Uislamu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
d Masahihisho aliyefanya 71.7.235.207 (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na MerlIwBot
Mstari 1: Mstari 1:
'''Waslamu''' (kwa [[Kiarabu]]: الإسلام ''al-islam'') ni [[dini]] inayotokana na mafunzo ya [[Mtume]] [[Muhammad]]. Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,400 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya [[Ukristo]] mwenye wafuasi milioni 2,200.
'''Uislamu''' (kwa [[Kiarabu]]: الإسلام ''al-islam'') ni [[dini]] inayotokana na mafunzo ya [[Mtume]] [[Muhammad]]. Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,400 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya [[Ukristo]] mwenye wafuasi milioni 2,200.


== Imani na kitabu chake ==
== Imani na kitabu chake ==

Pitio la 21:40, 8 Agosti 2011

Uislamu (kwa Kiarabu: الإسلام al-islam) ni dini inayotokana na mafunzo ya Mtume Muhammad. Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,400 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya Ukristo mwenye wafuasi milioni 2,200.

Imani na kitabu chake

Imani ya Waislamu ni kumwamini Mungu mmoja tu anayeitwa Allah. Wana kitabu kitakatifu cha Kurani ambayo wanaamini ilifunuliwa kwa Muhammad kutoka mbinguni kupitia malaika Jibrili; ni kawaida kusema Kurani "iliteremshwa" kwa Muhammad.

Pamoja na Kurani kuna mafundisho ya Sunna na Hadith ambayo ni maneno ya mtume Muhammad na masimulizi juu ya matendo yake ambayo pengine hutazamiwa kama mwongozo katika Uislamu.

Allah kama Mungu pekee ni muumba wa kila kitu. Kurani inasisitiza kwamba hana mshirika, hana baba wala mwana, hakuzaa wala hakuzaliwa, na hana mwanzo wala mwisho.

Pamoja na amri mbalimbali kuna mfumo wa sheria za kidini zinazoitwa kwa jumla "sharia"; inajumlisha maagizo kuhusu mambo mengi ya maisha, uchumi na siasa.

Historia ya chanzo cha Uislamu

Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithihttps://sw.wikipedia.org/w/index.php?search=Ali%20ibn%20Abu%20Talib&title=Maalum%3ATafuta&wprov=acrw1_2
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Muhammad alizaliwa mnamo mwaka 570 BK kama mtoto wa mfanyabiashara mjini Maka uliopo kwenye Bara Arabu.

Kufuatana na mapokeo ya Kiislamu malaika Jibril alimtokea alipokuwa na umri wa miaka 40 yaani mnamo mwaka 610. Kutoka kwa malaika alipokea maneno ya Kurani na ufunuo huu uliendelea hadi mwisho wa maisha yake.

Mtume alitangaza yale aliyosikia kwa wafuasi wake na maneno ya Kurani yalianza kukusanywa tayari wakati wa maisha ya mtume. Baada ya kifo chake mwaka 632 khalifa wa tatu Uthman ibn Affan alikusanya aya zote na kuziweka katika umbo kamili na Waislamu wanafundisha ya kwamba umbo hili halikubadilika tena na ni sawa na yale aliyotangazwa mtume.

Ujumbe uliohubiriwa na Muhammad huko Maka ulipata wasikilizaji wachache, lakini viongozi wengi wa Quraishi, waliokuwa kabila muhimu ya Maka, waliwaona kama hatari kwa Maka na mwaka 622 Waislamu walipaswa kutoka Maka wakahamia Yathrib mji wa jirani.

Uhamisho huu unaitwa hijra na tangu khalifa wa pili Umar ibn al-Khattab ni chanzo cha kalenda ya Kiislamu.

Mjini Yathrib mtume aliendelea kuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi. Alifanya mapatano na watu wa Yathrib iliyoitwa baadaye "madinat an-nabi"" ikajulikana kwa kifupi kama Madina.

Kutoka Madina mtume alianza kushambulia misafara ya watu wa Maka akawashinda mara kadhaa. Wakati huohuo aliwafukuza Wayahudi wa Yathrib.

Mwaka 628 viongozi wa Maka walilazimishwa kufanya mapatano na Waislamu na mwaka 630 jeshi la Waislamu iliingia mjini Maka.

Mtume alipoaga dunia mwaka 632 sehemu kubwa ya Bara Arabu ilikuwa chini ya Uislamu tayari.

Mafunzo ya Uislamu

Uislamu unawafunza wafuasi wake mambo mengi yanayohusiana na maisha, ikiwa yale yanayohusu ibada kama Swala, Zakat, Saumu na Hija; ambazo pamoja na kauli ya Shahada ("Nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hakuna Mola apasaye Kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mtume wake") huitwa nguzo za Uislamu au yale yanayohusu maingiliano baina ya wanadamu, yakiwa maingiliano ya kijamii kama ndoa na talaka na ujirani mwema, au ya kiuchumi kama biashara, au ya kisiasa kama kawaida za kumchagua kiongozi wa dola, au ya uhusiano baina ya mataifa mbali mbali ulimwenguni.

Uislamu unatazamwa kuwa mfumo kamili wa maisha ya binadamu, kiimani, kimaisha, kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Ibada katika Uislamu

Ibada katika Uislamu ni vile vitendo ambavyo Muislamu anamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake, kwani ibada yoyote haitakikani iwe na ushirikina ndani yake, na wakati itakapokuweko aina yoyote ya shirki basi ibada ile inakuwa haina maana wala thawabu wala ujira wowote, ni kazi ya bure.

Kwa hiyo, kila Muislamu anatakikana wakati anapofanya ibada yake afanye kwa ajili ya Mola wake aliyemuumba akampa kila aina ya neema na kumtukuza kuliko viumbe vingine vyovyote, kwa kumpa akili, fahamu na elimu.

Aina za ibada katika Uislamu

Nguzo tano za Uislamu: Nguzo za Uislamu ni tano, na katika madhehebu ya Wasunni wanafundishwa jinsi inavyoonyeshwa hapo chini.

Washia hawahesabu shahada kati ya nguzo tano wakiona shahada pamoja na imani ya Kiislamu ni msingi kwa nguzo tano halafu wanaongeza kama nguzo ya tano .

Nguzo hizo ziliwekwa taratibu katika mwaka ulioonyeshwa katika mabano: shahada (610), sala tano (622), zaka (623), saumu (623), hija (628).

  1. Shahada: Nguzo ya kwanza katika Uislamu hujumuisha kutoa kauli mbili: Hakuna Mola apasaye Kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wake. Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu.
  2. Salat: (kwa Kiarabu: صلاة‎) ni sala inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanya wudhu ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti na dua (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari.
  3. Zakat: Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri.
  4. Funga/Swaum: Wakati wa mwezi Ramadani kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo.
  5. Hija (Kar. الحجّ alhajj): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kufika Maka mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni.

Maingiliano katika Uislamu

Uislamu umeweka kawaida mbali mbali katika maisha wakati watu wanataka kuweka uhusiano fulani baina yao ili mambo yaende vizuri na uhusiano uzidi kuwa mwema baina yao. Katika maingiliano yaliyowekewa kawaida na nidhamu katika Uislamu ni mambo yanayohusu:

1- Nikaha au ndoa baina ya Waislamu 2- Biashara na mambo yanayohusu uchumi 3- Uhusiano wa kijamii baina ya watu katika mtaa au kijiji au mji au nchi 4- Uhusiano wa kimataifa baina ya madola mbali mbali, yakiwa ya kiislamu au yasiyokuwa ya kiislamu.

Vikundi na madhehebu

Kuna mielekeo mikubwa miwili ndani ya Uislamu ambayo ni vikundi vya Wasunni na Washia.

Kundi kubwa ni Wasunni waliopata jina kutokana na Sunna ("kawaida") ya mtume; takriban asilimia 85-90 ya Waislamu wote huhesabiwa humo. Kati yao kuna madhehebu 4 ambao ni Hanafi, Maliki, Hanbali na Shafii. Tofauti katika mafundisho si kubwa, zinahusu hasa sharia na fikh.

Kundi dogo zaidi ni Washia ambao wamegawanyika kati yao katika vikundi vingi. Washia walijitenga na Wasunni baada ya makhalifa wanne wa kwanza kuhusu swali ni nani anayefaa kuongoza Waislamu. Washia ni wale waliosisitiza sharti awe mtu kutoka ukoo wa Muhammad kupitia binti yake Fatima. Vikundi vya Washia vinatofautiana juu ya viongozi hawa. Jumuiya kubwa ya Washia ni Ithnashara walio wengi huko Uajemi, Irak na Lebanoni.

External Links

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA