Abuja : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Ondoa: nap:Abuja (deleted)
d r2.5.1) (roboti Nyongeza: az:Abuca
Mstari 39: Mstari 39:
[[am:አቡጃ]]
[[am:አቡጃ]]
[[ar:أبوجا]]
[[ar:أبوجا]]
[[az:Abuca]]
[[bat-smg:Abodža]]
[[bat-smg:Abodža]]
[[be:Горад Абуджа]]
[[be:Горад Абуджа]]

Pitio la 11:47, 26 Septemba 2011


Jiji la Abuja
Nchi Nigeria
Mahali pa Abuja kule Nigeria
Mahali pa Abuja kule Nigeria

Abuja ni mji mkuu wa Nigeria. Idadi ya wakazi wake imekadiriwa kuwa watu 178,462 [1]. Mwaka wa 1976, serikali ya Nigeria iliamua kuanzisha mji mkuu mpya badala ya Lagos. Wakachagua katikati ya nchi, na mipango ya ujenzi ikaundwa chini ya makampuni matatu ya Marekani: PRC Corporation; Wallace, McHarg, Roberts na Todd; na Archisystems. Mipango hiyo ikabadilishwa baadaye na Kenzo Tange, msanifu majengo maarufu wa Japani. Abuja ikatangazwa rasmi kuwa mji mkuu wa Nigeria tarehe 12 Desemba 1991. Iko mahali pa 9, 10, Kaskazini na 7, 10, Mashariki. [2]

Balozi za nchi nyingi zikahamishwa Abuja kutoka Lagos.

Historia

Sifa muhimu ya Abuja ni Mlima wa Aso ambao ni mwamba ulio na urefu wa mita 400. Upande wa kusini wa mlima huo, kuna Ikulu ya Rais, Bunge la Nigeria, Mahakama Kuu na sehemu nyingi za mji.

Majengo maarufu mengine ni Msikiti wa Taifa (Nigerian National Mosque) na Kanisa Kuu la Madhehebu (National Ecumenical Centre Cathedral). Kuna kiwanja cha ndege cha kimataifa (Nnamdi Azikiwe International Airport), karibu na Mlima wa Zuma. Sehemu nyingine za mji hazijajengwa ilivyopangwa, na majengo mengi yanaendelea kujengwa.

Mji wa Abuja unagombea kuwa mahali pa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa mwaka wa 2014 (2014 Commonwealth Games).

Marejeo ya nje