Jicho : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.2) (roboti Badiliko: nah:Īxtelolotl
d r2.6.4) (roboti Nyongeza: lbe:Я (чурх)
Mstari 101: Mstari 101:
[[la:Oculus]]
[[la:Oculus]]
[[lb:A (Sënnesorgan)]]
[[lb:A (Sënnesorgan)]]
[[lbe:Я (чурх)]]
[[ln:Lǐso]]
[[ln:Lǐso]]
[[lt:Akis]]
[[lt:Akis]]

Pitio la 19:25, 25 Julai 2011

Jicho la binadamu
Macho ya kuungwa ya inzi

Jicho ni sehemu ya mwili inayotuwezesha kuona. Ni ogani inayotambua mwanga na kutuma habari zake kwa ubongo.

Aina za macho ya viumbehai

Kuna mifumo mbalimbali ya macho kati ya aina mbalimbali ya wanyama.

Macho ya kimsingi kwa viumbehai vidogo yanatambua tu kama mazingira ina mwanga au la. Hata kati ya wenye seli moja hu kuna viumbehai vyenye protini zinazotofautisha giza na nuru. Kuna konokono ambao hawawezi "kuona" picha ya mazingira lakini wanatambua mwanga na uwezo huu unawawezesha kuepukana na mwanga wa jua ambako wangekauka.

Macho yaliyoendelea kiasi yana umbo kama kikombe na hii inawezesha kutambua ni upande gani nuru inapotokea.

Wanyama wengi huwa na macho yaliyoendelea zaidi yana uwezo wa kuona picha halisi ya mazingira pamoja na rangi na mwendo.

Jicho la inzi (drosophila) chini ya hadubini; lenzi ya kila omatidi inaonekana kama nusu tufe

Macho ya kuungwa

Wadudu na arthropoda hua na macho ya kuungwa na vijicho vingi vidogo vinavyoitwa omatidi; kila kijicho huwa na umbo la kijiti na kwenye mwisho wake kuna lenzi ya chitini. Mdudu anaweza kuwa na vijicho vielfu na picha ya mazingira inaunganishwa na picha nyingi ndogo za kila kijicho. Macho haya ya kuungwa yanamwezesha mdudu kuangalia asilimia kubwa ya mazingira yake kwa aina kadhaa hata nyuma yake. Macho ya kuungwa yanaweza kufunika hadi asilimia 80 ya eneo la kichwa. Mdudu haoni vikali kama mtu lakini anaona mabadiliko na mwendo haraka sana.

Wanyama wanaoishi katika vilindi vya bahari penye giza huwa na macho ambamo fuwele ziko kama kioo na kupazia nuru hafifu.

Kuna wanyama wanaoweza kuona nuru ambayo ni nje ya upeo ya kibinadamu kwa mfano nyuki huona mnururisho wa infraredi.

Macho ya mamalia

Macho ya binadamu kama ya mamalia huwa na lenzi moja tu. Lakini muundo wa jicho unaruhusu kuona rangi, umbali na mengi madogo.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jicho kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA