NASA : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: nap:NASA
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: be:НАСА
Mstari 27: Mstari 27:
[[az:NASA]]
[[az:NASA]]
[[bat-smg:NASA]]
[[bat-smg:NASA]]
[[be:НАСА]]
[[be-x-old:NASA]]
[[be-x-old:NASA]]
[[bg:НАСА]]
[[bg:НАСА]]

Pitio la 16:36, 5 Agosti 2011

NASA ni kifupi cha Kiingereza cha "National Aeronautics and Space Administration" (Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga). Mamlaka hii ilianzishwa 1958. Wajibu wake ni kusimamia miradi ya serikali ya Marekani ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. NASA inatawala utengenezaji wa roketi za kurusha vyombo vya angani na vyombo vya angani vyenyewe.

Roketi iliyorusha "Freedom 7" na Alan Shepard Jr.angani tar. 5.5.1961

Miradi ya NASA ilianzishwa kutokana na Mshtuko wa Sputnik yaani baada ya Warusi kushtusha dunia kwa kupeleka vyombo vya angani vya kwanza katika mradi wao wa Sputnik. Ulifuatwa na mradi wa "Vostok" ambao tarehe 12 Aprili, 1961 ulimfikisha Yuri Gagarin angani akiwa mtu wa kwanza huko kwenda angani.

Mradi wa kwanza wa NASA ulikuwa Mradi wa Mercury uliotakiwa kuonyesha ya kwamba wanaanga wanaweza kukaa angani kwa muda fulani. Alan B. Shepard Jr. alikuwa Mmarekani wa kwanza angani kwa muda wa dakika 15; John Glenn alikuwa Mmarekani wa kwanza wa kuzunguka dunia tarehe 20 Februari, 1962 kwa chombo cha angani "Friendship 7".

Mradi huo ulifuatwa na Mradi wa Gemini kuanzia mwaka 1965 ulionyesha ya kwamba watu wanaweza kukaa angani kwa muda wa siku kadhaa hata kutekeleza shughuli fulani. Gemini iliandaa Mradi wa Apollo uliopeleka watu wa kwanza mwezi. Chombo cha angani "Apollo 11" kilifikisha wanaanga Neil Armstrong na Buzz Aldrin kwenye uso wa mwezi tarehe 20 Julai, 1969 na kuwarudisha dunia tena.

Kutoka mwanzo ule kuna miradi mingi iliyofuata.

Buzz Aldrin akitembea kwenye uso wa mwezi wakati wa safari ya Apollo 11.

Viungo vya nje

Kigezo:Link FA