Usanisinuru : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.5) (roboti Badiliko: war:Fotosintesis
Mstari 71: Mstari 71:
[[jv:Fotosintesis]]
[[jv:Fotosintesis]]
[[ka:ფოტოსინთეზი]]
[[ka:ფოტოსინთეზი]]
[[kk:Фотосинтездің жарық және қараңғы фазалары]]
[[kn:ದ್ಯುತಿಸಂಶ್ಲೇಷಣೆ]]
[[kn:ದ್ಯುತಿಸಂಶ್ಲೇಷಣೆ]]
[[ko:광합성]]
[[ko:광합성]]

Pitio la 06:38, 1 Agosti 2011

Kila jani kina kiwanda cha kikemia ndani yake

Usanisinuru ni mchakato wa kibiolojia na kikemia ambako mimea ya kijani inageuza nguvu ya nuru ya jua kuwa nishati ya kikemia. Inatengeneza kabohidrati ikitumia nguvu ya nuru ya jua na dioksidi kabonia ya hewani pamoja na maji.

Nje ya mimea kuna pia aina kadhaa za bakteria na hasa mwani zinazofanya usanisinuru.

Fomula yake ni

6 CO2 + 12 H2O + nuru → C6H12O6 + 6 O2 + 6 H2O
dioksidi kabonia + maji + nishati nuru → glukosi + oksijeni + maji

Usanisinuru ni msingi wa maisha yote duniani. Unajenga mada ogania ambayo ni chanzo cha lishe katika mtando chakula kwa karibu viumbe vyote vingine kwa njia moja au nyingine. Kwa njia hii ni chanzo cha mtando chakula wa uhai wote wa kibiolojia.

Mchakato wa usanisinuru

Picha ya kiwiti (chloroplast)

Usanisinuru unaanza kwenye sehemu za kijani za majani. Rangi ya kijani inatokana na punje ndogo sana za kiwiti ndani ya majani. Wakati nuru ya jua inafikia kiwiti inasababisha kemikali ndani yake kuvunja molekuli za maji. Molekuli ya maji ikivunjwa inatoa oksijeni, hidrojeni na nishati. Protini ndani ya seli inatumia dutu hizi pamoja na dioksidi kabinia ya hewani kujenga glukosi na ATP ambayo ni molekuli ya fosifati inayotunza nishati nyingi ndani ya muungo kemia wake.

Katika mchakato huu oksijeni inaachishwa na hivyo usanisinuru ni pia chanzo cha angahewa ya dunia jinsi ilivyo na oksijeni nyingi.

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Usanisinuru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA