Aral (ziwa) : Tofauti kati ya masahihisho
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: hsb:Aralski jězor |
d Robot: no:Aralsjøen is a featured article |
||
Mstari 25: | Mstari 25: | ||
{{Link FA|lmo}} |
{{Link FA|lmo}} |
||
{{Link FA|nl}} |
{{Link FA|nl}} |
||
{{Link FA|no}} |
|||
[[ar:بحر آرال]] |
[[ar:بحر آرال]] |
Pitio la 03:40, 28 Novemba 2011
Ziwa la Aral (Kikazakhi: Арал Теңізі (aral tengizi), Kiuzbeki Orol dengizi, Kirusi Аральскοе мοре aralskoye more) ni ziwa la Asia ya Kati linalopakana na Kazakhstan na Uzbekistan. Hadi mwaka 1960 lilikuwa na eneo la maji la 68,000 km² lakini limepungua hadi kubaki na 17,160 km² pekee mwaka 2004. Tangu 1987 kupungua kwa maji kulisababisha ugawaji wa ziwa katika sehemu mbili upande wa kazkazini na upande wa kusini ambazo haziungana tena.
Mito mikubwa inayoingia na kubeba maji yake ni Amu Darya na Syr Darya na mito hii ilitumiwa katika mipango ya Umoja wa Kisovyeti kwa umwagiliaji wa mashamba makubwa ya pamba na mazao mengine. Miradi hii iliyoanzishwa katika mazingira yabisi iliendelea kwa miaka 30 hivi hadi kushindikana; maji yamepotea kwa wingi mashambani na katika mifereji kutokana na usimbishaji na kusababisha kupunguza kwa mazao. Kiasi cha chumvi ardhini kiliongezeka sana jinsi ilivyo mara nyingi katika miradi ya umwagiliaji ya nchi za joto na kumaliza rutba ya udongo.
Ziwa halikupokea tena kiasi chake cha maji likapungua. Sehemu kubwa za eneo la ziwa la awali zimekuwa jangwa. Maji yaliyobaki yameharibika kutokana na maji sumu ya viwanda na mbolea nyingi iliyosukumwa kutoka mashamba mitoni halafu ziwani.
Kuna mradi wa kuokoa angalau sehemu ndogo ya kaskazini. Ukuta ulijengwa kwa shabaha ya kuzuia upotevu wa maji katika jangwa la msingi wa ziwa la kale. Uwiano wa maji yamepanda tena katika sehemu hii ndogo.
-
Ziwa Aral mnamo 1850
-
Ramani ya Ziwa Aral mnamo 1960
-
Ziwa Aral 1985.
-
Kisiwa ndani ya ziwani liliunganishwa na bara kutokana na upotevu wa maji manmo 2000/2001
-
Sehemu ya Kaskazini imeanza kupanua kidogo
-
Picha ya Ziwa Aral inaonyesha eneo lake jinsi ilivyoonekana mwaka 2004 pamoja na mipaka ya ziwa mnamo 1960 (mstari mweusi)
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Aral (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |