Hifadhi ya Serengeti : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 111: Mstari 111:
[[th:อุทยานแห่งชาติเซเรงเกติ]]
[[th:อุทยานแห่งชาติเซเรงเกติ]]
[[tr:Serengeti Milli Parkı]]
[[tr:Serengeti Milli Parkı]]
[[uk:Серенгеті]]
[[uk:Національний парк Серенгеті]]
[[vi:Vườn quốc gia Serengeti]]
[[vi:Vườn quốc gia Serengeti]]
[[zh:塞伦盖蒂国家公园]]

Pitio la 09:22, 1 Agosti 2011

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

katika Hifadhi ya Serengeti
Mahali pa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
MahaliTanzania
Coordinates

2°19′58″S 34°34′0″E / 2.33278°S 34.56667°E / -2.33278; 34.56667Coordinates: 2°19′58″S 34°34′0″E / 2.33278°S 34.56667°E / -2.33278; 34.56667{{#coordinates:}}: cannot have more than one primary tag per page

Eneo14,763 km2
Kuanzishwa1951
Ramani ya Tanzania Kaskazini pamoja na Serengeti
Pundamilia na nyumbu wakati wa uhamaji
Machweo ya Serengeti

Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la savana na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na Kenya. Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.

Kuna idadi kuba ya wanyama wa pori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aini nyingi nyingine za wanyama kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.

Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya wanadamu wa kale kabisa yalipatikana liko ndani ya Serengeti.

Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia iko katika kaskazini-magharibi ya Tanzania na inaenea kwa kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. Ina enea kiwango cha mraba kilometa 30,000 2.

Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi duniani,[1] ambao hua ni tukio wa nusu mwaka . Uhamiaji huu ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu ya kusafiri.

Kanda hii ina hifadhi za taifa na hifadhi mchezo kadhaa. Serengeti imechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai, Maa; hasa, "Serengit" kumaanisha "Kiwara kisichoisha". [2] [3]

Inakadiriwa mamalia 70 kubwa na baadhi ya spishi 500 avifauna (yaani ndege) hupatikana huko. Tofauti huu wa juu upande wa spishi ni shughuli makazi mbalimbali kuanzia misitu ya riverine, mabwawa, kopjes, mbuga na misitu. [4] Nyumbu bluu, swara, punda milia na nyati ni baadhi ya mamalia kubwa ambao kwa kawaida hupatikana katika kanda hili.

Karibu Oktoba, karibu herbivores (yaani wanyama wanaokula majani badala ya nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za mvua. Katika mwezi wa Aprili, wao hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena kuvuka Mto wa Mara. Jambo hili kwa mara huitwa "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu zaidi ya 250,000 peke watakufa safarini kutoka Tanzania kwenda katika mbuga ya wanyama ya Masai Mara huko Kenya pande za juu, ambayo ni jumla ya maili 500. Kifo mara nyingi unasababishwa na maudhi au uchovu. [1] Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani.

Historia

Mvulana wa kimaasai (Moran au warrior) anatembea ndani ya Serengeti na miinuko ya Ngorongoro kama bakgrund.

Upande mkubwa wa Serengeti hapo awali ulijulikana kama Maasailand kwa wageni. Wamasai walijulikana kama shujaa wakali , na waliishi pamoja na wanyama wa pori huku wakiishi kwa kuwala mifugo yao pekee. Nguvu zao na sifa zilisababisha wasafiri kutoka Ulaya kutotumia wanyama na rasilimali ya nchi yao vibaya. Janga la "rinderpest" na ukame wakati wa 1890 ulisababisha upungufu wa idadi ya Wamaasai na wanyama. Uwindaji haramu ya wanyama wa pori na ukosefu wa moto, ambayo yalikuwa matokeo ya shughuli za binadamu, yaliweka hatua ya maendeleo ya misitu na vichaka kwa miaka 30-50 ijayo. Uongezekaji wa chafuo sasa ulisababisha kutokuwa kwa makaazi ya binadamu katika eneo hili. Moto, tembo, na nyumbu walikuwa na ushawishi mkubwa katika kuamua sasa muundo wa Serengeti. [5] Mnapo miaka ya 1960, idadi ya binadamu ilivyoongezeka, moto, aidha kuwashwa kwa makusudia na Wamaasai ili kuongeza eneo ya malisho ya mifugo, au kwa ajali, ulisababisha kuchomeka kwa miche mpya ya miti. Mvua nzito ulichangia ukuaji wa majani, ambao ulikuwa kama mafuta kwa moto wakati wa misimu kavu zifuatazo. Miti mzee ya Acacia, ambayo huishi tu miaka 60-70, yalianza kufa. Awali tembo, ambao hula miti changa na mzee, amekuwa walilaumiwa kwa kumaliza misitu. Lakini majaribio ilionyesha kuwa kulikuwa na sababu nyingine muhimu zaidi. Wakati huo huo, idadi ya tembo ilipunguzwa kutoka 2,460 mwaka 1970 hadi 467 katika mwaka wa 1986 kwa uwindaji haramu. [6] Mnapo miaka ya 1970 idadi ya nyumbu na nyati ya Afrika ilikuwa imeongezeka, na walikuwa wakipunguza idadi ya majani kwa kasi, basi kusababisha upuingufu wa mafuta ya kusambazaa moto. [7] kupunguka kwa ukali wa moto umesababisha Acacia kuwa imara tena. [5]

Ecology

Bara la Maasai ina mbuga ya wanyama bora zaidi Afrika Mashariki. [8] Serikali ya Tanzania na Kenya hutunza idadi kadha ya maeneo yaliyochunwa: mbuga, maeneo ya hifadhi, mapori ya akiba, nk, ambayo hutoa ulinzi wa kisheria kwa zaidi ya 80% ya Serengeti. [9]

Ol Doinyo Lengai, ikiwapo mlima wa moto ulio bado na uhai katika eneo la Serengeti, ni mlima wa moto pekee ambao bado hutoa "carbonatite lava". "Carbonatite lava", unapo fichuliwa kutoka kwa hewa, hubadilisha rangi kutoka samawati hadi nyeusi na kufwanana na "washing soda". Tabaka nzito ya jivu unaweza geuka kuwa hardpan iliotajirika na kalsiamu ngumu kama saruji baada ya kunyeshewa. Mizizi ya mti haiwezi kupenya safu hii, na kimsingi tambarare bila miti ya Serengeti, ambayo yako magharibi na upepo chini ya Ol Doinyo Lengai, ni matokeo. [10]

Miinuko ya mwamba, au "koppes", katika tambarare ya Serengeti.

