Bomu la nyuklia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 142: Mstari 142:
[[oc:Arma nucleara]]
[[oc:Arma nucleara]]
[[pl:Broń jądrowa]]
[[pl:Broń jądrowa]]
[[pnb:ایٹم بم]]
[[pnb:ایٹم بمب]]
[[pt:Bomba nuclear]]
[[pt:Bomba nuclear]]
[[qu:Iñuku huk'i ayñi]]
[[qu:Iñuku huk'i ayñi]]
Mstari 153: Mstari 153:
[[sl:Jedrsko orožje]]
[[sl:Jedrsko orožje]]
[[sq:Armët bërthamore]]
[[sq:Armët bërthamore]]
[[sr:Нуклеарно оружје]]
[[sr:Атомска бомба]]
[[su:Pakarang nuklir]]
[[su:Pakarang nuklir]]
[[sv:Kärnvapen]]
[[sv:Kärnvapen]]

Pitio la 06:15, 20 Julai 2011

Mlipuko wa bomu ya kinyuklia ya jaribio huko Nevada (Marekani) mwaka 1951.

Bomu la nyuklia ni silaha inayosababisa mlipuko mkubwa sana. Kati ya silaha zote ni yenye nguvu na pia yenye hatari zaidi.

Misingi ya kifizikia

Nishati ya mlipuko huu yatokana na mmenyuko mfululizo wa kinyuklia ambayo ni ama

Katika mmenyuko wa kinyuklia sehemu ya mada ya atomi hugeuzwa kuwa nishati.

Mabomu ya kawaida hutumia nishati ya mmenyuko wa kikemia ambamo viini atomia havibadiliki.

Aina za mabomu ya nyuklia

Kutokana na aina mbili za mmenyuko wa kinyuklia kuna aina mbili za silaha zinazoitwa:

Mabomu atomia hutengenezwa kwa kutumia urani au plutoni. Isotopi za elementi hizi zafaa kupasuliwa na kuingia katika hali ya mmenyuko mfululizo.

Mafundi wakimaliza maandalizi ya bomu la Hiroshima mwaka 1945

Mabomu ya hidrojeni yatumia isotopi za hidrojeni hasa deuteri na triti inayoungana kuwa heli. Mmenyuko huu huanzishwa kwa mlipuko wa bomu atomia ndani ya bomu ya hidrojeni. Nishati ya mabomu ya hidrojeni yapita kiwango cha mabomu atomia mara 100.

Uharibifu

Kama kila bomu silaha hizi zaleta uharibifu kwa njia ya

  • joto inayoangamiza
  • shindikizo inayovunja na kumega vitu vya mazingira katika upeo wake.

Kutokana na nishati kubwa inayopatikana matokeo yote mawili hushinda silaha za kawaida zinazotumia nishati ya kikemia tu.

Mabomu ya nyuklia zina tokeo la ziada ni

  • mnururisho inayoharibu vyembehai vya viumbe na mimea inayoathiriwa nayo.

Uwezo wa silaha hizi

Nishati inayopatikana kwa njia ya mmenyuko mfululizo wa kinyuklia ni kubwa sana. Bomu moja ya nyuklia yatosha kuharibu mji kabisa jinsi ilivyotokea mwaka 1945 huko Hiroshima na Nagasaki. Mabomu ya 1945 yalikuwa madogo sana kuliko mabomu yaliyotengenezwa baadaye.

Tangu Nagasaki hakuna bomu nyingine lililotumiwa vitani. Milipuko yote iliyofuata ilikuwa ya jarabio tu ama jangwani au baharini pasipo na watu. Nchi zote ziliogopa uharibifu mkubwa kupita kiasi ingawa hasa nchi kubwa za Marekani na Urusi ziliendelea kutengeneza maelfu ya mabomu.

Giza na baridi

Tangu miaka ya 1980 imejulikana ya kwamba milipuko ya robo hadi nusu ya silaha za nyuklia zilizokuwepo tayari ingetosha kumaliza maisha duniani kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ingetokea kwa sababu ya kiasi kikubwa cha vumbi kinachorushwa hewani na milipuko hii. Vumbi hiyo ingejaza anga na kuzuia nuru ya jua kufika kwenye uso wa dunia hivyo kusababisha giza pamoja na kushuka kwa halijoto kwa muda wa miaka kadhaa.

Mnururisho

Hatari nyingine inayojulikana ni mnururisho wa kinyuklia. Imejulikana kutokana na milipuko ya kwanza ya 1945 na majaribio ya baadaye ya kwamba ya kwamba watu na wanyama hufa kutokana na ugonjwa nururifu wakiathiriwa na kiasi kikubwa cha mnururisho au kupata kansa baadaye kwa wingi. Mnururisho huo hukaa kwa muda wa miaka katika ardhi pia hukusanyika na mimea hasa katika matunda na nafaka. Kwa njia hii yaathiri tena watu wanaotumia mimea hii au wanyama wanaotumia mimea yale kama chakula.

Imekadiriwa ya kwamba milipuko mingi katika vita atomia ingesababisha kiasi cha mnururisho kitakachobebwa na mawingu na upepo hadi pembe za dunia na kupeleka kifo hata pale pasipo na vita.

Nchi zenye silaha za nyuklia
nyekundu – Nchi tano za kwanza zenye silaha za nyuklia zilizopatana kutosambaza teknolojia;
njano nyeusi – Nchi nyingine zinazojulikana kuwa na nazo;
dhambarau – Nchi zilizokuwa nazo zikaziondoa;
buluu - nchi zinazojulikana zilikuwa na miradi ya utafiti wa silaha hizi zamani lakini bila kutengeneza;
njano – Nchi zinazoshtakiwa kuwa zinaendesha utafiti wa kujenga silaha za nyuklia kwa siri;
dhambarau nyeupe – Korea ya Kaskazini ilianza kutengengeneza silaha za nyuklia lakini ikapumzisha mradi;

Teknolojia ya kufyatua mabomu ya nyuklia

Kuna hasa namna mbili za kufikisha mabomu haya panapolengwa:

  • ndege za kivita
  • roketi

Kuna pia mabomu madogo yanayoingizwa katika makombora ya mizinga.

Palikuwa pia na mabomu atomia yanayofichwa kama bomu ardhini.

Nchi zenye mabomu ya nyuklia

Nchi ya kwanza iliyotengeneza mabomu haya ilikuwa Marekani. Ilifuatwa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia na Umoja wa Kisovyeti, Uingereza na Ufaransa. Baada ya China kuwa na bomu hii pia tangu 1964 nchi hizi tano zilijaribu kubana usambazaji wa silaha hizi kwa mkataba wa kimatifa.

Lakini nchi kadhaa ziliendelea kufanya utafiti na kugundua mbinu za kutengeneza silaha hzi kama vile Uhindi (1974) na Pakistan (1998). Afrika Kusini ilikuwa na silaha za kinyuklia lakini zimebomolewa baada ya mwisho wa apartheid.

Wataalamu wengi huona kuwa Israel ina pia mabomu haya lakini nchi haijawahi kukubali kama zipo. Korea ya Kaskazini ililipusha bomuy a kwanza ya majaribio mwaka 2006 lakini imetangaza baadaye ya kwamba haitaendelea.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bomu la nyuklia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tovuti za Nje

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA