Biashara ya watumwa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
dNo edit summary
Mstari 32: Mstari 32:
[[ru:Работорговля]]
[[ru:Работорговля]]
[[simple:African slave trade]]
[[simple:African slave trade]]
[[uk:Работоргівля]]

Pitio la 06:23, 24 Juni 2011

Kusafirisha watumwa katika Afrika ya karne ya 19
Soko la watumwa katika Roma ya Kale (picha ya karne ya 19)

Biashara ya watumwa ni biashara inayohusu watumwa yaani watu wasio huru wakitazamiwa kuwa mali ya wengine.

Katika historia ilitokea mara nyingi. Uchumi wa Roma ya Kale ilitegemea watumwa waliokamatwa na kusafirishwa kati ya pande zote za mazingira ya Bahari Mediteranea. Milki za makhalifa wa Uislamu ziliendelea kutegemea watumwa. Waosmani walichukua watoto wa kikristo kutoka nchi za Balkani na kuwapeleka kama watumwa katika sehemu za kusini za milki yao kama Misri walipofanya kazi za wanajeshi.

Mahitaji ya uchumi wa kimataifa tangu karne ya 15 yalisababisha kuongezeka kwa biashara ya watumwa hasa kutoka Afrika; mamilioni walikamatwa na watawala wa milki kwenye pwani za Afrika na kuuzwa kwa wafanyabiashara wazungu waliowapeleka Amerika walipohitajika kwa kazi kwenye mashamba makubwa ya miwa na pamba.

Biashara hii ilianza kupingwa tangu mwisho wa karne ya 18; Mkutano wa Vienna (1814-15) ilikuwa mapatano ya kwanza ya kimataifa yaliyolenga kukataa biashara ya watumwa kutoka Afrika.

Hata hivyo yaliendelea kwa miaka kadhaa hasa upande wa bahari Hindi ambako wanafayabiashara kama Tippu Tip waislamu waliendelea kukamata watumwa na kuwapeleka pwani.

Ukoloni ulimaliza biashara hii pia.

Tangu karne ya 20 utumwa na pia biashara ya watumwa zimepigwa marufuku katika mapatano ya kimataifa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Lakini miaka za nyuma imeona biashara mpya inayotumia nafasi za usairi wa kisasa; hata kama hakuna utumwa kisheria tena duniani ni hasa wanawake na mabinti wanaouzwa kwa kazi haramu ya ukahaba kati ya nchi na nchi.