Eneo la Kusini-Mashariki ambalo lipo katika kivuli mvua ya miinuko ya Ngorongoro na linajumuisha tambarare lenya majani mafupi bila miti na "dicot" tele ndogo ndogo. Udongo yana rutuba kwa wingi, yakiwa juu ya "calcareous hardpan" fupi. "Gradient" ya urefu wa udongo kaskazini-mashariki ukipita tambarare husababisha mabadiliko katika jamii na herbaceous na nyasi refu. Baadhi ya 70 km magharibi, misitu ya Acacia huonekana ghafla na kunyoosha magharibi kuelekea ziwa Victoria na kaskazini kelekea katika tambarare za Loita,[onesha uthibitisho] kaskazini mwa mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Maasai Mara. Aina 16 tofauti ya Acacia yapo katika msitu huu, usambazaji wao ukiamuliwa na hali "edaphic" na urefu wa udongo. Karibu na Ziwa Victoria kuna tambarare yenye mafuriko yaliyitokana na "lakebeds" za kale. Katika kaskazini magharibi, misitu ya Acacia yamebadilishwa na misitu ya "Terminalia-Combretum" yenye majani mapana, uliodhamiria kutokana na mabadiliko katika geologi. Eneo hili lina kiwango cha juu zaidi ya mvua katika mfumo na huunda kimbilio kwa kwa wanyama wanaohama mwisho wa msimu wa kiangazi. [11]

Muinuko katika Serengeti huanzia mita 920 hadi 1850 na joto wastani kuanzia digrii 15 hadi digrii 25 "Celsius". Ingawa kwa kawaida hali ya hewa huwa joto na kavu, mvua hutokea katika misimu miwili ya mvua: Machi-Mei, na msimu mfupi katika Oktoba na Novemba. Kiasi cha mvua inatofautiana kutoka kiwango cha chini cha 508 mm katika upande wa "lee" ya miinuko ya Ngorongoro na kiwango cha juu cha 1,200 mm katika pwani ya Ziwa Victoria. [12] Nyanda za juu, ambazo ni baridi kuliko tambarare na kufunikwa na misitu ya "montane", ndio alama ya mpaka wa mashariki ya bonde ambayo Serengeti uko.

Tambarare la Serengeti wazi ina miinuko ya "granite" inayojulikana kama "koppes". Miinuko haya ni matokeo ya shughuli kutokana na volkeno. "Koppies" hutoa makazi madogo kwa nyanda zisizo wanyamapori. "Koppe" moja unao uwezekano kuonekana kwa wageni huko Serengeti ni Simba Koppe (Lion Koppe). Serengeti ilitumika kama jukwaa utengeneza filamu ya "Disney" ya The Lion King na baadae uvumbuaji wa filamu za jukwaa.

Eneo hilo pia ni nyumbani kwa eneo lililohifadhiwa la Ngorongoro, ambayo ina "Olduvai Gorge", ambapo baadhi ya "hominid fossils" kongwe hupatikana, vilevile pia "Ngorongoro Crater", caldera ya volkeno kubwa zaidi ulimwenguni.

Marejeo

  1. 1.0 1.1 Partridge, Frank. "The fast show", The Independent (London), 2006-05-20. Retrieved on 2007-03-14. 
  2. Northern Tanzania with Kilimanjaro and Zanzibar, by Phillip Briggs, 2006, page 198. ISBN 1841621463.
  3. Maa (Maasai) Dictionary
  4. 403 Forbidden
  5. 5.0 5.1 Serengeti II: Dynamics, Management, and Conservation of an Ecosystem. Anthony Ronald Entrican Sinclair, Peter Arcese. 1995. University of Chicago Press. Kurasa 73-76. ISBN 0226760316.
  6. Serengeti II. Sinclair, Arcese. Ukurasa 76. ISBN 0226760316.
  7. http://www.sciencemag.org/cgi/content/full/278/5346/2059
  8. Africa's Great Rift Valley. Nigel Pavitt. 2001. Ukurasa 122. Harry S. Abrams, Incorporated, New York. ISBN 0-8109-0602-3.
  9. http://64.233.169.104/search?q=cache:rss9ABx99HUJ:www.ath.aegean.gr/srcosmos/showpub.aspx%3Faa%3D8868+serengeti+ecosystem+kenya&hl=en&ct=clnk&cd=4&gl=us
  10. Africa's Great Rift Valley. Pavitt, kurasa 130, 134.
  11. http://209.85.207.104/search?q=cache:j9xvfWrq0L0J:www.uoguelph.ca/ib/pdfs/Sinclair_2007_ConsBiol.pdf+acacia+trees+serengeti+fire&hl=en&ct=clnk&cd=6&gl=us
  12. http://www.glcom.com/hassan/serengeti.html

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Coordinates: 2°19′51″S 34°50′0″E / 2.33083°S 34.83333°E / -2.33083; 34.83333{{#coordinates:}}: cannot have more than one primary tag per page