonya wasifuate Upagani lakini wakakataa tena kumsikiliza (42-44).

Nyongeza

Kama nyongeza ya kitabu cha Yeremia tuna Maombolezo matano juu ya Yerusalemu ulioteketezwa, ambamo inaonekana toba halisi baada ya tukio hilo. Hatujui yametungwa na nani.

Viungo vya nje

Kitabu cha Yeremia katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.