Ali Hassan Mwinyi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: ru:Мвиньи, Али Хасан
Mstari 35: Mstari 35:
[[no:Ali Hassan Mwinyi]]
[[no:Ali Hassan Mwinyi]]
[[pl:Ali Hassan Mwinyi]]
[[pl:Ali Hassan Mwinyi]]
[[ru:Мвиньи, Али Хасан]]
[[rw:Ali Hassan Mwinyi]]
[[rw:Ali Hassan Mwinyi]]
[[yo:Ali Hassan Mwinyi]]
[[yo:Ali Hassan Mwinyi]]

Pitio la 18:54, 7 Oktoba 2011

Ali Hassan Mwinyi (amezaliwa 8 Mei, 1925) alikuwa Rais wa Pili wa Tanzania kuanzia 1985 hadi 1995. Aliyemtangulia ni Mwalimu Julius Nyerere, na aliyemfuata ni Benjamin Mkapa. Kabla hajachaguliwa kuwa Rais, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu Rais. Pia alikuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia 1990 hadi 1996.

Mwinyi alizaliwa kwenye kisiwa cha Unguja (Zanzibar).

Wakati wa urais wa Mwinyi, sera za Ujamaa zilianza kugeuzwa. Badala yake sera za soko huru zilianzishwa, masharti ya kuingiza bidhaa kutoka nchi za nje yalipunguzwa na uanzishaji wa biashara ya watu binafsi ulihamasishwa. Mwaka wa 1991, uanzishaji wa vyama vingi uliruhusiwa.

Sera za soko huru za Mwinyi zimeendelezwa chini ya Rais Benjamin Mkapa. Mwinyi mwenyewe, baada ya kustaafu, hakujiingiza katika mambo ya siasa tena. Anaendelea kuishi huko Dar es Salaam.

Alitanguliwa na
Mwinyi Aboud Jumbe
Makamu wa Rais wa Tanzania
1984-1985
Akafuatiwa na
Joseph Sinde Warioba
Alitanguliwa na
Julius Nyerere
Rais wa Tanzania
1985-1995
Akafuatiwa na
Benjamin Mkapa