Abidjan : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Ondoa: nap:Abidjan (deleted)
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: hy:Աբիջան
Mstari 76: Mstari 76:
[[hr:Abidjan]]
[[hr:Abidjan]]
[[hu:Abidjan]]
[[hu:Abidjan]]
[[hy:Աբիջան]]
[[id:Abidjan]]
[[id:Abidjan]]
[[io:Abidjan]]
[[io:Abidjan]]

Pitio la 16:07, 10 Septemba 2011


Jiji la Abidjan
Nchi Cote d'Ivoire
Mkoa Lagunes
Wilaya Abidjan
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 3,624,800
Tovuti:  www.district.abidjan.org
Eneo la Plateau na wangwa wakati wa usiku

Abidjan ni mji mkubwa nchini Cote d'Ivoire pia ni mji mkuu hali halisi. Vilevile ni bandari kuu ya nchi kwenye Ghuba ya Guinea ya bahari ya Atlantiki. Abidjan haiko baharini moja kwa moja lakini kwenye wangwa ya Ebrie inayotengwa na bahari kwa kanda nyembamba ya mchanga.

Abidjan imekua haraka kuanzia wakazi 65,000 mwaka 1950 hadi wakazi 3,624,800 mwaka 2000.[1] Ilikuwa pia mji mkuu rasmi kati ya 1934 hadi 1983.

Kuna viwanda vya ngozi, nguo, vyakula na mafuta.

Abidjan ilikuwa kijiji tu hadi mwaka 1904. Wakati ule iliteuliwa kuwa mwanzo wa reli ya kuelekea ndani. Reli ilianzishwa hapa kwa sababu ng'ambo ya wangwa ilikuwepo bandari ndogo ya Port-Bouët. Tangu reli kujengwa Abidjan ilikua haraka. Mwaka 1934 ilitangazwa kuwa mji mkuu wa koloni ya Kifaransa Cote d'Ivoire.

Mwaka 1950 mfereji wa Vridi ilikata kanda la mchanga na kufungua wangwa kwa meli kutoka bahari; wangwa ikawa bandari kubwa yenye usalama mzuri kwa meli, na Abidjan ikawa mji wa bandari iliyosababisha kukua kwa uchumi na kuongezeka kwa watu.

Abidjan kuna chuo kikuu tangu 1964.

Tangu mwanzo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2004 hali ya usalama mjini umeshuka chini sana.

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Abidjan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: